Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS) SPECIAL THREAD

Chuo kiboreshewe miundombinu ya kujisomea na hostel kwa maana kama ujawai kufika MUHAS unaweza kudhani ni bonge la chuo lakini kumbe ni kachuo kadogo sana, tunaomba wajenge majengo mazuri ya kujisomea na waboreshe hosteli maana zimechoka sana.

College of medicine itahamia Mloganzila,but future plan kozi zote za undergraduate zitahamia huko,hapo upanga zitabaki kozi za postgraduate.

Ujenzi wa majengo unaendelea huko Mloganzila pia mradi wa HEET unakusudia kuanzisha campus kubwa huko Kigoma.
 
Kujenga majengo mengine pale sidhani eneo dogo, labda kuboresha tuu, alaf nasikia kuna campus nyingine inajengwa kigoma baada ya kupokonywa ile ya mloganzira[emoji28] Google chrome

Ni kweli pale kwa sasa huwezi fanya ujenzi pamesha bana eneo ni dogo,labda wavunje majengo ya zamani kitu ambacho ni kigumu hata waseme wajenge pale ebola de camp haiwezekani.
 
Aisee alaf kwann kigoma, kuna mikoa mingi tuu imechangamka kuliko kigoma, kwann walichagua kigoma, kama kuna mtu ana majibu naomba anijibu?
 
Alaf hio ya kigoma ikikamilika undergraduate yote inahamia kigoma na postgraduate inabaki pale upanga au wataongeza tuu admission capacity?
 
Aisee alaf kwann kigoma, kuna mikoa mingi tuu imechangamka kuliko kigoma, kwann walichagua kigoma, kama kuna mtu ana majibu naomba anijibu?

Wamechua huko kwa malengo mengi ikiwepo kucatch wagonjwa wa nchi jirani za burundi,rwanda na congo na mikoa ya pembezoni ndio mana wana mpango wa kujenga hospitali kubwa sana huko ya kitaifa ili kupunguza influx ya wagonjwa muhas.

Pia ukanda huo ndio unaongoza kwa magonjwa mengi ya mlipuko kama ebola,marburg etc,hivyo kujenga pia kituo cha utafit na udhibiti wa magonjwa ya aina hiyo.

Sambamba na hayo ni kupunguza influx ya wanafunzi kuja dsm main campus na kuweza kucatch wanafunzi wa mikoa ya pembezoni na nchi jirani.
 
Good plans
 
Kujenga majengo mengine pale sidhani eneo dogo, labda kuboresha tuu, alaf nasikia kuna campus nyingine inajengwa kigoma baada ya kupokonywa ile ya mloganzira[emoji28] Google chrome
Nimesikia hilo pia kwamba wana plan ya kujenga new campus Kigoma.

MUHAS pale Mloganzila nadhani walishindwa kuiendesha ile ndio maana wakapewa MNH waiendeshe, ishu kubwa itakua hawakua na uzoefu wa kuendesha hospital, labda itakuja kurudishwa kwa MUHAS miaka ya badae.

Ila mloganzila palijengwa vizuri sana.
 
Of course ni jengo nzuri.
Pale mloganzira bhana walikuwa wanafanya uhuni, walimu hawawez kutibu, kufundisha na kutibu ni vitu viwili tofauti, wagonjwa walikuwa wanakufa sana pakaanza kupata sifa mbaya alaf kulikuwa hamna hata uongozi mzuri, mambo yalikuwa hovyohovyo, Magufuli akawapokonya akawapa MNH.
Mfano radiology Mashine zote pale CT, MRI, XRAY, ultrasound zote used ila walionunua wanakwambia tulinunua mpya na walitumia hela nyingi sana.
Chuo kilipiga sana hela pale mloganzira aisee.
 
Haya wana muhasso

Please update your info, kuna madadiliko makubwa kwenye uongozi mfano Nahya sio head wa Pediatric ila ni director wa Research, Said Abood ni DG wa NIMR
 
Please update your info, kuna madadiliko makubwa kwenye uongozi mfano Nahya sio head wa Pediatric ila ni director wa Research, Said Abood ni DG wa NIMR
Thanks, kama nilivosema hapo awali hizi information nimezitoa kweny website ya MUHAS naona bado hawaja update, kama kutakuwa kuna update zozote naombeni mniletee ili niweke mambo sawa.
 
Chuo kidogo sana plus watu ni wengi, wanafunzi, staff wa chuo, staff wa hospitali, wagonjwa, ndugu za wagonjwa lazima usafi utakuwa mgumu kidogo kwa sababu ya wingi wa watu.
Mbona pale Kairuki ni pasafi na panavutia ilihali na wao wanaidadi kubwa kubwa ya wagonjwa na wanafunzi pia
 
Nina swal moja..nmemaliza diploma kutoka chuo cha nactvet je gpa ya kuweza kujiunga muhas kwa ajili ya bach ya pharmacy n ipi kwa sasa na kama unajua jinsi ya ku calculate overall gpa naomba unisaidie
GPA 4.5
 
Hapana aisee sijui.
 
Overall GPA inapatikana kwenye transcript
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…