Muhimu: Usinunue Simu Used / Refubrished bila kusoma uzi huu

Mr_mkisi

Member
Joined
Sep 24, 2024
Posts
15
Reaction score
47
Watu wengi wanapenda simu za kisasa zenye uwezo mkubwa kwa bei ya kawaida. Hali hii inapelekea wengi wao kuamua kununua simu zilizotumika (used) kutoka nje ya nchi, katika masoko maarufu kama Kariakoo au Makumbusho, na maeneo mengine.

Hivi karibuni, kupitia jukwaa hili, kumeibuka mjadala mkubwa kuhusu changamoto wanazokumbana nazo wateja wanaponunua simu hizi. Wengi wao wanalalamika kuwa licha ya kupewa warranty, simu zao zinapoharibika hawapati msaada wowote kutoka kwa wauzaji.

Kabla ya kuendelea zaidi, ni muhimu kujua utofauti kati ya simu used na refurbished.

Utofauti kati ya Simu Used na Refurbished

  1. Simu Used
    Hii ni simu ambayo imetumika kwa muda fulani na baadaye kuingizwa sokoni kwa ajili ya kuuuzwa tena.
  2. Simu Refurbished
    Hii ni simu ambayo ilianza kama mpya, ikatumika kwa muda, lakini mtumiaji aliirudisha kiwandani au katika maduka maalum yanayotambulika na kampuni husika. Sababu za kurudisha zinaweza kuwa matatizo madogo au bila matatizo kabisa. Mara nyingine mteja anaweza kuirudisha kwa sababu ya kutumia warranty au kutaka kuboresha (upgrade).
Simu hizo hutengenezwa upya na kurudishwa sokoni zikiwa katika hali bora, mara nyingi zikiwa zimefungwa kwenye boksi na sealed. Hata hivyo, si rahisi kwa wateja wengi kutambua kuwa ni refurbished, hasa kwa sababu zinaonekana kama mpya.

Kwa mfano, kwa simu maarufu kama iPhone, unaweza kujua tofauti kwa kutumia vigezo hivi:
  • Non-Active User: Hii inamaanisha wewe ni mtumiaji wa kwanza wa simu hiyo.
  • Active User: Hii ni simu ambayo tayari imetumika na mtu mwingine kabla yako.
Kwa ujumla, si simu zote zinazokuja kwenye boksi zilizofungwa (sealed) ni mpya. Hili linaonekana zaidi kwa chapa kubwa kama Apple, Samsung, Google Pixel, na Sony. Lakini chapa ndogo kama Infinix au Tecno, mara nyingi biashara yao inalenga zaidi soko la Afrika.

Kuhusu Warranty Card

Hata simu used zinazotoka Dubai, Marekani, na nchi nyingine hutolewa na warranty. Unaponunua simu, hakikisha unapewa warranty, ambayo mara nyingi huwa ya muda wa miezi 6 hadi mwaka mmoja.

Hata hivyo, kuna mambo yanayoweza kufanya warranty yako isifanye kazi:

  1. Kupitisha muda wa warranty
    Ukirudi dukani baada ya muda wa warranty kuisha, hautapata msaada wowote.
  2. Kutokurudi na warranty card husika
    Hakikisha unarudi na warranty card yako pamoja na simu. Pia, IMEI namba iliyoko kwenye warranty card lazima ilingane na ile ya simu yako. Ikiwa umepoteza warranty card, hakikisha simu yako ina stika yenye namba ya kipekee (IMEI sticker).
  3. Kufanya marekebisho kabla ya kuwajulisha wauzaji
    Simu yako ikiharibika, usiipeleke kwa fundi kabla ya kuwajulisha muuzaji.
  4. Kuharibu simu kwa makusudi
    Matukio kama simu kuanguka, kutumbukizwa majini, au kupigwa shoti kwa makusudi, yatafanya warranty yako isifanye kazi.
Ikiwa umefuata vigezo vyote, unapokwenda dukani hakikisha haukabidhi warranty card yako bila kupata msaada unaohitaji. Hiyo ndiyo dhamana yako.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Kabla ya Kununua Simu Used au Refurbished

1. Fanya utafiti kuhusu simu unayotaka kununua
Jua sifa za simu unayotaka kununua, kama ukubwa wa kioo, uwezo wa betri, na teknolojia za mtandao (network compatibility). Usinunue simu kwa ushawishi wa rafiki bila kujua uwezo wake halisi.

2. Linganishha bei za simu sokoni
Tafuta wastani wa bei ya simu hiyo kwa kufanya utafiti kutoka kwa wauzaji 4-5. Epuka kununua simu kwa bei ya chini kupita kiasi au bei kubwa isiyo na msingi.

3. Jua historia ya muuzaji
Chunguza mitandao ya kijamii ya muuzaji, maoni ya wateja waliowahi kuhudumiwa, na jinsi anavyoshughulikia matatizo. Epuka wauzaji wa barabarani au wale ambao akaunti zao hazioneshi uwazi wa biashara yao.

4. Usijifanye mjuaji
Wauzaji wa simu mara nyingi wana uzoefu mkubwa. Jifanye hujui ili upate maelezo ya kina kuhusu bidhaa wanazouza.

Kwa mfano, mteja anaweza kutaka kununua iPhone 11 mpya, lakini akijulishwa kuwa Apple wameacha kutengeneza model hiyo haelewi. Wauzaji wengine wasio waaminifu wanaweza kumuuza iPhone refurbished kwa bei ya simu mpya.

5. Jipange kabla ya kununua simu
Unapotoka nyumbani, hakikisha unajua aina ya simu unayotaka, bei yake ya wastani, duka gani utaenda, na muuzaji unayemwamini. Pia, kuwa na mpango mbadala (plan B) iwapo hautapata simu uliyoikusudia.
Hii itakuepusha na kushawishiwa kununua simu za barabarani ambazo mara nyingi si za kuaminika.

Mimi ni BARAKA MKISI, muuzaji wa simu na laptop hapa Kariakoo, Mtaa wa Aggrey. Kama umependa makala hii, nitafute WhatsApp kupitia namba 0628210865. Nitakuunganisha kwenye kundi maalum linalotoa elimu ya simu na teknolojia bure.

Tuma neno NIUNGE kwa namba 0628210865 sasa hivi ili ujifunze zaidi! 🀝
 
Mkuu
Mkuu unavyosema kwa mfano nimekwambia nataka iPhone 11 mpya na wewe unanijib iPhone hawa tengenezi mpya unakua hamjaelewa Kampuni inaweza ikatengeneza bidhaa mfano iphone 12 lakini zikawa bado zipo hazijaisha kwenye stocks zao ukiziitaji unazipata sass kwanini unasema hakuna simu za iphone 12?
 
Note , kampuni inatoa simu na inajua idadi yake mfano copy laki 1 wanauza zikiisha kama itakua hawatoi tena model hio kwenye official page yao watakuandikia kabisa discontinued au o means hapo huyo mtu kweli akae na flagship dukan mpka ishindikane kuuzwa kwa muda huo mfano 12 uje uipate leo kweli?Inawezekana kibongo bongo mfano ukienda mitandao ya simu kama tigo utaikuta wanaiuza mpya ila sasa bei si ajabu ukakuta sawa na 14kwa sasa je utaenda wapi
 
sawa je hizi tunazoambiwa ni used kutoka Dubai ni used kweli au copy za simu original?
 
Niunge Kwa no 0764102565
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…