Aliyekuwa miongoni mwa waasisi na mwanachama front liner wa Chama Cha Jamii CCJ, Mashaka Seif, asubuhi ya leo ametangaza rasmi kujitoa CCJ na kuhamia TLP, katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo. Bwana Mashaka alimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Hamad Rajab Tao kadi yake ya CCJ na kukabidhiwa kadi mpya ya TLP pamoja na ilani ya Chama.
Bwana Mashaka pia ametangaza nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Rorya mkoani Mara, na amesema mgogoro wa usajili kati ya CCJ na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini ndiyo sababu kubwa iliyomfanya ahamishie majeshi TLP.