Muhimbili na Mloganzila kufikisha Wagonjwa 81 waliopandikizwa Figo nchini

Muhimbili na Mloganzila kufikisha Wagonjwa 81 waliopandikizwa Figo nchini

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inatarajia kufanya upandikizaji figo kwa wagonjwa sita ifikapo Julai.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Juni 30, 2023 na Mkuu wa Kitengo cha Figo Muhimbili, Dk Jonathan Mngumi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo.

Hadi sasa, wameshapandikiza figo watu 75, kwa mujibu wa Mngumi ambaye ni daktari bingwa magonjwa ya figo.

“Tumejadili na Mkurugenzi Mtendaji, tunatarajia Julai tutafanya tena huo upandikizaji na tuna wagonjwa sita ambao wapo kwenye kusubiria huduma hiyo,” amesema.

Aidha Dk Mngumi amesema idadi ya watu wenye uhitaji wa huduma kuchuja ya kusafisha damu kwa njia ya mashine imeongezeka ambapo amesema, dunia wagonjwa ni milioni 800, sawa na asilimia 10 ya idadi wa wote wana magonjwa ya figo.

Kwa Tanzania, asilimia saba wanatambulika kuwa na magonjwa sugu ya figo na wanaongezeka kwani katika kliniki yao ya wagonjwa wa figo kwa wiki hupokea watu 90 kwa ajili ya kucheki figo zao na watano kati yao hutakiwa kuanzishiwa huduma maalum ya kuchuja damu kwa kutumia mashine kitaalamu ikijulikana ‘Dialysis.’

“Huduma hizi kwa mtu mmoja hufanya saa nne kwa siku na anatakiwa kufanya mara tatu au mbili kwa wiki. Ni huduma ambayo gharama ya fedha kwa wagonjwa na muda, inabebesha mzigo mkubwa kwa taasisi na Serikali kwa ujumla,” amesema Dk Mngumi.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohammed Janabi amesema kwa siku hospitali hiyo huchuja damu wagonjwa 130 hadi 150.

Muhimbili (Upanga) inahudumia kati ya wagonjwa 110 hadi 120 kutegemea na siku na idadi ikijumlishwa na waliopo wodini na Muhimbili (Mloganzila), husafisha wagonjwa 30 hadi 50.

Profesa Janabi ametoa rai kwa watu kutunza afya zao kwani huduma ya kuchuja figo ni gharama na vifaa na dawa zinazotumika, zinatoka nje ya nchi na asilimia 30 hadi 40 ya wagonjwa wanaohitaji hawana uwezo wa kumudu.

Hata hivyo amesema zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa hao ambao huchuja damu ambayo amesema siyo siyo tiba ya mwisho, kwani wengi wao wanasubiria kupandikizwa figo kama tiba kamili.

“Kuna wale wenye bima ya afya na wengine wachache wanaotoa fedha zao mfukoni hata wao hawana uhakika watatoa kwa muda gani,” amesema.

Pia amesema katika wagonjwa 100, kati yao 90 wana shinikizo la juu la damu, na hivyo ametoa rai kwa Watanzania kujikinga ikiwamo kupunguza matumizi ya chumvi mezani.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom