Muhiddin Kimario alijivua Uwaziri na kuungana na wanajeshi kwenda kupigana Vita ya Kagera

Author

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Posts
1,715
Reaction score
8,058
Moja kati ya mashujaa waliokwenda kupigana vita Uganda dhidi ya Idd Amin Dada alikuwa ni Meja Jenerali 'MUHIDDIN KIMARIO'(marehemu kwa sasa). Wakati Idd Amin anavamia eneo la Kagera na kuishusha bendera ya Tanzania na kuipandisha bendera ya Uganda, Muhiddin Kimario alikua waziri wa Mambo ya ndani na ni miongoni mwa mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano katika historia ya Tanzania.

Mwaka 1978 alitumwa na Mwl. Nyerere kwenda Mwanza kwenda kuwaaga Wanajeshi ambao walikuwa wanakwenda kupigana vita mkoani Kagera, kumng'oa Idd Amin Dada. Wakati Muhiddin akitoa hotuba yake ndani ya uwanja wa Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuungana na wanajeshi hao kwenda kupigana vita hivyo, wakati akichukua maamuzi hayo alisema kuwa.

"Mkuu Wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa Mh. Rais kuwa ninajivua uwaziri na ninaamua kurudi Jeshini na wenzangu leo, kwenda kumshikisha adabu Amini.".

Huyo ndio alikua Muhiddin Kimario ambae alivaa uzalendo wa Taifa hili.

Alikuwa tayari kuacha cheo chake kwaajili ya kupigania Taifa hili.

Ni kiongozi gani kwa sasa ambae anaweza kufanya alichofanya Meja Jenerali Muhiddin Kimario, kukubali kuacha wadhifa mkubwa wa uwaziri na kuingia Vitani, sehemu hatarishi?

C&P

IMG-20210401-WA0000.jpg
 
Elewa kiswahili vizuri: huyu "hakuukataa uwaziri", bali "alijivua uwaziri" na kurudi jeshini ili aende kuongoza vitani. Alikuwa mwanajeshi kwanza baadaye akawa waziri na wakati wa vita akajivua uwaziri huo ili aurudi jeshini.

Halafu sina uhakika kama kweli taarifa yako ni sahihi pia kwani nadhani Kimario alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati huo. Nyerere alikuwa ameweka wanajeshi kuwa wakuu wa mikoa ya mpakani na Uganda. Waziri wa mambo ya ndani wakati wa vita ile alikuwa alikuwa ni Salmini
 
Elewa kiswahili vizuri: huyu "hakuukataa uwaziri", bali "alijivua uwaziri" na kurudi jeshini ili aende kuongoza vitani. Alikuwa mwanajeshi kwanza baadaye akawa waziri na wakati wa vita akajivua uwaziri huo ili aurudi jeshini. Husemi alikutaa uwaziri, bali alijivua uwaziri.
Itifaki imezingatiwa Kichuguu, Shukran!
 
Moja kati ya mashujaa waliokwenda kupigana vita Uganda dhidi ya Idd Amin Dada alikuwa ni Meja Jenerali 'MUHIDDIN KIMARIO'(marehemu kwa sasa). Wakati Idd Amin anavamia eneo la Kagera na kuishusha bendera ya Tanzania na kuipandisha bendera ya Uganda, Muhiddin Kimario alikua waziri wa Mambo ya ndani na ni miongoni mwa mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano katika historia ya Tanzania.

Mwaka 1978 alitumwa na Mwl. Nyerere kwenda Mwanza kwenda kuwaaga Wanajeshi ambao walikuwa wanakwenda kupigana vita mkoani Kagera, kumng'oa Idd Amin Dada. Wakati Muhiddin akitoa hotuba yake ndani ya uwanja wa Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuungana na wanajeshi hao kwenda kupigana vita hivyo, wakati akichukua maamuzi hayo alisema kuwa.

"Mkuu Wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa Mh. Rais kuwa ninajivua uwaziri na ninaamua kurudi Jeshini na wenzangu leo, kwenda kumshikisha adabu Amini.".

Huyo ndio alikua Muhiddin Kimario ambae alivaa uzalendo wa Taifa hili.

Alikuwa tayari kuacha cheo chake kwaajili ya kupigania Taifa hili.

Ni kiongozi gani kwa sasa ambae anaweza kufanya alichofanya Meja Jenerali Muhiddin Kimario, kukubali kuacha wadhifa mkubwa wa uwaziri na kuingia Vitani, sehemu hatarishi?

View attachment 1740218
Mwamba huyo
 
Mimi nilikuwa namfahamu huyu kamanda binafsi.
Alikuwa mtu wa hekima sana.
 
Ni kiongozi gani kwa sasa ambae anaweza kufanya alichofanya Meja Jenerali Muhiddin Kimario, kukubali kuacha wadhifa mkubwa wa uwaziri na kuingia Vitani, sehemu hatarishi?
 
Elewa kiswahili vizuri: huyu "hakuukataa uwaziri", bali "alijivua uwaziri" na kurudi jeshini ili aende kuongoza vitani. Alikuwa mwanajeshi kwanza baadaye akawa waziri na wakati wa vita akajivua uwaziri huo ili aurudi jeshini.

Halafu sina uhakika kama kweli taarifa yako ni sahihi pia kwani nadhani Kimario alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza wakati huo. Nyerere alikuwa ameweka wanajeshi kuwa wakuu wa mikoa ya mpakani na Uganda. Waziri wa mambo ya ndani wakati wa vita ile alikuwa alikuwa ni Salmini
Jamaa alikusudia kutufunga kamba
 
Muhiddin Kimaryo pia alizuia utekwaji nyara wa ndege moja ya ATC Boeing.

Ilitokea kwamba alikuwemo ndani ya ndege hiyo kama abiria na vijana (sikumbuki wangapi) waliiteka nyara kwa kutumia bomu feki na kuamrisha wapelekwe nje ya nchi.

Baada ya Mzee Kimario kutambua kwamba wale vijana hawana utaalamu wo wote aliwaambia mapilot wajifanye kama wametii amri ya watekaji na wazunguke halafu watue KIA wakati taa zikiwa zimezimwa. Nadhani kulikuwa na mawasiliano ya ziada lakini ndege ilipotua tu vijana walijikuta wamezungukwa na wanajeshi na kubebwa juu juu.

Hata sikumbuki wale vijana waliishia wapi.

Nani anaikumbuka kadhia hii? Ilitokea baada ya akina Musa Memba kufanikisha utekaji nyara wa Boeing mwaka 1981/82? na kutokomea nayo Uingereza.

Vijana walikuwa very desperate kutaka kuondoka Tanzania kwenda kutafuta maisha nje.
 
  • MUHIDIN Kimario - Jenerali
  • IMRAN Kombe - Jenerali
 
Muhiddin Kimaryo pia alizuia utekwaji nyara wa ndege moja ya ATC Boeng.

Ilitokea kwamba alikuwemo ndani ya ndege hiyo kama abiria na vijana (sikumbuki wangapi) waliiteka nyara kwa kutumia bomu feki na kuamrisha wapelekwe nje ya nchi.

Baada ya Mzee Kimario kutambua kwamba wale vijana hawana utaalamu wo wote aliwaambia mapilot wajifanye kama wametii amri ya watekaji na wazunguke halafu watue KIA wakati taa zikiwa zimezimwa. Nadhani kulikuwa na mawasiliano ya ziada lakini ndege ilipotua tu vijana walijikuta wamezungukwa na wanajeshi na kubebwa juu juu.

Hata sikumbuki wale vijana waliishia wapi.

Nani anaikumbuka kadhia hii? Ilitokea baada ya akina Musa Memba kufanikisha utekaji nyara wa Boeing mwaka 1981/82? na kutokomea nayo Uingereza.

Vijana walikuwa very desperate kutaka kuondoka Tanzania kwenda kutafuta maisha nje.
Hadithi ya Boeing ya ATC kutekwa ikazunguka angani na kurudi Dar bila watekaji kutambua hivyo na wakashikwa ni kweli kabisa ilitokea na naikumbuka sana. Pilot aliwadanganya kuwa anatii maagaizo yao huku akiwa anarudisha ndege Dar; vijana wale walikuwa hata hawajui kiingereza kwa hiyo hawakuweza kuelewa kabisa mawasiliano baina ya kapteni na control tower. Ila kusema ilikuwa ni kwa sababu ya Kimario, hilo sina uhakina nalo wala silijui na wala haikuwa kutangazwa mpaka nalisoma leo. Nilikuwa mwanajeshi wa TPDF wakati huo kwa hiyo ningekuwa na hint kidogo kuhusu Kimaryo kuhusika katika tafrani ile hasa kwa vile alikuwa na General wa TPDF, lakini sikusikia lolote kumhusisha kwenye tafrani ile.
 
..tukio la ndege ya Air Tanzania kutekwa mwaka 1988 limeandikwa hapa.

..Major General Muhidin Kimario alikuwa mmoja wa abiria waliokuwepo ktk ndege hiyo.

NB:

..pia kuna Kaburu[ alikuwa mkufunzi wa ANC] aliteka ndege ya Zambia iliyokuwa na wapiganaji wa ANC. Ndege hiyo ililazimika kutua Dsm na Kaburu huyo akashtakiwa hapa Tanzania. Baadae alikuja kurudishwa kwao wakati Afrika Kusini ilipokaribia kupata uhuru.

cc @kichunguu, bitimkongwe
 
Uwaziri haukuwa na marupulupu makubwa Kama sasa, katu asingekubali, mchaga yule
 
Ila kusema ilikuwa ni kwa sababu ya Kimario, hilo sina uhakina nalo wala silijui na wala haikuwa kutangazwa mpaka nalisoma leo. Nilikuwa mwanajeshi wa TPDF wakati huo kwa hiyo ningekuwa na hint kidogo kuhusu Kimaryo kuhusika katika tafrani ile hasa kwa vile alikuwa na General wa TPDF, lakini sikusikia lolote kumhusisha kwenye tafrani ile.
Sisi wengine wala tulikuwa hatumjui huyo Kimario mpaka ilipotokea kadhia ile ndiyo tukalisikia jina lake. Hata hayo mambo ya jeshini (kwa kwetu Zanzibar) enzi zile tulikuwa hatuna kwa hivyo tulikuwa hatumjui kabisa.
 
Yani Mimi source ya habari akiwa ni Yericko basi habari yote nakuwa na mashaka nayo.
 
Back
Top Bottom