Muajiri ana haki kujua hali yako ya hiv?

Muajiri ana haki kujua hali yako ya hiv?

TWANJUGUNA

Member
Joined
Jun 6, 2010
Posts
28
Reaction score
1
Ingawa ki-sheria, muajiri hana haki kujua hali ya mfanyakazi wake, waonaje kumuachia mtoto wako yaya usiyejua hali yake ya HIV?
 
Mwajiri ana haki ya kujua status ya mwajiriwa! sio tu wafanyakazi wa ndani, ni maeneo yote ya kazi! Hii ina imply hata ukiajiri taahira ujue kiwango chake cha utahira..., kiwete kwa mfano, ni lazima ujue na uelewe ni mazingira yapi anayoweza fanyia kazi kutokana na hali yake! Na ndio maana kwenye mikataba ya kazi cheti cha kuonyesha uimara au udhoofu wa afya yako ni mhimu!
 
Ingawa ki-sheria, muajiri hana haki kujua hali ya mfanyakazi wake, waonaje kumuachia mtoto wako yaya usiyejua hali yake ya HIV?

Yes anatakiwa kujua ili aweze kukusaidia na si kukuangamiza au kukudhalilisha ila pawe na makubaliano ya hiari na sim kulazimishwa
 
Huwezi kumlazimisha mtu akuambie status yake ndio umpe ajira. HIV status ni siri ya mtu binafsi.
Tafuta mtu matured (ambaye hatamnyonyesha infant wako wakati wewe haupo ku-test inakuwaje), ila nakushauri usiwapime mahausigeli, wengi wameathirika na utashindwa kufanya kazi zako uamue kulea mwenyewe. Nakupa ushauri wa bure huo, kama hauamini hiyo ni juu yako.
 
Mwajiri ana haki ya kujua status ya mwajiriwa! sio tu wafanyakazi wa ndani, ni maeneo yote ya kazi! Hii ina imply hata ukiajiri taahira ujue kiwango chake cha utahira..., kiwete kwa mfano, ni lazima ujue na uelewe ni mazingira yapi anayoweza fanyia kazi kutokana na hali yake! Na ndio maana kwenye mikataba ya kazi cheti cha kuonyesha uimara au udhoofu wa afya yako ni mhimu!

Hairuhusiwi kisheria kupekenyua status ya mtu, mfano kumpima kwa siri, unless una consent yake.
 
hali ya afya ya mtu ni makubaliano ya hiari kati ya mwajiriwa na mwajiri
na inapobainika kuwa umempima mtu kwa siri!!akikushtaki utamlipa fidia ujute maishani
including HIV ni siri ya mhusika tu labda aamue yeye mwenyewe kujulisha umma!!
wasaidizi wa kazi ni vizuri mshauriane nao wapime afya zao hasa kama anaangalia watoto,maana kuna magonjwa mengine ni hatari sana mf kifafa,kichaa,ngozi nk...
 
Back
Top Bottom