Fohadi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2020
- 772
- 2,421
Utangulizi
Kumekuwepo na utokeaji wa maafa mbalimbali kama vile moto, ajali n.k ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakisababisha athari ambazo zinaathiri ustawi wa mtu mmoja mmoja na ustawi wa jamii kwa ujumla. Baadhi ya athari ambazo zimekuwa zikijitokeza ni pamoja na upotevu mkubwa wa nguvu kazi, uharibifu wa miundombinu pamoja na mali za raia hali inayopelekea kufilisika na kurudi katika hali duni ya kimaisha baada ya athari hizo kutokea.
Serikali kupitia viongozi wake imekuwa ikiunda tume mbalimbali za kuchunguza vyanzo na athari za haya maafa mara tu yanapotokea. Matokeo ya tume hizi yamekuwa yakitumika katika kufanya mabadiliko katika uendeshaji wa eneo fulani au mifumo ya ufanyaji kazi ili kuzuia utokeaji tena wa maafa ya aina ile ile. Kwa lugha nyingine tume hizi huundwa ili kuipatia serikali taarifa kuhusu tukio na hivyo ni sawa na kusema serikali hujifunza kutokana na makosa.
Kujifunza kutokana na makosa ni kitu kizuri sana hasa katika mambo mengine kama ujasiriamali, usanii na michezo lakini sio kitu kizuri kabisa katika upande huu wa maafa kwani tunajifunza baada ya kuwa tayari tumepoteza rasilimali nyingi na tumepata madhara makubwa ambayo yatachukua miaka mingi kurekebishika na pengine yasirekebishike kabisa mfano upotevu wa rasilimali watu (Nguvu kazi).
Nini Kifanyike?
Ni muda sahihi sasa wa serikali kuanzisha tume maalum ambazo kazi zake zitakuwa ni kufanya tathimini ya maeneo mbalimbali na hivyo kubaini zile hatari zilizopo katika maeneo hayo na hivyo kuja na mapendekezo ya nini kifanyike ili kuzuia au kupunguza madhara ya hatari ile iliyobainika kabla haijatokea. Tume hizi zitatusaidia kujifunza kabla ya makosa na hivyo kujiandaa kikamilifu na kuweka mifumo ikiwemo kuchukua tahadhari zote muhimu ili kujiweka sawa na chochote kitakachotokea siku za mbeleni. Hii ni sawa na jinsi ambavyo wajasiriamali na wawekezaji hufanya upembuzi yakinifu wa biashara zao ili kugundua hatari zilizopo au zenye uwezekano wa kutokea hapo baadae wakati wakiendelea na biashara zao. Upembuzi yakinifu huu hufanyika kabla ya hatari hizi kutokea na hivyo huwasaidia kujiandaa kukabiliana nazo.
Baadhi ya maeneo hatarishi yanayohitaji tahadhari kubwa na za haraka kwa sasa
Kama nilivyogusia hapo awali, serikali imekuwa na kawaida ya kuunda tume baada ya madhara kutokea. Ila ukiangalia, hatua tunazozichukua baada ya maafa kutokea tuna uwezo wa kuzichukua hata kabla ya maafa na ndiyo maana ni wakati sahihi sasa kuunda tume za kuzuia maafa badala ya kusubiri maafa yatokee ndipo tuunde tume. Baadhi ya maeneo hatarishi ambayo kwa namna moja ama nyingine yamesahaulika ni pamoja na:-
Hitimisho
Kuna maeneo mengi sana ambayo ni hatarishi hata kwa macho lakini hakuna tahadhari madhubuti zilizowekwa ili kukabiliana nazo. Ni vema sasa serikali ikaunda tume maalumu ambayo kazi yake itakuwa kuchunguza na kufanya upembuzi yakinifu kwenye maeneo yote hatarishi ambayo yanaonekana kwa macho na yanayoonekana kwa macho ya kitaalamu ambayo yanaweza kuzuilika. Na kupitia wataalamu ndani ya hizo tume, tahadhari muhimu za kuchukua zitapendekezwa na serikali itazifanyia kazi.
Serikali inatakiwa kuandaa fungu la kutosha kama bajeti ya kutimiza matakwa na mapendekezo yatakayokuwa yametolewa na hizi tume. Uundaji wa tume za uchunguzi baada ya maafa imekuwa ni kama tabia inayorithiwa kutoka kwa uongozi hadi uongozi. Hivyo sasa tunapaswa kuunda tume kutathimini kiwango cha maafa kwa matukio yote ambayo yapo nje ya uwezo wa kibinadamu kama kimbunga lakini sio vyema kuendelea kuunda kamati kutathimini athari kwa maafa ambayo yanazuilika na yanaonekana kwa macho hata kabla hayajatokea.

- Kona kali za barabara. Kwa mfano, wale watumiaji wa barabara ya Dar – Iringa watakubaliana na mimi kuwa mlima kitonga una baadhi ya kona ambazo ni hatarishi sana na hakuna tahadhari iliyochukuliwa. Kuna baadhi ya kona ambazo kama gari itafeli breki au usukani moja kwa moja tutaanza kuokota vyuma chakavu vya magari kutoka korongoni na kupoteza nguvu kazi kubwa. Ni wakati sahihi sasa kutengenezwa kingo imara katika kona hizi ili kuzuia hatari hii inayoonekana wazi. Hatupaswi kusubiri tume ya kuchunguza chanzo cha maafa kwa kitu kilichowazi kama hiki.
- Maeneo ya viwanja vya mipira. Haya ni maeneo yanayokusanya watu wengi kwa wakati mmoja. Zaidi ya watu 10000 hukusanyika kutazama mechi. Hii ni hatari zaidi endapo mtu mmoja ataamua kujitoa muhanga. Japokuwa hatuna rekodi ya matukio kama haya ni vyema sasa mifumo maalumu na usimamizi madhubuti ili kuhakikisha hakuna silaha au kifaa hatarishi kinaingia ndani ya uwanja. Kwasasa naona usimamizi katika hili upo chini sana. Hatupaswi kusubiri maafa ili tuchukue hatua.
- Kituo cha uzalishaji umeme pale Ubungo. Kwa jinsi mitambo ilivyokaa pale, lile ni eneo hatarishi sana endapo kuna hitilafu kubwa itatokea. Na bahati mbaya wananchi wamekuwa wakiendelea na shughuli zao na wengine kusinzia kabisa bila kujua hatari iliyopo. Ni wakati sasa hatua zichukuliwe. Tusisubiri kuja kuunda tume ya kutathimini kiwango cha athari wakati tayari tutakuwa tumepoteza rasilimali watu.
- Vyombo vya usafiri wa majini. Kwa hapa nitatoa mfano wa hizi pantoni za kuvusha watu kutoka upande mmoja hadi mwingine. Hizi zinachukua idadi kubwa ya watu. Lakini ukiangalia idadi ya watu na idadi ya maboya au vifaa vingine vya uokozi ni tofauti. Idadi ya watu ni kubwa sana. Na mbaya zaidi, hata ukiangalia Kamba zilizo kwenye maboya zinaonekana zimekaa muda mrefu na zimepigwa jua kiasi kwamba zinaweza kuwa rahisi kukatika kama kuna nguvu kubwa itatumika. Kingine, hakuna elimu yoyote inayotolewa kabla ya kuanza safari jinsi mtu anaweza kutumia vifaa vile. Hii ni hatari inayoonekana wazi ambayo haitakiwi kusubiri madhara yatokee ili tuanze kuchukua hatua za kuunda tumen a kuwajibishana. Wakati ni sasa.

Upvote
0