Muhammad Ali: Mbabe anayeteswa na ugonjwa wa kutetemeka

Muhammad Ali: Mbabe anayeteswa na ugonjwa wa kutetemeka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
attachment.php





Na Hashim Aziz


MWANZONI mwa mwezi huu wa Februari, 2013 habari zilizagaa mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa bondia wa uzito mkubwa (heavy weight) mwenye historia ya kipekee duniani, Muhammad Ali yu hoi bin taaban na kwamba atakufa muda wowote kutokana na kuzidiwa na maradhi yaliyomtesa kwa muda mrefu.

Kauli hiyo iliyotolewa na kaka wa bondia huyo mkongwe, Rahman Ali ilikanushwa vikali na mtoto wake, Leila Ali ambaye alisema baba yake hajazidiwa kiivyo ingawa ni kweli kwamba bado anasumbuliwa na ugonjwa wa Parkinson's Syndrome.



HISTORIA YAKE KWA KIFUPI


Muhammad Ali alizaliwa Januari 17, 1942 huko Louisville, Kentucky nchini Marekani na kupewa jina la Cassius Marcellus Clay ambalo baadaye alilibadilisha baada ya kuslimu mwaka 1964 na kuanza kutambulika rasmi kama Muhammad Ali ‘The Greatest'.
Katika maisha yake ya masumbwi, Ali alipigana jumla ya mapambano 61, akashinda mapambano 56, kati ya hayo 37 akishinda kwa Knock Out huku akipoteza mapambano matano tu, rekodi ambayo imemfanya kuwa miongoni mwa wanamichezo wanaoheshimika zaidi ulimwenguni, akijizolea tuzo kibao


UGONJWA WAKE ULIVYOANZA


Septemba, 1977 kipindi ambacho umaarufu wa Muhammad Ali ulikuwa umeanza kupungua, alipambana na bondia Earnie Shavers ambaye alimdungua ngumi nyingi za kichwa kiasi cha kufanya pambano lisimamishwe kwa muda. Hata hivyo, Ali alishinda pambano hilo kwa pointi lakini daktari wake wa siku nyingi, Freddie Pacheco akathibitisha kuwa amepata madhara makubwa kwenye fuvu la kichwa, akamshauri astaafu ndondi.
Ushauri huo haukupokelewa vizuri na Ali, matokeo yake akamjia juu daktari wake na kumfokea sana, siku chache baadaye akatangaza kumfukuza kazi.
Aliendelea kucheza masumbwi mpaka mwaka 1979 alipoanza kuonesha dalili zilizowashangaza wengi. Sauti yake na mikono vilianza kutetemeka wakati akizungumza, akapelekwa Mayo Clinic na kutibiwa, tatizo lake likapungua kwa muda, miezi michache baadaye akaendelea na kazi.
Hata hivyo, ufanisi wake jukwaani ulipungua sana, mwili wake ukadhoofika na akaanza kupoteza mapambano kadhaa.


ASTAAFU, AANZA KUUGUA


Mwaka uliofuatia, 1980 alipanda ulingoni kutwangana na Holmes. Katika pambano hilo lililowatoa machozi mashabiki wake wengi, Ali alidundwa kwa Knock Out na kuhitimisha ubabe wake. Kuanzia hapo afya yake ikazidi kuzorota na baadaye ikabainika kuwa amepatwa na ugonjwa wa Parkinson's Syndrome (ugonjwa wa kutetemeka) unaoendelea kumtesa hadi leo.

Baadaye alitangaza kustaafu kabisa ndondi. Mpaka sasa Ali akizungumza, sauti inakwaruza na kutetemeka, pia viungo mbalimbali vya mwili wake vinatetemeka.

Huyo ndiye Muhammad Ali, mbabe ambaye kwa sasa hali yake kiafya ni ‘tia maji tia maji'.
 

Attachments

  • MUHAMMADALI.jpg
    MUHAMMADALI.jpg
    55.5 KB · Views: 379
Back
Top Bottom