Habari...!
Mimi ni mwanachuo wa mwaka wa pili katika chuo kikubwa Afrika mashariki na Kati. Katika kusoms kwangu toka nikiwa mwaka wa kwanza nilisikia chuo hiki kinafuata utaratibu wa Carryover under 16, ambayo inamfanya mwanafunzi arudie mwaka bila kufanya supplementary. Na hii ipo applied kwa wanaosoma masuala ya afya, yaani wanaosoma doctor of medicine, nursing, pharmacy, clinical nutrition. Nilifuatilia vyuo vingine kujua ili suala vyuoni kwao wanafanyaje.
Kwakweli, lipo lakini halitokei kwa mwanafunzi kwani kufanya mtihani wa UE ni sehemu pia ya kumuinua mwanafunzi na ku toa kwenye ile under 16 aloipata. Lakini chuo hiki kimeigeuza hii Carryover under 16 kama fimbo ya kuwasulubu wanafunzi na kuqaogopesha katika masomo yao, kwa sababu hata bila sababu za msingi.
Lecturer anaweza kumtongoza/kumtaka mwanamke kimapenzi, akikataliwa, binti alokataa atarudia mwaka. Au Lecturer hajakuelewa mwamba, muonekano wako wa kidharaudharau basi ujue mwaka utarudia. Na wamerudia wengi na pia wengi wameacha chuo sababu kubwa ni hii, ni hii kurudishwa mwaka mzima kulisoma somo moja tu ulilopata Carryover under 16.
Ombi langu.
1. Wasomi wakae chini na kuondoa sheria hii. Kwani, haina msaada kwa mwanachuo, kurudia somo moja mwaka mzima hakufanyi kulipenda au kulijua zaidi ya kulichukua na kumchukia Lecturer wa somo hilo.
2. Imekuwa njia ya kushawishi wadada kuingia kwenye rushwa ya ngono, Lecturers wanaitumia sheria kukandamiza mtu anayemkataa, na kuwatesa vijana wa kiume hasiowaelewa.
3. Inakuwa chanzo cha kuwavuruga wanachuo na msongo wa mawazo. Chuoni hapa, mwanachuo amewahi kujitupa chini toka ghorofa ya nne na kuvunjika miguu yote, sababu ya msongo wa mawazo uloletwa na hiyo sheria ya Carryover under 16. Wengine wengi, nawafahamu zaidi ya 10 mimi binafsi waloachana na chuo hiki sababu ya kupata hiyo Carryover.
4. Ni hasara kwa mzazi/mlezi kwani itambidi alipie somo wakati wa kurudia semester hiyo husika. Kama anapata mkopo, hautambui hii Carryover hivyo mwishowe lazima atalipa.
Nini kifanyike:
Baada ya kufuatilia sana, kwenye vyuo vikongwe na vikubwa hapa nchini. Haya ni moja ya namna za kufanya kwa chuo kikubwa kwa eneo la square meter, lakini kidogo kitaaluma.
1. Somo/course moja ifundishwe na walimu zaidi ya wawili. Wasomi wengi kipindi hiki webye ubavu na weledi mkubwa. Hii itapunguza chuki, na miemko ya kihisia baina ya mwanafunzi na mwalimu wake. Si rahisi kwa walimu watatu au zaidi kumuandama mwanafunzi mmoja kwa chuki au upendeleo wowote.
2. Matokeo yawekwe na jopo tofauti na walimu husika. Mwalimu apeleke matokeo kwa jopo husika, wao wajadili matoke ndipo waweke kwenye mifumo ya chuo.
4. Dean wa chuo, hasa chuo hiki kikubwa wawekwe wazi na kazi zao bayana kwa wanafunzi wote. Huyu ni mtu muhimu sana, japo elimu hii ni ya watu wazima. Ikumbukwe, watu wazima ndio uendesha familia, watu wazima ndio kioo cha watoto, watu wazima ndio wajenzi wa sasa wa taifa hili. Familia, ndugu, jamaa zinamtegemea mtu huyo anaepata elimu ya juu kabisa. Hivyo ni vyema kuhakikisha mtu huyu anafikia anapostahili kwaajili ya wengi na taifa kwa ujumla.
4. Vyuo viwe na dawati la saikolojia na kujiweka wazi (Psychology and openness). Hii itasaidia wanachuo kufunguka yanayowakabili na kutafuta utatuzi wa yale yanayowakabili. Ikiwezekana wanachuo wenyewe waunde jopo hili kwa utashi wao kuhusisha wanachuo wote (yaani waendeshaji na wanafunzi)
Mwisho:
Taifa hili halipo linapostahili, sababu ni uzembe na ujivuni wa wasomi tulionao. Wasomi wanalewa madaraka, vyeo na pesa wanazopata. Hiyo inawafanya kuwadharau wengine, kuwakandamiza wanaotafuta usomi, na kujihakikisha kama wasemi wa mwisho.
Elimu haina mwisho, hata usome vipi, kuna walosoma zaidi yako na wapo wasiosoma kama nyie wasomi na wanafanya makubwa mazuri zaidi ya usomi mlonao wasomi. Wasomi tumieni usomi wenu kama daraja la kuwafikisha wengi mbali zaidi.
Haikupunguzii chochote zaidi ya kukuinua wewe zaidi. Dunia ya sasa huwezi kumfunga mtu kirahisi kwa njia moja. Utamnyima degree ya udaktari leo, kesho ulomnyima degree atamuajiri mwanao. Wenzetu walioendelea wanatoa degree mpaka kwa paka aliyeishi chuoni miaka minne. Vyeti havijawahi kuwa maisha ya mtu, utu ndio maisha halisi.
Daktari mwenye cheti kizuri chenye A's za kutosha bila utu ni sawa na bure. Hata tusome vipi, na tujaze degree kibao mtaani, taifa hili bado linahitaji wasomi wengi zaidi. Tupo nyuma sana kiuelewa kwa wasomi na wasio wasomi. Chuo sio mahali pa kufeli, mtu kafaulu elimu zote alizopata huko akiwa hajielewi, aje afeli chuo kikuu. Nadhani chuo kikuu ni elimu saidizi, kwamba mtu tayari anajua mengi ila kumsaidia sasa aweze kufanya jambo kwa mafanikio kwa mafunzo stahili atayopata.
Habari hii naomba ifuatiliwe, ikiwezekana angalieni uwiano wa wanafunzi dahiliwa wanaoanza chuo kikuu hiki kikubwa kwa wanafunzi hitimu wa kozi hizo za afya. Kisha, tafuta sababu ya uwiano ya dahiliwa na hitimu. Niko 90% sure Carryover inaongoza.
Hide my Identity