Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,903
Rasimu ya warioba ingejibu kero nyingi
Ni muda mfupi,watanzania huenda wamemsahau Warioba na tume yake.
Lakini ili ujue ubora wa timu hii, jaribu kupitia Randama ya katiba na katiba pendekezwa ni tofauti kabisa,Rasimu ya warioba ilijibu kero nyingi.
Mfano baadhi ya mambo mazito yaliyojadiliwa humo nihaya;
ZAWADI
Mtumishi wa umma hataruhusiwa kupokea zawadi,akiwa kwenye shughuli za serikali akapewa zawadi,zawadi hiyo itakuwa mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo itakabidhiwa kwa katibu Mkuu kiongozi au wa wizara husika.ibara ya 15
Kufungua akaunti nje
Kiongozi wa umma,hataruhusiwa kumiliki au kuweka fedha kwenye akaunti nje ya nchi,isipokuwa sheria itakavyoelekeza
Ibara ya 88(1)
Rais anaweza kushitakiwa iwapo tu atapuuz au kukataa kutekeleza uamuzi au amei ya mahakama.
Au amepokea rushwa.
Wajumbe wa bunge la Muungano
Kutakuwa na wabunge sabini wa kuchaguliwa,na wabunge watano wenye ulemavu,katika kila jimbo wabunge watagombea wawili mwanaume na mwanamke.
Mamlaka ya kukopa
Serikali itaweza kukopa,lakini kifungu ( b),kinasema itaweka ukomo wa deni la Taifa na madhumuni ya kukopa.
Vyombo vya usalama
Viliwekwa wazi kuwa kutakuwa na vyombo vya usalama,vyombo hivi ni jwtz,jeshi la polisi,usalama wa Taifa na wajibu wao,katika shughuli zao hawataruhusiwa;
Kuwa na upendeleo,
Kuendeleza maslahi ya kisiasa ya chama chichote,
Kuhujumu maslahi ya kisiasa au mpango wa kisiasa ambao ni halali kwa mujibu wa katiba hii.
Kutishia,kudhulumu au kuwatendea ukatili raia na wengine.
Mamlaka ya kuwajibisha mbunge
Ibara ya 129(1), inawapa mamlaka wananchi kumwajibisha mbunge wao,endapo tu,atafanya haya,
Kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na maslahi ya wapigakura au kinyume na maslahi ya Taifa,au
Kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati,hoja zinazorokana na kero za wapigakura au kuacha kuishi au kuhama eneo lake la kazi.
Yapo mengi ambayo ni wazi kuwa Taifa kupitia pendekezo hayo ni dhahiri Taifa hili lilikuwa mfano wa kuigwa