Hi!
Kuna Watanzania tayari wanawasiliana kuanzisha mchakato mbadala wa Katiba kama nilivyonukuu mojawapo ya waraka wao happ chini.
"1. Tunatakiwa kuanza mchakato wa Mkondo-Sambamba wa Kuandika Katiba Mpya ya Tanzania sawia na mchakato rasmi wa (serikali) Bunge Maalum la Katiba. Kwa njia hii tutatoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kurejea maudhui ya Rasmu ya Pili ya Katiba. WanaAzaki, wajasiliamali, wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, wasomi, wanawake, vijana, wanataaluma, wanasiasa wachimba madini na wengineo watapata fursa ya kupitia na kusahihisha pale inapotakiwa, ibara zote za Rasimu ya Pili ya Katiba na hatimaye kupata Katiba mbadala wa ile itakayopitishwa na Bunge Maalum la Katiba. Katiba Mbadala itakayopatikana itachapishwa na kusambazwa kwa wananchi wote - kama nyenzo ya kuwashawishi wananchi wakati wa kampeni za Kura ya Maoni, kukubali au kukataa Katiba itakayokuwa imependekezwa na Bunge Maalum la Katiba.
2. Maandalizi ya Mkondo-Sambamba wa Katiba yanatakiwa kuanza sasa, kwa Wadau kadhaa kufanya mkutano wa awali wa maadalizi. Masuala kadhaa yanatakiwa kujadiliwa, kuangaliwa kwa mapana na kuafikiwa. Kwa mfano, kuna haja ya kukubaliana juu ya Muundo wa Kitaasisi na mfumo wa uongozi utakaofaa kuratibu Mkondo-Sambamba wa Katiba; kuweka utararatibu wa kupanua ushiriki na kuhakikisha wadau wengi wanashiriki katika Mkondo-Sambamba wa Katiba; na masuala mengine ya kiufundi.
3. Kutokana na umuhimu na uharaka wa suala hili, tunaomba wadau wanaotaka kushiriki katika mkutano wa awali wa maandalizi ya Mkondo-Sambamba wa Katiba watutumie jina na namba ya simu ya asasi/mjumbe mmoja anayependekezwa kushiriki mkutano huo. Tutatumia taarifa hizi kuwaalika wahusika tukiwataarifu mahali na siku/muda wa mkutano wa maandalizi."