Mbasa matinde
Member
- Feb 9, 2021
- 6
- 18
Muelekeo wa uchumi na tozo (uchumi kipofu)
Ebu tukae tulizungumze hili kwanza,
Kinachoendelea
Julai 1, 2021 serikali ilitangaza ongezeko la shilingi mia kwa kila lita moja ya mafuta.
julai 15, 2021 serikali ilianza rasmi ukatwaji wa kodi kwa watumiaji wa huduma za kifedha kwa njia ya simu ya mkononi kama mpesa, tigopesa, airtel money nk.
Agosti 1,2021 serikali ikaanza rasmi kukata rasmi kwa mtumiaji yeyote wa sim banking kila atakapoingia kwenye menu ya bank yake husika kiasi cha shilingi mia. Ndani ya huohuo mwezi seriakli ikahamisha ulipwaji wa kodi ya majengo kwa kutumia njia ya ununuaji wa umeme au luku kiasi cha shilingi alfu moja kila mwezi.
Baada ya muitikio mkubwa wa wanachi kwenye utumiaji wa benki kutuma nakupokea fedha zao kukimbia tozo, serikali imeamua kuwafata ukouko na kuanzisha tozo mpya kwa watumiaji wa huduma za kibenki kwenye kutuma na kupokea fedha zao.
Jamii imelichukuliaje
Upokeaji wa tozo hizi zote kwenye jamii ulikua hasi, ni swala ambalo linaenda kuathiri moja kwa moja Maisha ya kila mwananchi, malalamiko ni mengi na maswali ni mengi yaliyokosa kujibiwa, serikali imekosa vyanzo vya mapato? Hii ni njia sahihi ya kuongeza pato la taifa? Kipindi cha Mwenda zake serikali ilikua inatoa fedha wapi? Nk
Athari kwa ujumla
Uchumi wa Tanzania umeporomoka kutoka 7.0 mpaka 4.8 2020/2021, njia inayotumia na serikali ni ya kuua uchumu wala sio ya kunyanyua uchumi, sitaki kusema kwamba serikali imekosa wachumi weredi wakutafuta namna ya kunyanyua uchumi na kutafuta kipato kikubwa bila kudidimiza Maisha ya wananchi wachini kwa tozo hizo, ila ni dalili za kushindwa kuwajibika kwa serikali ya mama yetu kwenye mamb yanayohusisha jamii kwa moja kwa moja.
Bila ata kupepesa macho cha kwanza tatizo ni overtaxation, huwez kusaidia uchumi kwa kuongeza kodi nyonyaji kwenye jamii. Tartizo hili litaperekea kudididmia kwa wawekezaji wakubwa kwa wadogo pia, wawekezaji waliopo nchini wanaweza funga biashara zao kwa sababu ya kupanda kwa gharama za Maisha na ugumu wa biashara.
Kupungua kwa mzunguko wa fedha, hii itapelekea kukosekana kwa masoko ya bidhaa zinazozalishwa, jamii itakosa fedha maana kiasi kikubwa kinashikiliwa na serikali. Mzunguko mdgo wa fgedha utapunguza ajira na kudondoka kwa biashara na viwanada vingi vya wawekezaji kufungwa. Hili ni tatizo kubwa kwenye uchumi.
Ongezeko la gharama za Maisha. Kama hujui leo ngoja nikujuze kwamba mafuta yana athari ya 90% kwenye bei za bidhaa mbali mbali. Ongezeko la tozo liyapelekea gharama za Maisha kupanda maana kila ambacho utakigusa kununua kitapanda kwa bei.
Mfumuko wa bei za bidhaa, hii imeka ivi, kodi zitapelekea kufa kwa biashara kwa kushindwa kujiendesha, watu watakosa ajira, mzunguko wa pesa utapungua, kwa sabbu ya uchache wa viwanda na biashara uzalishaji utakua mdogo, lkn siku zote watu watahitaji kula, kuvaa nk, kwa sababu ya uhaba wa bidhaa biashara au vuwanada vitapandisha bei juu Ya bidhaa zao kwa sababu ya mahitaji makubwa kwenye jamii, hii moja kwa moja itaperekea mfumuko wa bei ambao si mzui kwenye uchumi.
Mwisho
Kuhamishwa kodi ya majengo kwa njia ya kulipia umeme au luku sio njia iliotazama kusaidia zaidi ya kunyonya. 70% ya wananchi waishio dar es salaam wamepanga. Ulipwaji wa kodi kwa njia ya luku ina maana watu wote hawa wanalipia malipo yasiyo yao.
Tanzania inaelekea kua na wananchi 65 million zaid, ni wanachi million 2 tu wanaolipa kodi, ni jambo aibu kwa mujibu wa mwendazake, serikali imeshindwa kukusanya kodi kwa weredi angalau tufike million 5 tu haya matatizo ya tozo yasingekuepo.
Tunapenda kulipa kodi kwa sababu ya maendeleo, hata izi tozo sio mbaya lakini zimekua umizi kwa sababu ni kwa kiasi kikubwa sana, kias kinachokatwa ni kikubwa na tunashindwa kuhimili kabisa wananchi wa kipato cha kawaida.
Hii sasa inaonyehsa kwamba ni Dhahiri shahiri serikali ya mama Samia Suluhu Hassan imeshindwa kutudhihilishia kwamba wananweza, ni uongozi mbovu tu unaweza fanya maamuzi kama hayo.
Serikali inabidi ikae irudie kwa umakini maamuzi haya ambayo ni maumivu kwa wananchi, wamepunguza kwa 30% lakini bado haitoshi, ili kuinua uchumi, inabidi mamlaka ya mapatoipanue wigo wa ukusanyaji wa kodi zilizopo mpk sasa. kupunguza kwakiasikikubwa kodi au tozo zilizoanzishwa sasa ka 70%. Kutafuta namna ya ulipaji mzuri wa kodi ya jingo bila kuwepo kwadalili zozote za unyonyaji kwa wale ambao si wahusika.
Upvote
1