Muhimu ya kuzingatia katika kuchagua rangi za kupaka kwenye nyumba yako

Muhimu ya kuzingatia katika kuchagua rangi za kupaka kwenye nyumba yako

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ukuaji wa teknolojia umeongeza kwa kasi mabadiliko katika ujenzi wa nyumba zetu miaka ya nyuma wengi walipaka rangi cream au nyeupe kwa ndani tofauti na siku hizi ambapo rangi huchanganywa kwa teknolojia ya kisasa ya kutumia kompyuta na kupelekea kuongeza wigo mpana wa uchaguzi wa rangi za kupaka ndani na nje ya nyumba zetu.

Muhimu kuzingatia ni kuwa rangi hizi zinazong’aa kwasana mfano rangi ya machungwa “Orange” zinapendeza kupakwa katika ukuta mmoja tu kwa ndani na kwingine zinabaki rangi zisizo na kelele yaani zilizotulia zaidi.

kwenye vyumba vya watoto wa kiume wengi hupendelea blue wakati kwa wakike pink,purple na rangi ya machugwa “orange” au rangi ya kijani “green” hupendeza zaidi.

Utakapohitaji kununua rangi za nyumba yako ni muhimu kujua ni rangi ipi ipo katika wakati, siku hizi rangi hata gypsum zinapendeza ukiweka tofauti na nyeupe kama wengi walivyozoea.

_MG_8599.JPG


4e16417ea6b93.JPG


4d7f956b8555ac55c207042b79cbefbd.jpg


Chanzo; Hivisasa blog
 
Back
Top Bottom