Habari za uhakika ni kwamba dr masau hakualikwa.aliyeongoza upasuaji wa moyo ni dr.Mahalu.huyu ni mmoja ya madactari wazawa ambae hapo awali alikuwa akifanya upasuaji wa moyo nchini Zimbabwe,na alikuwa akiheshimika saana nchini humo.
Swala la kuwa operation za moyo zilikuwa zikifanyika,nusu ni kweli na nusu si kweli.Hapo awali kilichokuwa kikifanyika ni upasuaji mdogo wa moyo kama kuondoa ganda la juu la moyo yaani pericardioctomy hapa moyo hauguswi ndani,na alikuwa akizifanya Prof L,Lema wa muhimbili, na labda kufunga vitundu vidogo ambavyo watoto wengine huzaliwa navyo yaani pantent ductus arteriosus.
Tofauti na KCMC ambayo hutegemea wataalam kutoka marekan,sasa kinachofanyika Muhimbili ni OPEN HEART SURGERY ambayo ni operation kubwa ya moyo,moyo unafunguliwa ndani kurekebisha shida husika,na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi imefanywa na madaktari,na manesi wazawa ambao wamesomeshwa na hela ya watanganyika.Hili ni jambo la kujivunia ambalo nilitegemea lingepata postive publicity kama iliyotolewa kwa Ile ya SAGA ya MOI yaani Emmanuel Mgay et al.
Kwamba ni majaribio,si kweli watu hawa wametrain vyema,kuna wazoefu wawili kama nilivyokwisha eleza,Dr Mahalu na Dr.Wandwi huyu ni mzawa,katrein na kufanya kazi Israel kwa mda wa takriban miaka mitano au saba kama sikosei.Kwa pamoja naamini watasaidiana na hawa vijana walotrain India.
Kwamba Dr.Masau anabaniwa na Serikali,sidhani kama ni kweli nafikiri pia yeye hana ushirikiano na wenzake.Nilipata bkuambiwa na nikashuhudia mwenyewe-yeye anatibu kama kadiologist,halafu kama kadiac surgeon na pia kama kadothoracic surgeon.Kwa mazingira ya kawaida na hata ya nchi zilizoendela hamna mtu anaeweza kufanya kazi hivyo na nafikiri ya Dr.Masau inastahili kuitwa MADE IN TANZANIA
Rai yangu,tuwaunge mkono na tuisihi serikari iwape msaada sitahili.Pia imsaidie Masau afikie lengo lake kwa wote wakiweza anaefaidika ni mtanzania
Nawasilisha