#COVID19 Mufti Zuberi: Ibada ya Hijja imefutwa kwa sababu ya Virusi vya Corona


Mkuu Lituye habari.

Mimi ni Mkristo "Born Again Christian" LAKINI niseme ulichoandika hapa kuhusu waislamu na ibada ya hija sio sahihi kabisa na ni busara kama utaomba Radhi; "Kuomba radhi ni dalili ya Unyenyekevu"

Ahsante
 
Taarifa yenye maneno ambuiguity.

Imefutwa and Watakao hiji ni waliokuwa tayari huko huko Saudia!

Elimu elimu elimu.
 
Kwa hiyo lakini siku kuu ya Eid El Haji itakuwepo kama kawaida muda utakafika au ?
 
Habari wadau..!
Ni mwaka wa pili sasa wale ndugu zangu waislam hawataweza kutekeleza ile nguzo muhimu ya uislam yaani ibada ya hijja.

Watanzania hawataweza kwenda hijja mwaka huu ,tangazo limetolewa na shekhe mkuu wa Tanzania Mufti Abubakar Zuberi Ally leo hii.
 
Nyoosha maelezo yako vizuri mkuu, Ibada ya Hijja haikufutwa bali Mahujaji kutoka nje ya Saudia hawataruhusiwa kuja kuhiji , only wataruhusiwa baadhi ya waliomo ndani ya nchi ya Saudia kufanya ibada hiyo.
 
Recently waliweka kizuizi kwa waumini ambao hawaja pata chanjo, now how?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…