Siku unapogundua jinsi teknolojia inayoweza kuipa dunia umeme wa bure na kufuta matumizi ya mafuta inavyoweza kugeuka amri ya kifo kwa mvumbuzi wake, ndipo utakapoelewa ukatili wa biashara ya trilioni za dola.
Katikati ya miaka ya 2010, mhandisi kutoka Zimbabwe, Sangulani Maxwell Chikumbutso, alitikisa ulimwengu wa sayansi baada ya kutangaza uvumbuzi uliodaiwa kuvunja sheria za fizikia: mfumo wa Micro-Acoustic Energy Transducer (MSET).
Chikumbutso alitengeneza teknolojia inayokusanya mawimbi ya redio (radio frequency waves) yanayoelea angani na kuyabadilisha kuwa umeme wa bure usioisha.
Ili kuthibitisha hili mbele ya dunia:
Alionyesha gari la umeme linalojiendesha kwa mawimbi hayo—bila kuhitaji kuchajiwa wala kutumia mafuta. Iko hivi yeye hakutengeneza hilo gari mwanzo mwisho, ila kuna kampuni ya kichina ndo ilitengeneza yeye akaliwekea hiyo mifumo ya bila kutumia umeme wa kuchaji wala mafuta
Alionyesha mfumo wa umeme unaoweza kuwasha nyumba nzima bila mafuta au waya za serikali za kutoka grid ya taifa.
Teknolojia hii ilitakiwa kuikomboa Afrika kutoka kwenye giza la umeme na utumwa wa mafuta. Lakini badala yake, dhoruba ya kutisha ikamlipukia:
Uvumbuzi huo ulipoanza kuteka vyombo vya habari, Chikumbutso alilishwa sumu kali na watu wasiojulikana. Alinusurika kifo kwa muujiza baada ya kulazwa hospitalini kwa muda mrefu huku afya yake ikiharibika vibaya. Hili lilimpata akiwa Marekani.
Mabaraza ya kimataifa ya hati miliki yaligoma kusajili uvumbuzi wake, yakidai unapingana na "Sheria ya Pili ya Thermodynamics."
Alianza kupokea vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa majasusi wa makampuni makubwa ya mafuta. Hakuna kampuni yoyote kubwa iliyokubali kuwekeza ili gari hilo litengenezwe kwa wingi.
Biashara ya mafuta na magari inazungusha trilioni za dola. Teknolojia inayotoa nishati ya bure ni tishio la moja kwa moja kwa utajiri wa mataifa makubwa na mabepari wa dunia.
Je, unaamini wavumbuzi kama Chikumbutso wanazimiwa taa kwa sababu wanatishia maslahi ya mataifa makubwa.
Nakumbuka pia, kuna jamaa miaka ya nyuma aliwezaga kutengeneza bunduki, na ikawa inaweza kurusha risasi zile za gobore, asee Siku polisi walipata taarifa, jamaa alichezea kichapo na maonyo ya kutosha, sidhani kama atawai kurudia, huku ni kuua vipaji kwa sisi wenyewe pia, kabla ya kulaumu wazungu.