Sekenke,
Mkuu sasas wewe unaanza udini na kupotosha watu. Mahakama ya kadhi haihusiani kabisa na hukumu za makosa ya jinai Pleasee!.
Kisha kibaya zaidi ktk mjadala huu wamejaa wakristu wasiojua Uislaam ni kitu gani.. acheni waislaam wenyewe tujibu hoja hizi badala ya kutoia majibu yenu huku mmeshika Biblia mikononi.
Mtazame Mwanakijiji ambaye watu kibao wanamuamini humu anakuja na swala ya kuona kama swala hili ni Muhimu kwa Waislaam kuliko yote yanayozungumzwa, utafikiri huwa anapiga kelele yeye peke yake na kanisa lake..Wao, wao...them, them - ndio hoja yake ya msingi!
Mkuu Mwanakijiji, hawa ni Viongozi wa dini na wanawakilisha waumini wa dini, hii ndiyo kazi yao kidini sii kuingilia Siasa ambazo hawana hata hzihusiani na dini wala hawana elimu nayo..Ikiwa Mapadre wenu wanaingilia Siasa hata ktk maswala yasiyohusiana na ibada zenu hiyo ni Ukristu wenu, usitake kuwavuta waislaam pia kuiga yanayopfanywa na Wakristu. Mufti akiingilia siasa hizi basi jua anazungumza kama raia mwninge na anaweza kuja hapa kijiweni kama Mkandara!
Wanabodi,
Nitarudia kusema hivi siku zote HOJA hujibiwa na HOJA ikiwa mnapingana na huyu Mufti njooni na hoja inayoweza kuivunja nguvu hoja ya huyu Mufti lakini kuingia hapa na Gear zenu za Ukristu mnaonekana wapuuzi tu..Hivi akili zetu hukoma kufikiri inapofikia maswala ya dini jamani?
Utafikiri mnamjua yesu kuliko yesu mwenyewe! Looh - salaaaala!
Kuna makosa mengi kayasema huyu Mufti na mtazamo wake umekingwa na vumbi kiasi kwamba anatakiwa kuelimishwa zaidi..Na sii kuja na hoja zilizojaa pumba zaidi ya Mufti mwenyewe.
Hakuna Sura wala sheria yoyote inayosema ni lazima Muislaam jina, ndiye atoe hukumu ya kesi za madai..hasa ktk nchi ambayo Waislaam wanaoana na Wakristu. Hayo madai ya kwamba Mkristu hawezi kumhumu Muislaam ni opofu mkubwa sana kwa sababu kama kweli yeye ni Muislaam safi na madai yake yanafuata elimu yake ya dini basi bila shaka hata mahakama za jinai angepinga hukumu zake! hukumu zake hazilingani wala kufanana na Uislaam, tofauti ya mahakama hizi mbili ni uzito wa kesi zenyewe tu lakini wanaohukumiwa ni pamoja na waislaam...Hivyo basi ni ujinga kukubali hukumu za mahakama moja ukapinga mahakama nyingine tena ndogo zaidi yenye maswala madogo ya madai.
Waislaam wengi hawawezi kumsikiliza mjinga huyu wala kufuata ushauri wake..namwita mjinga kwa sababu hafahamu Utawala na kikubwa zaidi kama Mufti ameshindwa kutazama WATU, MAZINGIRA na Elimu dunia kuwa kigezo kikubwa cha hotuba yake. Ni hawa hawa wajinga wanaofanya waislaam tanzania wanafunga mwqezi wa Ramadhan siku mbili tofauti kwa sababu tu ati mwezi haukuonekana Dodoma au Dar.. Wangejua kwamba huku Canada kuna sehemu inaitwa Yellow Knife Jua huwepo miezi sita bila usiku wa kiza na wakati mwingine Usiku kwa miezi sita vile vile, sijui wao watafunga vipi Ramadhani ikiwa sababu ni kuuona mwezi, hiyo sayansi ya miaka ya nabii Nuhu..Kisha basi Sayansi ambayo ina justify maelezo mengi ya Kuran inaonyesha wazi kwamba dunia nzima tofauti yetu ni kwa masaa 24 tu..Ikiwa na maana hatupishani kwa siku nzima,sasa kwa nini nchi zifunge Ramadhan siku mbili tofauti..
Kisha basi kiibaya zaidi ni kwamba siku ya Idd Hajj sisi hatuongezi ziku moja zaidi wala kusali tofauti na Saudia..Why tuna sababu gani ya kukatiza kufikia Al Hajj lakini tunakataa siku ya mwezi wa Ramnadhan na siku ya Idd El fitr!.. Hawa mai Mufti wa kuchalkiwa na CCM hiyo hiyo!
Wakuu zangu watu kama hawa tuachieni sisi, tunawajua vizuri sana kwamba hawa ni Wanafiki wa Dini, huwezi kuihusisha dini ktk siasa kwa sababu ya Mahakama ya kadhi ambayo hata sisi waislaam wengine tunaona ni kupotosha..
Matatizo yote mnayotaka kuyashughulikia hayana sheria kwa Waislaam zaidi ya kubakia vitabuni. waislaam wanaoa wake bila sababu za msingi na wafungishaji ni hawa hawa Ma Mufti!, Waislaam wanaoa nje ya dini zao, wanazaa nje ya ndoa zao, watoto waliozaliwa mnawaita wana haramu na kuwanyima Urithi..hivi kweli mtaweza kutoa haki kwa wahusika!
Hapana, nasema hapana kwa mahakama ya Kadhi, hatuihitaji ila tunahitaji sheria ziundwe kuwabana wazazi wanaowanyanyasa wake na watoto ktk ndoa na mirathi..Sheria ambazo zinaweza chukua yaliyo bora toka ktk Uislaam na mengine nje ya Uislaam kwa sababu tunachotaka zaidi sisi wananchi Waislaam ni kulinda haki za victims kama hawa watoto mnaowaita haramu, wake mnaowaita Mistress na kadhalika kwa sababu tu ndoa haikufungwa kufuata misngi ya Kiislaam au Kikristu..Sheria ambayo inakuwa msumeno kwa yeyote yule atakaye tumia dini kama kisingizio cha kufanya ayatakayo kinyume cha ustaarabu...