Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tukio la mmoja ya waandamanaji wa kike ambaye jina lake halijafahamika, akamatwa na Polisi alipokuwa akifanya maombi, eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam.
Septemba 11, 2024 Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe alitangaza kufanyika maandamano ya kulaani matukio ya watu kutekwa na kuuawa, akiwemo aliyekuwa kada wake, Ali Kibao. Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, David Misime lilitangaza kuyapiga marufuku.
Kwa mujibu wa Mbowe, wameamua kuweka mkazo wa suala hilo, baada ya maombi ya mahitaji, ikiwemo kutaka kujiuzulu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni, viongozi waandamizi wa ulinzi na usalama kama sehemu ya uwajibikaji.