Mufindi: Polisi waua watu watano kwa madai ni majambazi

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewaaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huku wengine saba wakidaiwa kukimbia katika majibizano ya risasi yalitotokea kiwanda cha Daazhong, kilichopo Changarawe, Mafinga Mjini wilayani Mufindi.

Watu hao wameuawa katika majibizano ya risasi yaliyotokea baina yao na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa, Septemba 30, 2022 saa 8 usiku katika tarafa ya Ifwagi baada ya polisi kuweka mtego kwa ajili ya kuwakamata waharifu hao.

Amesema mtego wao uliweza kuwanasa majambazi 12 ambao tayari walikuwa wamevamia kiwanda cha Daazhong ndipo askari walipowaamuru wajisalimishe lakini walikaidi na kuanza kujibizana kwa risasi.

“Jeshi la polisi lilipokea taarifa kuwa majambazi ambao wamekuwa wakijihushisha na uhalifu na walikuwa wamepanga kufanya uhalifu katika kiwanda kiitwacho Daazhong ndipo waliweka mtengo na kufanikiwa kuwauwa majambazi hao na wengine saba wakafanikiwa kutoroka lakini tunaendelea kuwatafuta ili kuhakikisha wote wanakamatwa.” Amesema Bukumbi

Kamanda Bukumbi amesema watuhumiwa hao walifariki wakiwa wanakimbizwa katika Hospitali ya Mafinga kutokana na majeraha ya risasi waliyoyapata.

Aidha, kamanda huyo alitaja baadhi ya vitu ambavyo wamefanikiwa kupata ni silaha mbili moja ikiwa aina ya shotgun ikiwa na risasi zake (13) na nyingine ni pump action, mabegi Mawili madogo ya mgongoni lakini begi moja ndani walikuwa likiwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania

Pia, ametaja vitu vingine kuwa katika Begi la pili walifanikiwa kukuta sare za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jacket moja la mtumba ambalo linafanana na kombati za jeshi, shoka moja, nyundo moja na kitambaa kimoja kinachofanana na kombati za jeshi sanjari na Line za simu za mitandao mbalimbali ikiwemo tigo (12),Airtel (25),na Voda (7)

MWANANCHI
 
Kama wanachodai ni kweli Bravo Mapolisi wetu.
 
Dah, hili wimbi la majambazi, linaongezeka kila kukicha.

Kuna mdau humu aliwahi kutoa angalizo kwa hawa JKT wanao rudi nyumbani kwa kosa ajira, watatusumbua sana aisee
 
Kama ni kweli yalikuwepo majibizano police wapewe tuzo kwa kuwarudisha majambazi kuzimu kwa hiari
 
Nondo nenda Mufindi kesho tena ukafanye mahojiano usisahau kulipia maturubai ,viti na maji ya uhai.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewaaua watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huku wengine saba wakidaiwa kukimbia katika majibizano ya risasi yalitotokea kiwanda cha Daazhong, kilichopo Changarawe, Mafinga Mjini wilayani Mufindi.

Watu hao wameuawa katika majibizano ya risasi yaliyotokea baina yao na polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Allan Bukumbi amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa, Septemba 30, 2022 saa 8 usiku katika tarafa ya Ifwagi baada ya polisi kuweka mtego kwa ajili ya kuwakamata waharifu hao.

Amesema mtego wao uliweza kuwanasa majambazi 12 ambao tayari walikuwa wamevamia kiwanda cha Daazhong ndipo askari walipowaamuru wajisalimishe lakini walikaidi na kuanza kujibizana kwa risasi.

“Jeshi la polisi lilipokea taarifa kuwa majambazi ambao wamekuwa wakijihushisha na uhalifu na walikuwa wamepanga kufanya uhalifu katika kiwanda kiitwacho Daazhong ndipo waliweka mtengo na kufanikiwa kuwauwa majambazi hao na wengine saba wakafanikiwa kutoroka lakini tunaendelea kuwatafuta ili kuhakikisha wote wanakamatwa.” Amesema Bukumbi

Kamanda Bukumbi amesema watuhumiwa hao walifariki wakiwa wanakimbizwa katika Hospitali ya Mafinga kutokana na majeraha ya risasi waliyoyapata.

Aidha, kamanda huyo alitaja baadhi ya vitu ambavyo wamefanikiwa kupata ni silaha mbili moja ikiwa aina ya shotgun ikiwa na risasi zake (13) na nyingine ni pump action, mabegi Mawili madogo ya mgongoni lakini begi moja ndani walikuwa likiwa na sare za Jeshi la wananchi wa Tanzania

Pia, ametaja vitu vingine kuwa katika Begi la pili walifanikiwa kukuta sare za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Jacket moja la mtumba ambalo linafanana na kombati za jeshi, shoka moja, nyundo moja na kitambaa kimoja kinachofanana na kombati za jeshi sanjari na Line za simu za mitandao mbalimbali ikiwemo tigo (12),Airtel (25),na Voda (7)

MWANANCHI
Mungu ndiye anajua ukweli, kwa polisi wa Tanzania, correct statement can not be said over them!
 
Hongereni jeshi la polisi kwa kazi nzuri, naimani waliotoroka watapatikana
 
"Polisi waliweka mtego, majambazi yakaanza kuwarushia risasi Polisi kisha Polisi wakajibu, majambazi wakajeruhiwa wakafa wakati wakikimbizwa hospitali".... Hii kauli Polisi huwa wanafundishwa chuuoni.
 
Hawa jamaa kwa kutengeneza muvi tu, hawajambo. Usikute hata hayo majibizano yenyewe ya kurushiana risasi hata hayakuwepo!

Sema tu ndiyo vile nchi yetu kwa sasa haina utawala wa sheria. Hawa jamaa kama wameruhusiwa vile kuua watu hovyo hovyo kwa kisingizio cha ujambazi na upanya road.
 
Back
Top Bottom