Kama sheria inavyotamka kila mwenye gari kubwa iwe ni bus au lori anatakiwa awe amelipia gharama ya Latra. Kwa uchungu kabisa kulipia Latra kumekuwa na changamoto kubwa sana. Mfano unatakiwa uende kwa vehicle inspector akague gari lako na ulipe gharama inayotakiwa.
Pili unatakiwa ulete bima yako na mwisho unatakiwa uende sasa kwenye stationery ili ukafuate taratibu zote ili upate control number ya kwenda kulipia.
Hapa kwenye stationery ndipo kuna vishoka wanaowalangua wateja na kuwadanganya na mwisho wa siku mteja anatakiwa kulipa gharama kubwa pasipo sababu.
Nina ushauri muhimu kwa Latra. Nyaraka zote za magari yanayotakiwa kulipiwa Latra wanayo.
Ninaomba kama muda wa kulipia umefika basi ni vema Latra imtumie muhusika wa gari control number ya kulipia deni analodaiwa kuliko kupitia hatua nilizozitaja na kuchukua muda mrefu kulipia deni analodaiwa.