OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya nchini kuacha mara moja kamatakamata ya bodaboda isiyo na tija akisema Maaafisa usafirishaji (bodaboda) na Maafisa wa Serikali wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano katika Mikoa na Wilaya ili kwa pamoja washiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Mchengerwa ametoa maelekezo hayo akiwa Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijiji Dar es Salam wakati akizindua sare maalum (uniform) na mfumo wa kidijitali (kanzidata) wa Madereva bodaboda na Bajaji wa Jiji la Dar es salaam.
“Kuanzia sasa sitaki kusikia kamata kamata ya hovyo, inayotokana na wakati fulani kuwepo na sintofahamu baina yenu na Maafisa wa Serikali, mchango wenu ni mkubwa sana hivyo Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawathamini sana ninyi Maafisa usafirishaji wa bodaboda na bajaji, na ndio maana ninataka kuona ushirikiano mzuri unakuwepo baina yenu na Serikali”
Mchengerwa amesema, Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua mchango wa kila Mtanzania katika ujenzi wa Taifa, wakiwemo Madereva bodaboda, Madereva bajaji, Mama lishe na wengineo hivyo haiko tayari kuona yeyote akisumbuliwa au kunyanyasika.
Mchengerwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya Nchini kuwa na utaratibu wa kukutana na vikundi vya bodaboda mara kwa kwa mara kwa lengo la kutatua kero na changamoto zinazowakabili, ambazo ndio chanzo cha kufarakana na kuibua migogoro.
My Take
Boda jiandaeni kutumika kama mpira wa kiume