MUGALU: Persona Non Grata

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
Mchezaji huyu ameonyesha kiwango cha chini kabisa cha uchezaji ambacho hakilingani kabisa na hadhi ya Simba na hasa pale anapokosa magoli ya wazi mechi baada ya mechi.

Waliofanya scouting walifanya makosa makubwa kumleta Simba na badala yake amekuwa akituletea machungu makubwa na pale anapo poteza nafasi nyingi za wazi. Kwa mtazamo wangu mimi naona tija yake kwenye timu ni ndogo sana na nisingependa kumuona akiichezea Simba msimu ujao.

Imagine, Simba tungekuwa na Dube leo tungekuwa wapi? Simba wafanye mchakato wa kumpata Dube mchezaji mwenye viwango ambaye anastahili kuchezea Simba na sio Azam. Hapa Simba itabidi wavunje benki ili msimu ujao aje Msimbazi kuziba pengo la striker ambaye ni clinical and tactical ambaye Simba inamkosa sasa hivi.

Kwaheri Mugalu, we deserve someone better. Na cocha asipoangalia ataondoka nae kwani sisi wana Simba ameisha tu-boar kupita kiasi.
 
Mugalu ni mchezaji wa hovyo sana na sijui kwanini kocha anapenda kumtumia na hii ni bahati mbaya kwa club ya Simba kuwa na makocha wanaopenda kutumia washambuliaji wabovu mfano Omog na Luizio na kocha gani sijui na Maguli,ni trending hiyo.

Lakini pia umeshauri asajiliwe Prince Dube. Ndio ni mchezaji mzuri ila kwa maoni yangu anaweza asilete matokeo chanya kwenye haya mashindano ya kimataifa Anaweza kuwa mzuri kwenye michezo ya akina Ihefu,Gwambina n.k ila kwenye timu kubwa akashindwa.

Tutafute washambuliaji wazuri hata nje ya Africa hata 1 mwenye viwango vya kadiri kutoka hata Asia au ulaya mashariki.
 
Mugalu ni mchezaji wa hovyo sana na sijui kwanini kocha anapenda kumtumia na hii ni bahati mbaya kwa club ya Simba kuwa na makocha wanaopenda kutumia washambuliaji wabovu mfano Omog na Luizio na kocha gani sijui na Maguli,ni trending hiyo...
Siku zote wachezaji wazuri wapo tena wengi tu. Jw Tanzania tumefika kiwango cha kuwalipa 100M kwa mwezi?

Au hizo 100M ni mshahara wa akina Chama watano au sita?

Tuna kazi kubwa mbele yetu!
 
Dube atatufaa Simba.
Kwa sisi tuliowahi kucheza mpira wa ushindani tunajua.
Dube ana miaka 23 kwa sasa yaani ndo kwanza anachipuka.
Dube ana talent zote za mfungaji mahili.
Kwenye timu yake ya awali huko Zimbabwe Dube alifunga sana ktk mechi za Kimataifa hata Azam alifunga ndo maana wakamchukua ktk tim yao.
Dube ana
Kasi
Tageti
Shuti kali
Hadaa
Position vizuri
Stamina (msuli mkubwa)
Piga chenga mabeki.
NK

Dube anakilakitu kinachohitajika ktk mshambuliaji.

Humu nilisha mkosoa Mugalu siku nyingi nikashutumiwa sana kusema namchukia.
Wakamtetea kwamba ni Mkabaji mzuri.

Dube akija Simba ataendelea kukua kichezo na ki umri atakuja Kutisha baadae kidogo tu.

Mi nazungumza kama Mchezaji Mpira niliyecheza Beki na Winga kwamba Dube atatufaa Simba.

Pale Simba kwa sasa kama wanataka kusonga mbele wawaondoe.
Chikwende
Mugallu
Kagere na
Morrison ( ni mzuri ila ana mizaha sana, hayuko Siriaz ktk mechi muhimu

Wasajiri straiker wawili wanaweza kumchukua Dube na yule Beki wa AS Vita [emoji117]Djuma Shaabani ni mshambuliaji mzuri sana kuliko akikaa Beki.
Na wengine wawili.

Manara akizungumza na Rafiki yake Saidi Bakhresa atupe Dube, atatupa.
Nasema ni Manara pekee anayeweza kumshawishi Bahresa atupe Dube, wengine hawataweza.

Nazungumza kama mchezaji mpira wa zamani.

NB
Tungekuwa na Dube Kaizer Cheif tungewatoa kiulaini tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…