Mucormycosis: Maradhi mengine yanayosababishwa na corona

Mucormycosis: Maradhi mengine yanayosababishwa na corona

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
13,265
Reaction score
4,735
Wakati wimbi kali la pili la maambukizi ya Covid-19 linaloua watu likiikumba India, madaktari sasa wanaripoti ongezeko la haraka la visa vya maambukizi ya nadra ya kuvu -ambao pia huitwa "black fungus" - miongoni mwa wagonjwa waliopona Covid-19.

Mucormycosis ni nini?​

Mucormycosis ni maambukizi ya nadra sana. Hutokea pale mtu anapokaa katika mazingira ya ukungu unaofanana na kamasi ambao kwa kawaida hupatikana katika udongo, mimea, mbolea na matunda yaliyooza, na makamasi ya watu wenye afya," anasema Dkt Nair.
Huathiri pua, ubongo na mapafu na unaweza kutishia maisha kwa watu wenye maradhi ya kisukari au wenye tatizo kubwa la ukosefu wa kinga mwilini kama vile, watu wenye magonjwa ya saratani au HIV/UKIMWI

Madaktari wanaamini mucormycosis, ambayo kwa ujumla ina uwezekano wa kuua kwa kiwango cha 50%, huenda husababishwa na matumizi ya homoni zinazotengenezwa na binadamu (steroids), tiba ambayo hutumiwa kwa mtu mgonjwa wa Covid-19 ambaye maisha yake yamo hatarini.

Steroids hupunguza hali ya kuungua katika mapafu kutokana na Covid-19 na inaonekana kusaidia kuzuia baadhi ya uharibifu ambao unaweza kutokea wakati mfumo wa kinga ya mwili unapohangaika kupambana na virusi vya corona.

The WHO has classified the coronavirus variant first found in India last year as a variant of global concern

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini pia zinazuia upungufu wa kinga ya mwili na kusukuma juu viwango vya sukari ya mwili miongoni mwa wagonjwa wenye kisukari na wasio na kisukari wanapopata maambukizi ya Covid-19.

Inadhaniwa kwamba kushuka huku kwa kinga ya mwili kunaweza kusababishwa na visa hivi vya kuvu aina ya mucormycosis.
"Kisukari hushusha kinga ya mwili, virusi vya corona vinaizidisha , na halafu steroids ambayo husaidia kupambana na Covid-19 huwa kama mafuta kwenye moto kwa kuzidisha hali hiyo ," anasema Dkt Nair.
Dkt Nair - anayefanya kazi katika hospitali tatu mjini Mumbai, mojawapo ya miji iliyoathiriwa sana na wimbi la pili -anasema amekwisha shuhudia wagonjwa wapatao 40 wakiwa wanaugua kuvu hiyo mwezi Aprili.

Wengi wao walikuwa na ugonjwa wa kisukari na walikuwa wamepona Covid-19 wakiwa nyumbani. Kumi na mmoja kati yao ilibidi wafanyiwe upasuaji wa kuondoa macho yao.

Kati ya Disemba na Februari, madaktari wenzake katika hospitali za miji mitano - Mumbai, Bangalore, Hyderabad, Delhi na Pune -waliripoti visa 58 vya maambukizi hayo.

Wengi wa wagonjwa waliyapata maambukizi katika kipindi cha sku 12 na 15 baada ya kupona Covid-19.

Hospitali yenye shughuli nyingi ya mjini Mumbai Sion, imeripoti wagonjwa 24 wa maambukizi ya kuvu, katika kipindi cha miezi miwili, kulingana na Dkt Renuka Bradoo, kuu wa kitengo cha magonjwa ya masikio, macho na koo.

Kumi na mmoja kati yao ilibidi apoteze jicho , na sita kati yao walikufa. Wengi miongoni mwa wagonjwa hao walikuwa na umri wa kati wa utu uzima waliokuwa na ugonjwa wa kisukari na walipata kuvu(fungus) baada ya kupona . "Tunashuhudia tayari visa viwili hadi vitatu kwa wiki. Ni tatizo katika kipindi hiki cha janga ," alisema.

Dkt Nair anasema amekutana na visa visivyopungua 10 mjini Mumbai katika kipindi cha miaka mwili iliyopita. "Mwaka huu ni kitu tofauti," anasema

Katika Bengaluru, Dkt Hegde hajawahi kushuhudia zaidi ya kisa kimoja au viwili kwa mwaka katika kipindi cha muongo mzima alichofanya kazi ya udaktari , lakini anasema pia mwaka huu visa vimeongezeka.

Wagonjwa wanaougua maambukizi ya kuvu (fungal infection) wana dalili za kuvimba na kutokwa damu puani, uvimbe wa jicho, kushindwa kuona vyema na hatimaye, kupoteza kabisa uwezo wa kuona.

Kunaweza kuwa na ngozi yenye vipele vyeusi kando ya pua.

Mucor mould is found in soil, plants, manure and decaying fruits

Chanzo cha picha, Getty Images

Madaktari wanasema wengi miongoni mwa wagonjwa wao hufika wakiwa wamechelewa hospitalini, wakati tayari wanapoteza uwezo wa kuona, na hivyo kuwabidi madaktari kuwafanyia upasuaji wa kuyaondoa macho yao ili kuzuia maambukizi kuufikia ubongo.
Katika baadhi ya wagonjwa,madaktari nchini India wanasema, wagonjwa wamepoteza uwezo wao wa kuona katika macho yao yote mawili. Na katika visa vya nadra, madaktari wamelazimika kuondoa kabisa mifupa ya taya ili kuzuia ugonjwa kusambaa katika maeneo mengine ya mwili.

Njia mojawapo ya kuzuia uwezekano wa maambukizi ya kuvu ni kuhakikisha kwamba wagonjwa wa Covid-19 - wanapopokea matibabu na baada ya kupona wanapewa dozi sahihi na kupewa homoni za steroids ipasavyo , anasema dokta Rahul Baxi,daktari bingwa wa maradhi ya kisukari mwenye makao yake Mumbai.

Anasema aliwatibu wangonjwa wapatao 800 wenye kisukari waliokuwa na Covid-19 mwaka uliopita, na hakuna hata mmoja wao aliyepata maambukizi ya kuvu. "Madaktari wanapaswa kujali viwango vya sukari ya mwili baada ya wagonjwa kuruhusiwa kwenda nyumbani ," anasema dokta Baxi.

Mgonjwa wake mwenye umri mdogo kwa wote alikuwa na miaka 27 mwanaume, ambaye hata hakuwa na maradhi ya kisukari . "Ilitubidi tumfanyie upasuaji wakati wa wiki yake ya pili ya Covid-19 na kuondoa jicho lake. Ni pigo kwa kweli."

CHANZO: BBC www.bbc.com/swahili/habari-57091131
 
Hii kuvu inashambulia macho tyuu??

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Msitutishe pumbavu zenu.
nimecheka mpaka barakoa imeloa: lisemwalo lipo - punguza hasira, wakati covid ilipotangazwa kuwa imeanza kuwatafuna wachina, sisi tulififkiri halitafika kwetu
 
Back
Top Bottom