Muda na fedha ujenzi nyumba two storeys

Muda na fedha ujenzi nyumba two storeys

zakarya

Member
Joined
Nov 1, 2015
Posts
36
Reaction score
5
Kujenga nyumba ya aina hii sasa kunachukua muda gani ? Na fedha gani. Mkoa wa Tanga.
1107883
 
Mkuu hiyo ni picha tu inayoonyesha muonekano wa Nyumba unayoihitaji, hapo ungeongezea mahitaji yako ya vyumba kwa kila floor ndiyo mtu anaweza pata picha juu ya maswali yako.
 
Inaonekana hujawahi kabisa kujenga hata kibanda cha kuku... maana hata ABC za ujenzi huna...

1. Tafuta mchoro kulingana na mahitaji yako, uwezo wako na eneo lako..
2. Tafuta mshauri akupe gharama za jengo lako
3. Pata kibali, anza kujenga..


Haya mambo ya kuonyesha tuu picha za kuokota mtandaoni ukitegemea jibu sahihi ni yakitoto.. Tena diaspora ndo wanahaya mambo ya ajabu ajabu, na exposure yote walionayo...
 
Kuhusu, muda, kama uko vizuri four to five months unamaliza unahamia...
 
Muda wa kujenga hadi kumaliza inategemeana tu na mfuko wako. China wamejenga hospitali kubwa ya wagonjwa wa covid-19 kwa siku ngapi? Ukitaka ijengwe kwa wiki 3 ni wewe tu, mwaka, miaka mitatu. Gharama za ujenzi pia inategemea unataka material ya ubora gani, vya bei rahisi vipo na vya bei juu pia vipo. Vile vile ukitaka ijengwe kwa muda mfupi sana gharama za labour zitakua juu.
 
Back
Top Bottom