elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Chimbuko lake ziara ya ghaa JPM, Yasuka upya wataalamu ughaibuni, Mapato yapaa bn 2.6/- hadi bilioni 5 .
MNAMO Novemba 9 ya mwaka 2015, akiwa mgeni madarakani, kwa mara ya kwanza Rais Dk. John Magufuli, alifanya ziara ya kushitukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kusikiliza kero za wagonjwa. Baada ya hapo, alitoa maelekezo na fedha za kumaliza matatizo, zikiwamo za uhaba wa vitanda, magodoro, wodi za wagonjwa, vifaa tiba na dawa.
Kuanzia hapo hadi sasa, Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Lawrence Museru, anasema ameshatumia Sh. bilioni 37.4 kununua vifaa tiba na mashine za uboreshaji miundombinu na kujenga uwezo wa wataalamu katika miaka hiyo minne. Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari, Prof. Lawrence Museru, anasema maboresho makubwa MNH imefanikiwa kuongeza mapato kutoka Sh bilioni 2.6 kila hadi Sh bilioni 6 kila hadi Sh. bilioni tano wa mwezi. “Katika kipindi cha siku 1,460 tangu Rais Magufuli atembelee Muhimbili na kutoa maagizo kadhaa. Tumeshatumia zaidi ya Sh. bilioni 37.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” anasema Prof. Museru.
MAELEKEZO YA JPM
Mkurugenzi huyo anasema, waliagizwa kushughulikia shida ya ukosefu wa dawa, wagonjwa waliokuwa wakilala chini wapatiwa vitanda na kulipa stahiki za wafanyakazi, zikiwamo posho na nauli za likizo.
Prof. Museru anasema, pia waliagizwa kutoa huduma za ubobezi kupunguza rufaa za nje ya nchi, kuboresha mazingira ya kazi, kununua na kukarabati vitendea kazi. Anasema, baada ya maboresho walifanikiwa kuokoa Sh. bilioni 32 ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa kutibiwa nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Prof. Museru, huduma zilizoanza kutolewa MNH na kiasi kilichokookolewa kwenye mabano ni, upandikizaji wa figo (Sh. bilioni 4.5), upandikizaji vifaa vya kusaidia kusikia (Sh. bilioni 2), huduma ya mfumo wa chakula na ini (Sh. bilioni 1.3) na huduma ya radiolojia (Sh.bilioni 24).
Prof. Museru anasema, pia wametoa dawa bure kwa wananchi zinazogharimu Sh. bilioni 72 katika miaka minne ya uongozi wa Rais Magufuli, ikiwa ni sawa na Sh. bilioni 1.5 kwa mwezi. “Tofauti na miaka ya nyuma, tulikuwa tukitumia Sh. milioni 400 hadi 700 kila mwezi kwa ajili ya dawa za wagonjwa wasiyoweza kumudu gharama za matibabu,” anasema Prof. Museru.
Mtendaji huyo mkuu wa MNH, anafafanua kwamba kila , mwezi wanatumia Sh. milioni 600 kutibu wagonjwa wasiyo na fedha za matibabu. Prof. Museru anataja kingine, walifanya matengenezo ya mashine ya MRI (Magnetic Resonance Imaging) ambacho si cha upasuaji kinachotumika kuchunguza magonjwa mwilini, kupitia mawimbi ya sumaku, redio na kompyuta, kutengeneza picha inayoonyesha sehemu husika inayochunguzwa.
Anasema matengenezo ya mashine ya kuchughuza mwili ya CT-Scan, nayo yalifanyika na inaendelea kufanya kazi vizuri tangu Desemba mwaka 2015.
Kuhusu ukosefu wa dawa, anasema wameboresha na hadi sasa wagonjwa wanapata dawa kwa zaidi ya asilimia 96 kutoka kwenye maduka ya hospitalini, kulinganisha na wastani wa 40 kabla ya uboreshaji hpo. “Hospitali ilianzisha mfuko maalumu kwa ajili ya dawa ambapo fedha zote zinazopatikana kutokana na mauzo ya dawa hutumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa,” anasema Prof. Museru. Anaeleza kuwa, kwa sasa Sh. bilioni 1.5 zinatumika kununua dawa kila mwezi sawa na Sh. bilioni 18 kwa mwaka na katika miaka minne, hospitali imenunua na kuwapa wagonjwa dawa zenye thamani ya Sh.bilioni 72.
MATATIZO?
Kuhusu changamoto ya wagonjwa kulala chini, Prof. Museru, anasema walitekeleza kuhamisha wagonjwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) kutoka wodi mbili walizokuwamo na chumba cha wagonjwa wa uangalizi maaluma (ICU), yenye vitanda 15.
Eneo lingine walilofanyia marekebisho ni matatizo ya watumishi, kwamba katika kipindi cha miaka minne, MNH imelipa malimbikizo ya madai ya wafanyakazi, ikiwamo muda wa ziada, wauguzi usiku na posho za watendaji wa tiba “Hali hii ilishusha morali kwa kiwango kikubwa sana na hivyo wafanyakazi kupunguza kasi ya ufanyaji kazi kwa kujituma na matokeo yake ni kukosekana tija katika utoaji huduma. Kwa sasa, wafanyakazi wengi wa MNH wana ari,” anasema Prof. Museru.
KWENYE MABORESHO
Kuhusu upunguzaji rufani za nje ya nchi, anasema kwa nyakati tofauti MNH imepeleka wataalamu wake nje ya nchi, kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu.
Anataja kada ya wataalamu waliopata ujuzi na elimu ya kutoa huduma hizi kwa ufanisi, ni katika fani anazozitaja kuwa; madaktari bingwa, wauguzi, maabara, radiolojia, magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, saratani za damu Prof. Museru anasema, ni mafunzo yaliyogharimu Sh. bilioni 3.597 na kwamba yamewasaidia Watanzania wengi kuhudumiwa nchini, badala ya kupelekwa nje, vivyo hivyo kiasi kikubwa cha fedha za serikali.
Anataja eneo lingine lililoboreshwa ni kuanzishwa huduma za upandikizaji vifaa vya kusaidia watoto kusikia na kunufaisha wagonjwa 34 na wawili walijigharamia. Jumla serikali ilitumia Sh. bilioni 1.15, sawa na Sh. milioni 36 kwa kila mgonjwa, tangu Juni mwaka 2017 na kufanikiwa kuokoa Sh. bilioni 2.05 kama wangetibiwa nje ya nchi.
Profesa Mseru anasema, Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo kupitia hospitali za umma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Prof. Museru anasema katika mwaka huo 2017, Tanzania iliandika historia ya pili kupitia MNH kufanya upandikizaji figo kwa mara ya kwanza na hadi sasa, kuna wagonjwa 51 kwa gharama Sh. milioni 30 kila mmoja, sawa na Sh. bilioni 1.530.
Anaeleza, mbadala wake kama tiba hizo zingelenga kufanyika nje ya nchi, serikali ingetumia Sh. bilioni 6.120 sawa na Sh. milioni 120 kwa kila mgonjwa. Hivyo, imeokoa fedha Sh. 4.590. “Kabla ya huduma hii kuanza nchini, serikali ilisafirisha wagonjwa 150 nje ya nchi katika kipindi cha miaka 15, wastani wa wagonjwa 10 kwa mwaka,” anasema Prof. Museru na kuongeza: “Kwa miaka miwili, Muhimbili imefikia asilimia 34 ya wagonjwa waliopelekwa nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 15,” anasema
RADIOLOJIA NCHINI
Anataja Novemba mwaka 2017, MNH ilianzinzisha kwa mara ya kwanza huduma za tiba radiolojia ikishirikiana na watalaam kutoka Kenya na Chuo Kikuu cha Yale, Marekani na kuna wagonjwa 558 waliopatiwa huduma kati yao 274 walikua na uvimbe wa kinywa 96 kwa mgonjwa mmoja kwa safari nne zinazohitajika.
Serikali imeokoa Sh. bilioni 24.112 kutoa huduma hizi nchini,” anasema Prof. Museru. Anasema, MNH ilianzisha na kuboresha huduma za uchunguzi kwa wenye matatizo ya mfumo wa chakula na ini. Wagonjwa 380 walihudumiwa kwa Sh. milioni 116.8 na hospitali imefanikiwa kuokoa Sh. bilioni 1.397.
SARATANI
Pia, Prof. Museru anasema wametoa huduma ya saratani iliyoanza kutolewa, ikiwamo uchunguzi wa ugonjwa huo na matibabu ya awali kwa wagonjwa. Anasema hospitali inakamilisha mipango ya uanzishwaji wa huduma ya upandikizaji uloto (bone marrow transplant) muda wowote kuanzia sasa.
Ilidharimiwa kati ya mwezi huu na mapema mwakani. Kwa mujibu wa Profesa Museru, hospitali husika imeshatumia Sh. milioni 117 kwa ajili ya mafunzo hayo na fedha hizo zimetokana na vyanzo vya ndani vya hospitali.
Kingine anachokitaja mkurugenzi ni kuendelea kuboresha mazingira ya kazi katika kipindi cha miaka minne, ikighalimu jumla ya Sh. bilioni 10, ikijumuisha vyumba vya upasuaji, ili kuendana na kasi ya ongezeko la wagonjwa na uanzishwaji wa huduma mpya hospitalini. Prof. Museru anasema wamefanikiwa kukarabati na kuongeza vyumba vya upasuaji kutoka 13 hadi 20.
Anafafanua: “Hospitali imepunguza msongamano wa wagonjwa kusubiri tarehe ya mbali ili kufanyiwa upasuaji. Jumla ya Sh. bilioni 2.46 zilitumika kiufanya kazi hiyo.” Anasema, pia hospitali iliweza kukarabati na kuongeza vyumba vya wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu, yaani ICU kutoka vitanda 25 hadi 78 na vimejengwa na kuwekewa vifaa tiba