Elections 2010 Mufti Simba asisitiza watanzania kutopiga kura kwa misingi ya kidini

Elections 2010 Mufti Simba asisitiza watanzania kutopiga kura kwa misingi ya kidini

The Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2009
Posts
1,282
Reaction score
21
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku wa leo (TBC) Shehe Mkuu Simba amewajia juu viongozi wa dini wanaohamasisha wafuasi wao kupigia watu fulani. Nina wasiwasi hii itaongeza tension maana tunakoelekea ndiko siko. Habari ndio hiyo
 
Yuko sawa kabisa kama wameshindwa kwa ukabira sasa njia rahisi ni udini tafakari chukua hatua
 
kama angekemea na udini ule unaohamasisha waislamu misikitini kupigia kura waislamu wenzao na si vinginevyo, ningempa tano. Otherwise ni unafiki tu.
 
Nakumbuka 2005 kabla Kikwete hajateuliwa kuwa mgombea wa CCM masheikh fulani waliwataka waumini wao wasipigie kura CCM.
 
Mimi kwa jinsi nilivyo sikia kaongelea in General terms iwe kwa waislamu au kwa wakristo, kwamba no one of them should vote according to her/his religion.

Labda kama hiyo statement imechujwa/kukachuliwa.

Sasa ukitaka kwenda zaidi nani ni mlengwa inabidi uangalie ni akina nani walio kuwa wanaongelea watu wampigia kura mtu kufuatana na Dini yake? Is it Kakobe, TEC, CCt, kkkt, au baadhi ya misikiti au baadhi ya waumini nk.

lakini ukienda huko naona tutachafua hali ya hewa, madhali watu wameisha elewa somo, na kuona hali hii haita wafikisha popote, na hali hii pia inakiadhiri chama tawala na baadhi ya viongozi wake wasio wadini fulani? kikristo/kiislamu ndio maana imebidi kauli hii itoke.

aisee! shombo!

hivyo namuunga mkono ingwa wanachelewa chelewa saaana kutoa matamko kwa wakati kabla madhara haya jawa makubwa
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku wa leo (TBC) Shehe Mkuu Simba amewajia juu viongozi wa dini wanaohamasisha wafuasi wao kupigia watu fulani. Nina wasiwasi hii itaongeza tension maana tunakoelekea ndiko siko. Habari ndio hiyo
Jamani kuna siku niliwahi kusema hapa kwamba baadh ya waislamu wenzangu, hawana haja na kujua mustakabali wa taifa hili, wanachowaza kwao ni udini tu, huyu si muislamu ata kama ni kiongozi mzuri.
 
Mimi ni Mwislam safi, nilitegemea kauli ya jopo la ma-sheikh lingezingatia kuwahamasisha watanzania kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuiongoza nchi yetu kufikia maendeleo yanayotarajiwa...
 
Kwangu mimi Bakwata ni adui nambari wahid wa jamii ya waislamu Tanzania.

Hata hivyo ni wazi kuwa amechelewa kusema maana katika wakati tuliopo watu tayari wamewiva udini kiasi kwamba hata anapoongea watakimbilia kumnyamazisha lakini pia kutengeneza mazingira kuwa anamtetea mgombea mwislamu mwenzake zaidi ya amani ya Tanzania.

Ningefurahi angetumia nafasi hii kukemea misikiti inayoendesha kampeni za kumchagua Kikwete mradi tu ni muislam. Hayo ya Kakobe and the like angewaacha kina Malasusa na pengine Kilaini kuwa na uthubutu wa kukemea kwa upande wao.
 
Mimi ni Mwislam safi, nilitegemea kauli ya jopo la ma-sheikh lingezingatia kuwahamasisha watanzania kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuiongoza nchi yetu kufikia maendeleo yanayotarajiwa...
Kama alivyo fanya kakobe....
 
Sheikh Simba (Nyau in this case) ameonekana kuanzisha malumbano kwani viongozi wa Kikristo walisema tusiangalie maisha binafsi ya mtu, yeye anasema tuangalie maisha binafsi (ambayo sidhani kama yanatusaidia sana zaidi ya dhamira ya mtu). Waislamu ndio wadini namba moja na nimewasikia mara nyingi misikitini na hata wakikutana wakimpigia debe muislam mwenzao ingawa si kwa kumtaja moja kwa moja.

Ningeshauri viongozi wa dini wakae kimya ( wanawachanganya waumini wao) , makamba na kinana wanatosha kumwaga upupu wa ccm.
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku wa leo (TBC) Shehe Mkuu Simba amewajia juu viongozi wa dini wanaohamasisha wafuasi wao kupigia watu fulani. Nina wasiwasi hii itaongeza tension maana tunakoelekea ndiko siko. Habari ndio hiyo

Mkuu nadhani huko sahihi na alichokisema Sheikh mkuu ni general statement kuhusiana na viongozi wa dini na uchaguzi kitu ambacho ni sahihi kabisa. Sasa sielewi malengo ya hii thread yako. Ila kila la kheri muungwana
 
Hivi Londa alipopiga Kampeni Msikitini Mufti Alisema Chochote Kuhusu Hili? Mufti amechelewa Kauli yake ingekuwa na Mvuto kama angeitoa wakati Baadhi ya waislam ( Kama Londa) Kutumia Swala ya Eid kupiga Kampeini, Hata kama Kauli yake ya Leo ina nia Nzuri lakini ni Rahisi sana kuonekana kama Anamjibu Kakobe
 
Simuelewi huyu bwana, mbona wao ndo wanahamasisha wachaguliwe watu wenye imani sawa na wao? Nadhani angeawaambia wenzie siku ya ijumaa manake yanaanzia hukohuko!
 
Katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku wa leo (TBC) Shehe Mkuu Simba amewajia juu viongozi wa dini wanaohamasisha wafuasi wao kupigia watu fulani. Nina wasiwasi hii itaongeza tension maana tunakoelekea ndiko siko. Habari ndio hiyo
Waislamu tusipoangalia sisi ndo tutakao leta matatizo makubwa katika nchi hii. Hakuna kiongozi yoyote wa kikiristo ambaye amempigia debe mgombea bali wamesema wasifu wa kiongozi anatakiwa kuwaje. HAKUNA KITU KINACHONIUDHI KAMA HAYA MAMBO YA UDINI. HAKUNA DINI ILIYOBORA . NA NDIO MAANA TUNATAKA RAISI MSAFI KATIKA UONGOZI WAKE AWE MUISLAMU AMA MKRISTO
 
Kule Tunduru alienda RiziWani Kikwete akakuta watu wanaambiwa wasimchague mgombea wa ccm kwa kuwa ni kafiri... Naskia Sumbawanga mjini wanaambiwa wasimchague mbunge wa ccm kwa kuwa ni muislam.

wa maana hiyo hali imeishakuwa mbaya tayari, na ukiangalia wale Masheikh walioongozana na Simba vizuri usoni wanaonekana kama wanatoa tamko kwa shinikizo fulani na tayari wameishachagua tayari mgombea fulani. Kwa mtazamo wangu pale ni unafiki mtupu, wameona hali ya baba wa taifa ni mbaya wanajaribu kuokoa jahazi lakini kumbe wanachochea udini zaidi.
 
Mambo ya kuleta udini ni hatari. Wahusika waache mara moja. Lakini wadau mnaonaje hili? Hivi ni kweli hii nchi ina dini? Nashauri waache mambo hayo. Au wametumwa? Hii inaweza kuwa njama. Tafakari, chukua hatua.
 
Sasa ningependa kuona viongozi wa vyama vyote wakianza , jemedari wetu J Mrisho K, akitoa tamko kama hilo, na Silaa, Lipumba, nk nk na ikiwezekana Viongozi wa TEC, CCT nk au ikiwezekana wote kwa siku moja mahali pamoja moja baada ya mwingine watoe kauli kama hii, na kukemea tabia ya baadhi yetu, makanisa/msikiti nk kutumia udini au kupigia upato kwa kutumia dini. Na ikiwezekana kuwaapisha kwa dini zao kutotumia dhana ya udini ili kushinda kula
 
CCM wenyewe wadini.

Kwani huyo Shehe chama gani?

Kwenda huko!!

Ng'wanangwa toa quote yako hapo chini, mimi ni mkristo lakini innikwaza sanaaaaa
sizani kama hapo unawazungumzia CCM zaidi ya kuharibu sifa nzuri ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom