SoC04 Muarobaini wa rushwa

SoC04 Muarobaini wa rushwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

usshindi

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
5
Reaction score
10
Adui wa haki kwa miaka yote ni rushwa.rushwa limebaki kua fumbo zito kwa nchi nyingi duniani kulitatua ikiwemo nchi yangu pendwa Tanzania, ni Imani yangu kama usipopatikana muafaka wa hili suala ni wazi hatuwezi kufikia Tanzania tunayoitaka.

Kuna wakati nimekua nikikaa nikitafakari jinsi nchi yangu inavyoyakosa mAendeleo kwa sababu ya rushwa naona kabisa tuna mwendo mrefu mpaka kufikia nchi tunayoitamani.

Wakati nikiwaza njia Bora ya kuondokana na rushwa nilipata mawazo mengi ya aina tofauti tofauti ya kuisaidia nchi yangu kuondokana na rushwa mawazo mengi yalkua na ugumu kutelelezwa na mawazo machache yalionekana kua na wepesi kutekelezeka nikianza na mawazo niliyoyaona ni magumu kutekekezwa lakini ni rahisi kuzuia rushwa kwayo ni

Matumizi ya teknolojia ya CCTV camera na gps kwa watendakazi wa serikali na ofisi zao hawa ndio watu tunaowategemea kwa asilimia kubwa kuleta mAendeleo kama serikali ikiweza kufunga CCTV camera katika Kila ofisi za serikali na kuweka gps kwenye mifumo ya mawasiliano ya viongozi hao ni Imani yangu kua rushwa itapunguzwa kwa asilimia kadhaa ofisi hizo inapaswa ziwe zote ikiwemo ofisi za maaskari wa usalama barabarani yaani maeneo ambayo husimama kuzuia gari kwa ajili ya ukaguzi yafungwe CCTV pia mfumo wa gps uunganishwe ngazi zote mpaka taifani Ili atambulike mhusika kwa urahisi kwa kuwa kama ikiachwa kwa miunganiko ya ngazi ndogo ndogo kama halmashauri kuna uwezekano rushwa ikatumika pia kulizima suala Hilo kwa kununua mikanda na mambo mengine ugumu wa suala hili nilivouona kwangu ni sauala la bajeti kwa vile bajeti ya nchi yangu haijatanuka sana suala

Hili linaweza kupata changamoto sana kutimizwa ukichukulia mahitaji ya msingi ya wananchi kama umeme,maji na mengineyo hayajatimizwa. Kama serikali itatimiza mahitaji ya msingi ya wananchi wa Tanzania kama umeme kupatikana vitongoji na mitaa yote nchini na maji kupatikana nchini kote ninashauri hili lifanyike Ili kuzuia.

Suala nililolifikiria kichwani mwangu linaloweza kuzuia hili bila kuangalia kiwango Cha bajeti ni suala la sheria. Sheria iliyopo nchini kwangu haijajitosheleza kuzuia vitendo vya rushwa kama serikali ikiweka ugumu zaidi na ikatekeleza sheria hii Tanzania bila rushwa inawezekana.

Sheria nimayoiona ni Bora kutumika nchini kwetu ni sheria ya kuwagusa wapendwa wa mtoa rushwa na mpokea rushwa ninamaanisha mchuma janga hula na wa kwao nikiwa na maana kuwa kama mtu atatenda kitendo cha kupokea au kutoa rushwa adhabu kali inayofuata haki za kibinadamu itolewe lakini adhabu hii iihusishe familia yake Moja kwa Moja.

Pia kama ilionekana ni bora na wao wafungwe, ifanyike ama kama ni kutaifishwa Mali zao wataifishwe, nikiwa na maana kuwa kuna aina ya watu wanaona ni sawa kutenda rushwa kwa sababu familia yake ndiyo imemuonesha kuwa rushwa ni sawa tu kupokelewa au kutolewa kwa maana na wengine wamekua wakishuhudia rushwa ikizifanya familia zao kufanikiwa na mambo mengine mengi kisaikolojia Kuna watu wanaofanya uhalifu wa aina yoyote ikiwemo rushwa kwa vile tu wanajua hata wakiguswa familia zao zitabaki kuishi kwa raha mstarehe

Wao husema wanajitoa mhanga jambo ambalo wanajua kabisa linairudisha nyuma nchi yetu katika maendeleo kama Serikali ikipitisha sheria hii Inayomuonesha mtenda kosa kua hata familia yake pendwa itaguswa kama atatenda makosa familia zitawafunza vyema watoto wao na watu hawatofikiria kutumia njia ya rushwa kutafuta mafanikio yao.

Suala lingine no serikali kuwafunza kwa vitendo na sio nadharia wanafunzi wake madhara yanayotokea kwa sababu ya rushwa hapa mitaala ya nchini unapaswa kuwekwa kwa vitendo yaani mifano hai na madhara yanayoikuta serikali yanapaswa kua wazi tangu elimu ya msingi wanafunzi wanapaswa wapewe nafasi ya kusoma hata matukio kadhaa yaliyothibitika kua ni vitendo vya rushwa na madhara yaliyoisababishia nchi adhabu zilizotolewa kwa wahusika na mambo mengi hili litasaidia kuwaonesha wanafunzi namna wanavyopaswa kuilinda nchi yao kwa gharama yoyote Ile kwa kupiga vita rushwa suala lingine ni kutengeneza mazingira rafiki kwa watoa taarifa ya vitendo vya rushwa kulindwa na kuishi kwa amani kwa vile wanakua hatarini wanapofichua Siri zinazohusiana na vitendo vya rushwa ulinzi uwekwe mkali sana.

Suala la mishahara kwa watendakazi katika mamlaka linaonekana kua kichocheo Cha upokeaji na utoaji wa rushwa serikali ilipe mishahara kwa watendakazi wake kutokana na ofisi anayofanya kazi namna inavyoingiza pesa kwa maana wengi wao huingiwa tamaa kwa kua hufanya kazi katika ofisi zinazoingiza pesa kubwa ingali wao hupokea mshahara kiduchu kwa hiyo kama ikitokea nafasi yoyote ya kupokea rushwa hua inawawia vigumu kusita kupokea rushwa mshahara wa kuridhisha nao ni muarobaini tosha wa vitendo vya rushwa nchini kwetu
 
Upvote 8
Sheria nimayoiona ni Bora kutumika nchini kwetu ni sheria ya kuwagusa wapendwa wa mtoa rushwa na mpokea rushwa ninamaanisha mchuma janga hula na wa kwao nikiwa na maana kuwa kama mtu atatenda kitendo cha kupokea au kutoa rushwa adhabu kali inayofuata haki za kibinadamu itolewe lakini adhabu hii iihusishe familia yake Moja kwa Moja.
Weeeeeeh! Itakuwa kinyume na haki. Labda kama huyo kiongoz/mtendaji yupo chini ya miaka 18 ndio tuseme ni mtoto na hawakumkanya wa kwao😄

i Inayomuonesha mtenda kosa kua hata familia yake pendwa itaguswa kama atatenda makosa familia zitawafunza vyema watoto wao na watu hawatofikiria kutumia njia ya rushwa kutafuta mafanikio yao.
Ika kama ukosisitiza sana uhusika wa watu wake wa karibu. Iwe kwa kutumia sheria ya walijua ametenda kosa na hawakuripoti uhalifu...... hapo itabidi uthibitisho kwamba wamefahamu ama kishirikiana naye kutumia mali wanayojua ni ya wizi_rushwa

Suala la mishahara kwa watendakazi katika mamlaka linaonekana kua kichocheo Cha upokeaji na utoaji wa rushwa serikali ilipe mishahara kwa watendakazi wake kutokana na ofisi anayofanya kazi namna inavyoingiza pesa kwa maana wengi wao huingiwa tamaa kwa kua hufanya kazi katika ofisi zinazoingiza pesa kubwa ingali wao hupokea mshahara kiduchu kwa hiyo kama ikitokea nafasi yoyote ya kupokea rushwa hua inawawia vigumu kusita kupokea rushwa mshahara wa kuridhisha nao ni muarobaini tosha wa vitendo vya rushwa nchini kwetu
NDiyo, kila mtenda kazi alipwe ujira wake stahiki, asizidishiwe wala asidhulumiwe. Mwanasiasa akilipwa posho nzuri na mwanahalmashauri alipwe vizuri hivyohivyo
 
Back
Top Bottom