Vigezo vya kuoa au kuolewa ni umri wa kuanzia kisheria yaani zaidi ya miaka 18 na ukomavu wa akili ambao kipimo chake ni wewe mwenyewe.
Ili kujua kama umeshakomaa kiakili kuweza kuchukua dhamana ya kubeba Roho ya mwenzako jipime kwa kujiangalia vitu kama ubinafsi, ukweli na uadilifu, kujitoa muhanga kwa familia (Sacrifice) hasa kama wewe ndiye Baba; uwezo wa kusahau maisha ya ujana ya kujaribu kupima mafuta kila sehemu; uwezo wa kubeba lawama bila kuteteleka na kusimama katika ukweli; Je? Unaweza kusimama kidete mbele ya jamii na kukinga kifua kwa ajili ya famili yako? Unaweza kumsamehe mwenza wako kwa kumwamini au bado utaenda kuomba ushauri kwa bosi kuhusu mambo ya chumbani? Na vitu vingine ambavyo havina shule ila vyote vinaunganishwa na uwezo wa wewe kujua thamani ya mwenza wako kama binadamu!
Nyote wawili mkiwa na miaka 18 na kuweza kujiuliza maswali ya hapo juu.basi mnaweza fanya maamuzi. Kumbuka kwenye orodha sijaweka gari, nyumba, kiwanja, mali, etc.. jumuisho la vyote ni kujitoa muhanga kwa dhiki na faraja hasa kwa kile ambacho hujui mwisho wake!