Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Yaani Mufti mzima ameshindwa kuzungumzia haki? Hili neno HAKI inaonekana halipo kabisa katika vitabu vinavyotumiwa na BAKWATA.Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) litaendelea kusimamia maslahi ya Taifa, huku akiwataka Watanzania kuendeleza uzalendo na kulinda amani ya nchi.
Mufti Zubeir ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe, alipokutana na baadhi ya viongozi wa dini na serikali, ambapo amesisitiza kuwa jukumu kuu la BAKWATA ni kuhimiza amani, umoja, na uzalendo miongoni mwa wananchi.
“Tunaizungumzia amani na uzalendo kwa sababu tunajua umuhimu wake katika Taifa. Wapo wanaodhani sisi ni vibaraka wa serikali, hapana — hatutumwi na serikali. Tunatambua wajibu wetu wa kuisaidia jamii kuelewa maana ya kuwa mzalendo wa kweli,” alisema Mufti Abubakar Zubeir.
Ukiongeza neno moja tu:"HAKI" kwenye maneno haya; nitakubaliana na maoni ya kiongozi huyu wa dini.Mufti Zubeir ametoa kauli hiyo leo Oktoba 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Njombe, alipokutana na baadhi ya viongozi wa dini na serikali, ambapo amesisitiza kuwa jukumu kuu la BAKWATA ni kuhimiza amani, umoja, na uzalendo miongoni mwa wananchi.
HAPANA.Mufti ni kama anataka kujisafisha, na wakati ukweli ndiyo huo! Tena siyo vibaraka tu! Bakwata pia ni tawi tiifu la ccm!
Tena anahudumiwa na serikali. Huyu jamaa ni hovyo sana.Mufti ni kama anataka kujisafisha, na wakati ukweli ndiyo huo! Tena siyo vibaraka tu! Bakwata pia ni tawi tiifu la ccm!