Muhimbili kuanzisha maabara ya kwanza nchini ya Upasuaji wa Sikio

Muhimbili kuanzisha maabara ya kwanza nchini ya Upasuaji wa Sikio

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Hospitali ya Taifa Muhimbili imesaini mkataba na Kampuni ya Medel kutoka nchini Austria wenye lengo la kuanzisha maabara ya kwanza ya aina yake Afrika Mashariki ili kufundisha na kuboresha upasuaji wa sikio kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi.

Akisaini mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameshukuru kwa ushirikiano huo ambao unalenga kukuza taalamu sambamba na kwenda na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia.

"Tunashukuru Kampuni ya Medel kwa kushirikiana na Muhimbili kwa kuanzisha maabara hi ambayo itaenda kusaidia wataalamu wetu wa ndani na wa nchi jirani kuja kupata elimu kwetu a pia kupata madaktari bingwa wengi", amesema Prof. Museru.

Kwa upande wake, Bw. Fayaz Jaffer ambaye ni Mtaalamu wa kupima masikio, amesema maabara hiyo ya kisasa itasadia kutoa mafunzo kwa wataalamu, pia itapunguza madaktari bingwa kwenda kupata mafunzo haya nje ya nchi kama ilivyo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom