Muda wa kuingia katika ndoa

ngellesh

New Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
3
Reaction score
1
nimeumiza sana kicha juu ya ni mda gan mwanaume au mwanamke aamue sasa nataka kuowa au kuolewa kwa sabab watu wengi hufanya hivyo pindi wanapokuwa na pesa za kutosha, wengine wanapomjaza binti mimba na wengine pale umri unapoenda sana na kuogopa aibu huku wengine wakifanya hivyo kwa kulazimishwa, swaali langu ni hiv, '' when is the right time to marry''.
 
When u think that it is a time to do that no matter what factor (s)
Hata ukiwa na miaka 18 ukiona unaweza kuoa na kukaa na mwanamke ndani ya nyumba au mume unaweza kuoa au kuolewa au ukiw ana miaka 45 baada ya kuona kuw andio muda wako huo umefika
 
i will marry when i...............................,by the way i am still hanging
 
Igwe isije ikawa ni mpaka ............................or the beautiful one is not yet born
 
Igwe isije ikawa ni mpaka ............................or the beautiful one is not yet born

Usijali kaka,....tutaoa,...................beautiful woman are there and i like them girls......girls,girls,girls............
 
Usijali kaka,....tutaoa,...................beautiful woman are there and i like them girls......girls,girls,girls............


I know kaka real men are there and beautiful gals are there just prove to them that you are real men till that real time
 
Pale unapohamua kuoa ndo muda muafaka.
 
Pale unapohamua kuoa ndo muda muafaka.

Mkirua shimbonyi shapfo
Real ukiamua muda wowote unawez akuchukua maamuzi sidhani kama kuna mahali imeandikw aumri wa kuoa ni huu
Mradi tuu muoaji na muolewaji wafikie umri unaoruhusiwa kisheria hapa kwetu
 
eeeeeeehe njoo leo na mbuzi jike mwemye mimba ya wiki nne na siku tatu

Ngoja niangalie kama kuna mbuzi wa aina hiyo hapa home nitakuja
Ni hilo tuu unataka hakuna kingine
 
Ngoja nikaangalie ratiba ya basi la kutoka hapa kijijini maana huwa linakuja mara moja kwa wiki
poa dah afadhali bwana na mimi nitakuwa bibi harusi mwaka huu
 
poa dah afadhali bwana na mimi nitakuwa bibi harusi mwaka huu

Usiwe na shida nitakuja pia na unga wa muhogo na mtama uje unipikie ugali maana sijazoea vyakula vya mjini
 
Vigezo vya kuoa au kuolewa ni umri wa kuanzia kisheria yaani zaidi ya miaka 18 na ukomavu wa akili ambao kipimo chake ni wewe mwenyewe.

Ili kujua kama umeshakomaa kiakili kuweza kuchukua dhamana ya kubeba Roho ya mwenzako jipime kwa kujiangalia vitu kama ubinafsi, ukweli na uadilifu, kujitoa muhanga kwa familia (Sacrifice) hasa kama wewe ndiye Baba; uwezo wa kusahau maisha ya ujana ya kujaribu kupima mafuta kila sehemu; uwezo wa kubeba lawama bila kuteteleka na kusimama katika ukweli; Je? Unaweza kusimama kidete mbele ya jamii na kukinga kifua kwa ajili ya famili yako? Unaweza kumsamehe mwenza wako kwa kumwamini au bado utaenda kuomba ushauri kwa bosi kuhusu mambo ya chumbani? Na vitu vingine ambavyo havina shule ila vyote vinaunganishwa na uwezo wa wewe kujua thamani ya mwenza wako kama binadamu!

Nyote wawili mkiwa na miaka 18 na kuweza kujiuliza maswali ya hapo juu.basi mnaweza fanya maamuzi. Kumbuka kwenye orodha sijaweka gari, nyumba, kiwanja, mali, etc.. jumuisho la vyote ni kujitoa muhanga kwa dhiki na faraja hasa kwa kile ambacho hujui mwisho wake!
 
Mkuu Tulizo umemaliza kila kitu
Kingine ni yeye mwenywe muhusika ajiangalie tuu kama yuko tayari kuweza kuishi na mwenza katika maisha na kujiandaa kwa changamoto mbalimbali zinazokuja huko mbele na ajue kuwa anaongeza familia na si yeye mwenyewe tena bali kuna mke na watoto watakaokuja iwapo Mungu atawajalia. Pia ajue kwa familia za Kiafrica extended family zetu ajue kuwa kuna familia ya wakwe imeongezeka ajue kuwa ni jukumu lake

Na je yuko tayari kuweza kuhimili yale yanayotokana na kuoa
 
Mkirua shimbonyi shapfo
Real ukiamua muda wowote unawez akuchukua maamuzi sidhani kama kuna mahali imeandikw aumri wa kuoa ni huu
Mradi tuu muoaji na muolewaji wafikie umri unaoruhusiwa kisheria hapa kwetu

Natsicha tupu monowama!! kindo ngiliie nakilya ulengienenga!

Na ndio maana wahusika wakishafikia umri dini au wazazi hawawezi kuwashurutisha...
 
Natsicha tupu monowama!! kindo ngiliie nakilya ulengienenga!

Na ndio maana wahusika wakishafikia umri dini au wazazi hawawezi kuwashurutisha...

Ngekutafuta inu ngikuenenge kindo kicha mnu
kabisa na wala hakuna haja ya kusema sijui nini wala nini unajikuta mwenyewe umejipeleka mdomoni mwa mamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…