Muhimu katika Rasimu ya katiba mpya

Muhimu katika Rasimu ya katiba mpya

Imma Saro

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
394
Reaction score
197
Posho ni upotoshaji wa Malengo Muhimu katika Rasimu.
Mosi Muhimu katika Rasimuniwapongeze wale waote waliobahatika kuteuliwa kuwa wajumbe wa bunge la katiba na mungu awaongoze katika kila jambo,Pia niwape moyo wale wote waliokosa nafasi ya kuingia ndani ya bunge la katiba,Kupanga ni kuchaguwa basi waliochaguliwa tuwatie moyo tuwape ushirikiano wakutosha katika kila jambo na kuwakosoa pale inapo bidi kuwapongeza pia ni muhimu pale wanapo fanya jambo jema.

Ramisu yetu ina mambo mengi muhimu sana katika kuleta tija katika ustawi wa taifa letu.

Kunahitajika umakini wa hali ya juu katika kuijali rasimu hii Kila mmoja wetu anafahamu hii ni kazi iliyofanywa na binadamu hivyo makosa madogomago hayawezi kukosekana,kunamaboresho yanayoitajika katika rasimu ,Maswala ya Resilimali,Aridhi,Muungano,Mambo ya nje na nakadhalika yanahitaji umakini katika kuyajadili.

Posho;
Posho(pesa) hili neno ni jema na ni neno baya katika kufikia malengo ya taifa,Inaonekana mbaya tu pale inaotumika kinyume na kuonekana ya maana sana pele kwenye kuleta mema.

Kwa muda sasa pese imetuhamisha kutoka kwenye rasimu na kuanza kuijadili kitu ambacho kwangu binafsi naona kama inatuhamisha kwenye kujadili na kuiboresha rasimu yetu.

Kila mmoja wetu anafahumu posho ni kubwa na inawatosha lakini ili kuweza kuwagawa na kuweze kuwatawala basi azisha ajenda ya posho wengi watahama na kuijadili,ndicho kilicho fanyika hivi sasa,kutawaliwa na posho na sio rasimu muhimu katika taifa letu.

Tunaandika katiba inayotokana na wanachi basi hakuna sababu ya kuendelea kuijadili hii posho kila siku, tujikite kwenye maswala yaliyoko katika rasimu yetu.

Taifa letu kwa muda limeyafaidisha mataifa makubwa kama ni kuliwa limeliwa sana na kwa muda mrefu sana na hii yote ni katiba mbovu ndio chanzo kikubwa.

Wakijilipa milioni moja tutapiga kelele lakini watapokea tu,Tutaweza kupiga kila kona na Mh Raisi akamua kufutilia mbali bunge la katiba tukabaki kama mwanzo,tukapata hasara kubwa sana tume ya kukusanya maoni imetumia fedha nyingi ambazo ni kodi zetu,ukumbi wa bunge umeboreshwa kwa mamilioni ya shilingi.

Swali jepesi nani anae fahamu yale mabilioni ya nje yako wapi,fedha za rada,Nani anafahamu tume ya Jaji Warioba walikuwa wanalipwa kiasi gani kwa siku kuna tetesi kwa siku ilikuwa kwenye 420,000 kwa siku huku gari mafuta ya serekali.

Tume ya Richmond kwa siku nani aliekuwa anajuwa kiasi walicho kuwa wakilipwa?Tume ya kuchunguza bombu lilorushwa kwenye mkutano wa chadema,kanisani wanalipwa kiasi gani? nani alie wahi kuhoji haya yote.

Niweke wazi msimamo wangu siungi mkono ongezeko wala sioni kwani waongezewe,pili sioni sababu kubwa ya kujikita kujadili posho wakati mambo muhimu tume ya Mzee wangu Warioba imeniwekea kwenye rasimu ndio nao yajadili.

Tusikubali kuijadili posho kupoteza malengo yetu kama watanzania,Tujikite kwenye rasimu yetu
1621905_609493709134627_904688194_n.jpg
 
Back
Top Bottom