Mugabe aagiza polisi kuwakamata wanamichezo wote waliokuwa olympic

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,455
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemwagiza mkuu wa Polisi wan chi hiyo Augustine Chihuri kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda inchini Brazil kwenye mashindano ya Olympic mara tu watakapokanyaga kwenye ardhi ya uwanja wa ndege wa Harare.

Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31. Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata nafasi ya nane

Mugabe amemwambia mkuu huyo wa polisi kuwakamata wanamichezo hao: Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda kupoteza pesa zetu” alisema.

Kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera, tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe wakatuwakilishe.

Akaongeza kwamba, pesa iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha inchi ingeweza kutumiwa kununulia dawa na kujenga shule. Jambo hili ni sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake watano, maana yake nini? Nitahakikisha tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila kujali hata kama itachukua miaka 10, sasa pesa hizo zinabadilika na kuwa mkopo tuliowapa kwenda Brazil kama watalii, hawana faida” akamaliza.
 
Hahaha daah mzee wa matamko nae akiisoma hii nadhani atakurupuka na tamko
Lo! Bob kachoka. Wa kukamatwa ni wale maofisa ambao hawakuwaandaa vizuri wachezaji. Hao warudishe posho na nauli zao. Tatizo utakuta wote ni watu wake wa Karibu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Africa hakuishi vituko
 
Wakati mwingine Nyani Ngabu huwa anasema miafrika ndivyo tulivyo na huwa simwelewi ila sasa nimeanza kumwelewa.
 
Na yeye alifanya zimbabwe kuwa fukara wa kutupwa apewe adhabu gani??
 


Wakurupukaji...Birds of a feather fly together...Ndege wafananao huruka pamoja!
 
Ha ha ha ha ha,duh ukali huo angeutumia kwenye kubadilisha sera ya uchumi wa nchi mbona wangekuwa mbali sana kimaendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…