OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 113
- 172
Mtoto wako anaweza kugeuka kutoka kichwa kuwa upande wa juu na akageuka -hadi nafasi ya kichwa kuwa chini kuelekea kinena (heads-up to a heads-down position) na kurejea tena kama alivyokuwa kwa mara nyingine mwanzoni mwa ujauzito. Watoto wengi hugeuka na kukaa katika nafasi ya kichwa (yaani kutanguliza kichwa) mwanzoni kabisa katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito (the third trimester). Kikawaida mtoto hugeuka na kutanguliza kichwa chini mimba inapofikisha wiki 35 mpaka wiki 36. Ikiwa mtoto wako bado hajageuka na yuko kwenye nafasi ya (breech) yaani katanguliza makalio badala ya kichwa, daktari wako anaweza kupendekeza chaguzi za kumuhimiza mtoto wako kuzunguka, na ikiwa hatogeuka basi mapendekezo ya upasuaji hufanyika (schedule a C-section)