strategist22
JF-Expert Member
- Jun 6, 2017
- 655
- 599
Mwanafalsafa na mwanahisabati wa Uyunani ya kale Paithogorasi alipoulizwa muda ni nini ? alijibu "Muda ni pumzi ya ulimwengu " nakubaliana na majibu yake .
Neno pumzi Kiyunani hujulikana kama "Pneuma" neno "pneuma "linafanana na neno la kiebrania "ruach" yote mawili yakiwa na maana Pumzi, pumzi ya uzima. Katika mazingira ya sasa au ya kidini, neno "Pneuma" pumzi ya Uzima hujulikana kama "Roho" au "Nafsi"
Muda kama pumzi ya uzima
Bila kujali unatoka wapi,upo wapi, rangi, kabila, kipato tajiri au masikini watu wote tumepewa pumzi,pumzi ya uzima bure. Muda na pumzi ya uzima ni bure. Wapi wanapouza pumzi ya uzima au muda ? nani anayeuza pumzi ya uzima au muda ?. Kuuza ni kitendo cha kufanya bidhaa au huduma inapatikana ili watu waweze kununua. Hakuna awezaye kuuza pumzi ya uzima au muda.
Unafikiri unaweza kununua pumzi ya uzima au muda ? Kununua ni kupata kwa kubadilishana, kupata miliki ya..., au haki ya... kwa kulipa au kuahidi kulipa sawa hasa kwa fedha yaani unatoa pesa ili kupata kitu kinachouzwa. Kiasi gani cha pesa unahitajika kutoa kununua pumzi ya uzima au muda ? Mabilioni ya pesa hayawezi kununua pumzi ya uzima na muda.
Kununua ni kupata miliki ya.... je tunaweza kumiliki pumzi ya uzima au muda ? Kumiliki ni kuwa na... .kuwa na udhibiti juu ya..... Je tunaudhibiti juu ya pumzi ya uzima na muda ? .Hatuna udhibiti juu ya pumzi ya uzima na muda.
Pumzi ya uzima na muda uliopotea hatuwezi kuvirudisha, yaani hatuwezi kurudisha uhai ukipotea kwa namna yeyote sawa na muda ukipita umepita ukipotea umepotea. Kamwe hatuwezi kurudisha hata sekunde moja iliyopita nyuma.
Pumzi ya uzima na muda havihifadhiki ni kiwa na maana uwezi kuchukua muda au pumzi ya uzima na kisha ukahifadhi mahali hadi hadi utakapo kuwa na uhitaji.
Pumzi ya uzima na muda ndiyo maisha yetu. Pumzi ya uzima na muda ni kama maji ya mto yanayotiririka.Maji ya mto hutiririka bila kujali yanatumika au hayatumiki, yanatazamwa au hayatazamwi, kuna matukio au hakuna yanaendelea kutiririka. Maji uliyoyagusa leo kamwe hutayagusa tena, wakati uliokuwa nao leo kamwe hautakuwa nao tena.
Muda na Maisha yetu
Maisha yetu yamefungwa kwenye muda, muda ni sehemu ya maisha yetu. Ni muhimu kuuthamini muda.Maisha ya kila siku hutegemea sana muda. Muda ndicho kitu maisha yetu yamejengwa kwacho.
Muda ni Maisha
Mwanasayansi mashuhuri kutokana na nadharia yake ya maendeleo ya uhai katika karne ya 19,Charles Darwin alisema"Mtu anayethubutu kupoteza saa moja ya wakati hajagundua thamani ya maisha. " Muda ndicho kitu maisha yetu yamejengwa kwacho. Nakubaliana na Mwanafalsafa William Penn aliposema "Muda ni kitu tunacho kihitaji kwa kiasi kikubwa, lakini tunakitumia vibaya kabisa. "
Usipoteze Wakati wako.
Ukipoteza muda, muda utakupoteza zaidi. Kila muda tunaopata kuishi, una umuhimu wake mkubwa. Mwandishi Joyce Meyer anesema "usikubali watu waibe wakati wako, usipoteze wakati wako na usiseme nina jaribu kupoteza wakati kidogo... muda wetu ni bidhaa ya thamani twapaswa kuutoa kwa lengo na kwa busara"
Wakati Uliopita.
Hivi majuzi, nilipokuwa nasikiliza wimbo wa mtunzi na mwimbaji wa uingereza Michael David Rosenberg anayejulikana zaidi kwa jina la jukwaani Passenger "When we were young " Niliona funzo kubwa juu ya maisha yetu na muda, unaweza kuchelewa lakini muda hauwezi. Muda hausubiri mtu huenda kwa usahihi wake.
Passenger anasema "Kumbuka tulivyo Kuwa vijana, kusanya jana zetu, tulifikiri tutaishi milele. Angalia siku nzuri za zamani, tulikuwa wavulana kwenye pwani, kila kitu kilikuwa kinafikika. Siku huenda mbio na kujificha, wiki zinateleza na kuponyoka, miaka inaondoka haraka. Najua ni ngumu kukumbuka. Jinsi miaka inavyotoweka ghafla na kabisa. Siku zote nilitaka kujifunza Kihispania na kusafiri kuzunguka Amerika ya kusini .Tulisema tutafanya kesho lakini kesho haikuonekana kamwe kuja"
Mara nyingi tunapokaa na wazee wetu, wanatupa habari za kupendeza juu ya siku za ujana wao "siku nzuri zamani" Wanatuonyesha jinsi walivyo furahia maisha wakati huo "siku nzuri zamani "Utaona walikuwa na furaha zaidi wakati uliopita kuliko sasa. Sasa wanaonyesha dhahiri jinsi wanavyo huzunishwa kushindwa kufanya mambo muhimu wakati muda walikuwa nao,lakini hawakutumia wakati ipasavyo.
Wakati Haungoji Mtu,huenda sahihi.
Jinsi walivyokuwa wakiendesha maisha yao ,bila kuzingatia wakati. Katika" siku nzuri zamani",Kila kitu kilikuwa rahisi lakini hawakutumia wakati huo Kutengeneza siku za fanaka,hata baada ya nyakati hizo kupita. Kwa ajili yao wenyewe na familia zao sasa na Kesho.
Twaona yale wanayofanya si ya wakati wao,ninapoangalia kile wanachofanya kinastahili kufanywa "siku nzuri zamani "lakini wakati hauwezi kurudi nyuma wapate fursa ya kujijenga tena fursa ya kuwa bora kila wakati, wakati wote iliyopotea. Neno "ningelijua.." huzunguka kwenye akili. Kuna methali ya kifaransa inayosema "hazina zote za duniani haziwezi kurudisha fursa moja iliyopotea" Wakati ni fursa, maisha ni fursa. Huu ni ukweli wa maisha unaoshangaza "Ukichagua kucheza na muda huwezi kukwepa matokeo yake ambayo siku zote ni mabaya sana".Ukipoteza muda, muda unakupoteza zaidi.
Kila Jambo Kuna Majira Yake
Kuna mafundisho muhimu juu ya kujali wakati kwenye maisha yetu kwenye biblia. Nimejifunza kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya jua. Hatuwezi kupanda mbegu msimu wa kuvuna wala kuvuna msimu wa kupanda mbegu. Kila kimoja hufanyika kwa wakati wake.
Jana Na Leo.
Hatuwezi kuchanganya jana na leo. Hazichanganyiki, kama utajaribu leo itaharibika zaidi. Acha kusikiliza sauti toka jana, ya kale yamepita. Sisi sote tumepotea, jana tumejifunza leo tunaweza kusimama na kutenda jambo jipya. Hatuwezi kubadili jana tunaweza kuanza leo kuibadili Kesho yetu.Majuto yanafanya turudi nyuma, badala ya kusonga mbele..
Strategist22
Sent using Jamii Forums mobile app