Muda wa kunyonyesha kwa wafanyakazi (Sekta binafsi na watumishi wa Umma) waongezwa!

Muda wa kunyonyesha kwa wafanyakazi (Sekta binafsi na watumishi wa Umma) waongezwa!

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
694bca454fd40ef6880640bf6eb0954d.jpg

SERIKALI imeongeza masaa ya unyonyeshaji kwa watoto kwa watumishi wa serikali, mashirika pamoja sekta binafsi ili kuwezesha watoto kuwa na afya bora inayotokana na maziwa ya mama.

Hayo ameyasema Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua Wiki ya Unyonyeshaji, amesema kuwa mama mzazi baada ya kumaliza miezi mitatu ataingia kazini 3:30 na kuondoka saa 7:30 katika kumuwezesha mama kunyonyesha mtoto bila kuingiliwa na majukumu ya kikazi.

Waziri Ummy amesema kuwa watendaji wa Umma na mashirika pamoja na taasisi lazima wafanye hivyo katika kutambua umuhimu wa mama mzazi kunyonyesha kwa muda uliowekwa kwa kipindi cha miezi sita.

Amesema kuwa ni gharama kubwa katika kuhudumia watoto walio na utapiamlo ambao unatokana moja ni kukosa maziwa ya mama kwa muda mrefu hivyo kuepuka ni njia rahisi ikiwemo kutengwa kwa masaa hayo.

Waziri ameongeza kuwa suala la lishe lazima liangaliwe kwa ukaribu na wadau wote katika kuweza kuwaondoa watoto katika utapiamlo ambao unafanya kudumaa kwa akili.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chakula na Lishe Nchini(TFNC), Joyceline Kaganda amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika juu ya masuala ya lishe na wadau kwa mifumo mbalimbali.

Amesema kuwa wiki ya unyonyeshaji wa kina mama ni muhimu katika katika ukuaji wa mtoto wa kumjenga katika afya bora.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Lishe nchini (Panita), Tumaini Mkindo amesema serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. Pombe Magufuli imwemeka kipaumbele katika ubaoreshaji wa lishe nchini.

Amesema kuwa sera zimeweza kuongezeka katika masuala ya lishe ikiwa eneo la kipaumbele katika mpango wa taifa wa miaka mitano pamoja mikoa na halmashauri kuwa na bajeti ya lishe.
 
Yeye ndio kasema au sheria ndio inayosema hivyo. Mimi niujuavyo sheria inataja muda wa juu wa masaa mawili kila siku hii ya masaa 3 hadi 5 ameitoa wapi waziri. Au ndio anawachongea wasiajiriwe?
Employement and Labour Relation Act 2004, artcle 6 (33)(10) inaelezea hayo niliyosema
"Where an employee is breast-feeding a child, the employer shall allow the employee to feed the child during working hours up to a maximum of two hours per day."
 
Pia kifungu hicho kimefanyiwa marekebisho maana kilikuwa hakitaji ukomo wa masaa hayo mawili, sasa itakuwa ni kwa kipindi cha miezi sita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom