Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa

Huwa napenda wachangiaji wenye michango chanya na wewe ni mmojawapo. Hongera!
 

Yote hayo mkuu hayamsimamishi kwa jahiri aliyekubuhu kufanya yake. Waulize pana vi nchi hapo magharibi yetu.

Kupongeza tunapofanya maendeleo, ni strategy nzuri ya mapambano.

Yasijekuwa yale ya Katiba mpya. Kidogo kidogo hujaza kibaba na Pole pole ndiyo mwendo.
 
Awali ya yote, hakutakiwa kabisa kubughudhiwa na kwahiyo kilichotokea sio favor!! Na kwa upande mwingine, hapo hakuna suala la nia njema hapo, kwa sababu hiyo nia mbaya, haitakiwi kuwepo kwa sababu zozote zile!!

Lakini kubwa zaidi, it's too soon tu assume kwamba eti jamaa wamebadilika au kujirudi kwa sababu mazingira yenyewe yaliyopo, ni wapumbavu tu ndie wangefanya move yoyote against TL!

Na kama nilivyosema, I'm certain hata international media zilikuwa zinafuatialia kurejea kwa TL ili kuangalia endapo atapita salama pale airoport!! Any attempt to TL, ingekuwa na international coverage kubwa sana within a short time... utawala walilijua hilo!!!

Mathalani in the next few days ikitolewa hati ya kukamatwa kwake, coverage yake itakuwa tofauti sana na endapo wangefanya hivyo pale airport, wakati iwe amekamatwa airport au baadae, bado ni kitu kile kile kwa upande wa wapenda demokrasia lakini huku ikiwa ni nafuu kwa watawala kufikia lengo lile lile lakini bila mayowe!!

Na kwa upande mwingine, they're not that stupid to wash their dirty linen in public!!

Itoshe tu kusema kwamba, "it's too soon to say it's finally over, they've changed"!
 
Kwanini isiwe TL tosha?
 



Mkuu, angalia hii comment #419:



Comment #419 kwenye uzi huu:

Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Makamanda, vita (mapambano) ni strategy. Strategy ya mapambano ni pamoja na kutokumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Kufahamu nini unataka namna gani ukipate ndiyo busara yenyewe.

Tunaweza kuganga yajayo katika namna ambayo ni muafaka zaidi kwa usalama na amani ya kila mtu huku tukiwapongeza na hata kuwashukuru watesi wetu inapobidi.

Wapumzike kwa amani kina Mao, Che, Castro na washupavu wengine.
 

Halima amefanya vyema leo kulipongeza jeshi la polisi, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano hii rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi lake binafsi
 

Mkuu nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa. Hapana haja ya jazba makamanda.

Ila kesho twende msibani. Twende na Lissu msibani akiweza. Twende kuhani. Ule msiba ni wetu sote.

Tukatoe heshima zetu kwa mzee Mkapa na tukaionyeshe nia njema kwa kuepuka vitendo vyovyote hata kama watakuwapo wasioitakia mema nchi yetu au provocation ya aina yoyote. Hiyo ndiyo maturity wakuu.

Msibani hakuna mwenyewe. Ndiyo uswahili wetu huo tulio barikiwa nao.

Hata hivyo na kwa namna yoyote usalama wa maisha ya Lissu linapaswa kuwa ni kipaumbele haswa na kwa muda wote.
 
Mmh! Sijui kama anaweza kutoa pole. Huyu jamaa siyo mpatanishi by nature, bali ni mpenda shari na visasi. Akitoa pole jua litakoma kuchomoza.

Tusiifunge milango wakuu (ila usitake ncheke). Tanzania ni kubwa kuliko mtu au kikundi cha watu.

Kukiri upungufu mbona ni kitendo cha kiungwana tu. Siyo unyonge.

Kwa mswahili inamgharimu nini kusema "pole."

Tuwe na matumaini.

Obama anasema "the audacity of hope."

Kwa kweli pana mwanga mwisho wa pango.
 
Ngojeni tumalize msiba jamani, camera za dunia zote zimegeukia huku 🤣🤣🤣
 
Aisee Kuna logic Fulani hivi.
 
Kabisa huu ni mwanzo mzuri sana kwa siasa za ukombozi za nchi yetu, sikuamini macho yangu kwa namna watanzania walivyojitokeza kumpokea shujaa Lissu. Ni pigo kubwa mno kwa waliokuwa na nia ya kumuua.
Shetani ameshindwa Tena.
 
Mmh! Sijui kama anaweza kutoa pole. Huyu jamaa siyo mpatanishi by nature, bali ni mpenda shari na visasi. Akitoa pole jua litakoma kuchomoza.
Kwa aliyoyaona leo sijui kama keshi Msibani ataenda.
 
Kwani Magu anaogopa breaking News?? Jambo la kushukuru Mungu tu. Hapa ni Mkono Wa Rehema wa Yehova umetenda kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…