Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

Game Theory kumbuka kuwa Tanzania umezaliwa umeikuta na utakufa utaiacha but Waislamu na Wakristo wapo na wataendelea kuwapo. Dhambi ya ubaguzi wa dini ni kitu kibaya sana.

Kuhusu ufisadi data zote zilizotelewa except radar hazina substance wala proof zaidi ya barua ambazo hazisigniwa na wahusika. Fulani amekutana na fulani, na zaidi fulani alinunua kampuni fulani. Kumbuka mtuhumiwa katika court huwa anatizamwa kama si mkosa hadi vielelezo vimtuhumu kuwa ni mkosa. Katika forums mengi yaliyoandikwa ni wivu na chuki ambazo watu fulani wanazo kwa watu wengine. Sidhani kwa mtu mwenye hekima hili ni jambo la kukimbilia mfano kama mtu unamtuhumu ni fisadi leteni data zinazoonyesha alichukua fedha from account ya kampuni x kwenda Y na haya malipo yawe yamejitosheleza kwa vielelezo na sio fulani amefungua kampuni tu basi hiyo haina msingi kwani Tanzania ni nchi huru hivyo basi kila mtu anahaki ya kufanya kitu cha maendeleo.

Kimsingi mahakama ya kadhi ni sticky issue na serikali isipotumia busara nafahamu waislamu ni watu huwa na hasira na jazba za haraka. Sidhani kama wamewatendea haki. Isitoshe nawaelewa serikali watakuja kuwapoza na OIC wakidai eti OIC inafaida kwa Tanzania. Hilo litakuwa halitoshi kwani tutaanza kuhoji misaada ya OIC nyuma ilikuwa ikienda wapi na kina nani wamenufaika na tupate data maana data za OIC zipo za misaada je Tanzania wanaweka record zao tuzione. Kimsingi serikali ilikuwa na advantage kwenye mahakama ya kadhi kwani iko katika mipaka yao wangelitazama wenzao wa jirani wamefanyaje. Bila hivyo tanzania haitakuwa tena nchi ya amani tuliyoizoea ambavyo jirani yako ni muislamu wewe mkirsto na hapo tutakuja kuyakumbuka maneno ya baba wa taifa aliyesema dhambi ya ubaguzi ikianza inasambaa kwa kasi ya ajabu
 
wewe mkristo inakuhusu nini?
Unajuaje walichokosa kwenye mahakama mama?
wapeni haki zao what is the issue here?

Mahakama zianzishwe nje ya mfumo wa serikali! Unajua Kadhi Mkuu Zanzibar anateuliwa na Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa The Kadhis Courts Act, 1985?
 
Sidhani kuwa kauli ya Sheikh Mkuu (Muft) inaashiria nia ya kutoipigia CCM kura. Nadhania anachotaka kukifanya ni kuonyesha hasira zake kuwa muda unakwisha na hakuna jitihada za wazi za kutekeleza ahadi anayodhani walipewa kuhusu kuanzishwa kwa Kadhi Mkuu.
Nakuhakikishia, hata serikali isiposema lolote, watu wataipigia kura tu. Ni maajabu kama hayo ndio yanayofanya mijadala iwe mirefu.
 
Waislamu hawajakatazwa kuwa na mahakama zao kwa ajili yao, ila wakitaka wazianzishe kwa utaratibu wao ndani ya misikiti yao kwa ajili yao na kwa gharama zao wenyewe, sio kuchangiwa na wananchi wote.

Wasilazimishe mahakama za kiislamu zianzishwe na Serikali ili zilipiwe kodi na watu wote (waislamu, Wakristo na wasio na dini), na ili ziajiri waislamu tu.

Wenzetu hawa huwa wanaweka kando mabaya yote wakishupalia dini, ndiyo maana ukiwaambia mbona hamsemi mtaikacha CCM kwa ajili ya EPA, RICHMOND/DOWANS, DEEP GREEN, TANGOLD, MWANANCHI GOLD, MEREMETA, IPTL, KIWIRA wanabaki mhhh...

Anyway, wakiiacha CCM itakuwa poa tu, watarudi kwao CUF...
 
Naunga mkono Serikali haijatenda haki sawa hapo,kwani inachelea nini kuwapatia haki yao ya msingi jamii ya kiislam Tanzania ilhali nchi jirai wameweza. watoe sababu za msingi sio tu kuishia kukataa kutoa kile wananchi wake(muslims) wanahitaji na ikiwezekana waitishe hata kura ya maoni na midahalo ili kuweka nini tatizo. kwa mtazamo wangu WAPEWE MAHAKAMA YAO ili watoe suruhu zinahusiano na imani yao.
Kwani bila hivyo sidhani kama misingi yao ya kiimani itakuwa iko timilifu.
 

Suppose CCM wakafanikiwa kutekeleza ahadi zote hata baada ya 2010 isipokuwa la kadhi watabadili mwelekeo? Inaonekana kama vile kadhi ndio muarobaini wa matatizo yote nchini wakati suala lenyewe linahusu ndoa, talaka na mirathi. Sijajua hili la kukata watu mikono huwa liko kwenye sheria ipi ya Kiislamu!
 
Kura watapiga tu,watakipigia chama gani ni siri ya mtu mwenyewe.
 
CCM itashinda kwa kishindo kikuu.

Kuna watu walisema piga ua lazima mahakama ya kadhi ianzishwe, sasa hivi hawaamini masikio yao! Mwakani watashangaa tena vitisho vya kutokipigia kura ccm kitakapokuwa kama kelele za chura zisizoweza kumzuia ng'ombe kunywa maji!
 
Mahakama ya Kadhi iruhusiwe kuundwa na Waislamu chini ya Sheria ya Non-Governmental Organizations (N.G.O.).

Taasisi hiyo ishughulikie tu mashauri baina ya waumini wa Kiislamu ambayo si ya jinai, na endapo hukumu ya Mahakama hiyo haitamridhisha mmoja wa wahusika, akate rufaa katika mahakama za kiraia za kawaida.

Gharama za Taasisi hiyo zisilipiwe na fedha za walipa kodi wa Tanzania (yaani Serikali), bali kama NGO nyingine, Mahakama ya Kadhi iweze kukusanya michango ya hiari toka kwa waumini wa Kiislamu na wafadhili wengine wa ndani na nje.

Kama Taasisi nyingine ktk kundi la N.G.O.s, Serikali itataka kujua Mahakama ya Kadhi inaendelea vipi. Kwa hiyo Mahakama ya Kadhi itakuwa inawasilisha Serikalini repoti na accounts zake za mwaka, zilizokaguliwa na Mkaguzi anayekubalika chini ya sheria za Tanzania.

Naamini ni kinyume na Katiba ya Tanzania kuingiza Sharia Law au Canon Law katika orodha ya Sheria za nchi yetu. Katiba inatamka kwamba Tanzania haina dini maalum, na kila mtu ana haki ya kuabudu jinsi anavyoamua yeye mwenyewe. Pia inatamka kwamba kila mtu atakuwa sawa mbele ya Sheria, na sheria yoyote ktk Sheria zetu itamhusu kila mtu bila ubaguzi.

Endapo Serikali ya J.K., ikishauriwa na Mathias Chikawe, itang'ang'ania kuingiza sheria za Kiislamu (yaani Sharia Law) katika sheria zetu na kuzirekebesha eti ili ziwiane, watakuwa wanakiuka Katiba. Na kwa kweli hakutakuwa na mwisho: maana Wakatoliki nao watataka Canon Law nayo iingizwe katika Sheria za Tanzania, na Torat ya Wayahudi pia inaweza kutakiwa kuingizwa! Sijui wapagani watataka kuingiza sheria na mila zipi.

Sasa hivi, mashauri mengi yahusuyo urithi na maisha ya ndoa hushughulikiwa na vikao vya ukoo kulingana na mila, utamaduni na desturi za jamii husika. Nyingine hushughulikiwa na vikao vya viongozi wa kanisa. Pale inaposhindikana, wahusika wote huenda mbele ya mahakama za kawaida. Kwa hiyo Mahakama ya Kadhi ingeweza kutambuliwa tu kama ni mpangilio wa kusuluhisha mashauri baina ya Waislamu, tofauti ikiwa na kwamba BAKWATA wataratibu mambo kitaifa, kulingana na Sharia Law.
 
...
Kimsingi mahakama ya kadhi ni sticky issue na serikali isipotumia busara nafahamu waislamu ni watu huwa na hasira na jazba za haraka.
Haa haa haaa!! Kwamba serikali itumie busara kwa kuwa waislamu huwa na hasira na jazba za haraka!!! Sasa kwa nini waislamu nao wasiwe na busara kama serikali inavyotakiwa iwe?
 
Kama ilivyo kwa wakatoliki period!!
 
Kwani Lipumba anaipigia debe hii mahakama?
 
Hiyo ahadi haikuwa absolute, ila ccm ilikuwa inaangalia uwezekano wa kuanzisha mahakama ya kadhi!

Eee sawa mkuu mliangalia uwezekano sasa mme wezekana!

Uroho wenu wa kura mnarukia vitu ambavyo vinaivunja katiba! eti iingizwe kwenye katiba, lakini waislamu tu ndo watoe maoni? na waislamu tu ndo wawe mahakimu? Kwahiyo itabidi serikali isomeshe mahakimu wa kiislamu kwa ajili ya kuhudumia mahakama hizo? yaani yaaani...
 
Mimi nilishawahi kusema kuwa CCM ndio waliyataka mambo haya, Kwanini wanafanya hivyo?? Walijua na Jk alijua hilo kuwa kwenye Ilani ya CCM kuna Mahakama ya Kadhi. Sasa Waislamu wana Haki ya Kudai hilo.. Kama wao walijua linashindikana waliliweka la Nini?? Mbona Jk alisema kuwa anajua Ilani ya CCM??Basi wakubali kuwa ILani ya CCM haitekelezeki??
 
Waseme Watakuwa Upande gani?? Tunataka waseme watakuwa upande gani??
 


Mkuu umegusa ukweli wenyewe. Ukiangalia tatizo jingine la uongozi wa taasisi za kiislamu utakuwa, hii inayoitwa elimu dunia ni kama haipo. Kama ipo basi ipo kiduchu sana. Ukiangalia viongozi wa TEC hata leo ukiwataka waunde serikali wanaweza kuunda serikali yenye mwelekeo, lakini ukisema uwape leo Bakwata unaweza kufikiri mara kumi. Jaribu kuangalia CV za watu wa TEC, hata wakristo wenyewe hawana tatizo na uwezo wao, ndio maana hata serikali haioni haja ya kuwasumbua au hata kuwa na wasiwasi nao, wanajua uongozi wao unafanya mambo kwa makini. Hata kama una tatizo nao wanajua kuwa kuna channels ambazo wanaweza kuzitumia kushighulikia mambo yao. Hili kwenye Bakwata lina walakini kidogo, hata waisamu wenyewe wana malalamiko mengi kuhusu taasisi yao.

Kama wasaidizi wa Sheikh wangekuwa ni watu ambao wamekwenda kitambo kidogo kwenye elimu dunia, basi wangeweza kuongoza hata mambo ya elimu ya akhera vizuri sana.
 
Tusiongee Dini hapa jamani tuongee masuala kwanini CCM iliweka Mahakama ya kadhi kwenye Ilani ya CCM?? Walikuwa na ajenda gani?? Mbona walikuwa wanasema kuwa wanaitekeleza Ilani mpaka sasa??Jk alipita kifua mbele kwa kusema kuwa anaitekeleza ilani hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…