Muda wa kuomba mkopo bodi waongezwa

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677


Veneranda Malima

Serikali imeongeza muda wakupeleka maombi ya mkopo Bodi ya Mikopo ya Wanafunziwa Elimu ya Juu (HESLB), kwawanafunzi watakaojiunga namwaka wa masomo wa 2013/2014.
Hayo yalisemwa na Ofisa Habari Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Veneranda Malimaalipokuwa akizungumza na NIPASHE, ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kutokana na baadhi ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita kuchaguliwa kwenda kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), muda wa mkopo umeongezwa hadi Julai 31 mwaka huu.
“Tumetoa muda zaidi kwa ajili ya wale wanaokwenda kujiunga na JKT lakini ni fursapia kwa wale ambao bado hawaja jaza fomu za kuomba mkopo,” alisema.
Alisema kuwa mwaka huu 2013/2014 wanakadiria kutoa mkopo kwa wanafunzi35,000 kwa wale waliotuma maombi mapya na wale watakaothibitishwa kupewatena.

CHANZO: NIPASHE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…