Muhimu: Zijue athari za kuondoa thermostat kwenye gari yako

duh afadhali kuna bwege mmoja nusu aniingize mkenge kisenge yan kuhusu iyo ishu ya kutoa thermostat..nikamwambia hii imekaa hapa kwa sababu walioweka sio wajinga

Ni vizuri ulifanya hivyo mkuu. Na hata ikitokea siku ikaleta shida basi funga tu nyingine ila usiitoe jumla.
 
yah ilibidi nipambane nikafunga mpya tu

Yaani kitu ambacho hakimake sense ni kwamba kama kifaa kilikuwepo na mtu alikuwa anatumia gari bila shida, Kwanini kinapoleta shida kiondolewe na kisiwekwe kingine?
 
Shukrani sana Mkuu yaani umeeleza vizuri sana....
dah mkuu ulichokisema ndicho kimenikuta, mwaka 2017 nilinunua noah sr40 showroom ikiwa vizuri sana but baada ya miezi minne ikawa inachemsha sana, nikampelekea fundi akasema kuchemsha kunasababishwa na thermostat so tuitoe, akaitoa gari ikawa vizuri kwa wiki tu ikaanza kuchemsha tena nikampelekea akaunga radiator fan ikawa inazunguka na engine wakati wote, ikapelekea gari kubadili behaviour ikawa inakula wese sana japokuwa tatizo limekwisha.

sasa mkuu naomba ushauri nini nifanye ili gari irudi kama zamani, kumbuka thermostat haipo na fan inazunguka muda wote
 

1. Rudisha thermostat kwa maana thermostat ikiharibika inatakiwa kuwekwa nyingine na siyo kuondolewa.

2. Radiator fan pia irudishwe kama zamani ilipokuwa inawaka na kuzima.

Kama kutakuwa na tatizo basi hilo tatizo liangaliwe wakati hayo mawili yakiwa tayari yamesharekebishwa.
 
Asante mkuu nitafanya hayo ubarikiwe sana
 
Dah....umeniokoa mleta mada......gari yangu coolant kila baada ya wiki inaisha kuna fundi nikaongea nae akaniambia niende atoe hiyo thermostat....ndo nlikua najipanga niende....

Kazi ya thermostat ni kuhakikisha engine inafanya kazi katika joto linalotakiwa.

Sasa kwa akili ya kawaida kabisa thermostat haiwezi kuwa inapelekea maji kupungua kwenye rejeta. Na hivyo kuiondoa hakutaondoa hilo tatizo bali ni kuongeza matatizo mengine ambayo ni makubwa.

Angalia kama radiator fan zinazunguka na pia jaribuni kutafuta kama kuna sehemu kuna leak ambayo inapelekea maji kuvuja.
 
Mkuu kwema mimi nina kirikuu jamaa alitoa thermostat sasa toka niitoe gari inashake/ vibrate sana hasa wakati nataka kuiwasha wakati mwingine unawasha gari inawaka ila ina vibrate mpaka inazima tena
 
Mkuu kama wameshaitoa sasa naweza kupata nyingine mpya nikairudishia aina ya gari ni Suzuki Carry cabreta
 
Asante,
Naendelea kufuatilia,ngoja tusubiri na utetezi wa wale wanaomini kwanini thermostat inapaswa kutolewa
Gari ya mzee ilitolewa thermostat miaka 10 iliyopita ila mpaka leo ipo vizuri na haina tabia ya kuchemsha wala haijawahi kubadilishwa na huwa inaenda safari ndefu
 
Mkuu kwema mimi nina kirikuu jamaa alitoa thermostat sasa toka niitoe gari inashake/ vibrate sana hasa wakati nataka kuiwasha wakati mwingine unawasha gari inawaka ila ina vibrate mpaka inazima tena

Sometimes gari ikiwa inamiss huwa inavibrate...
 

Atakuwa ashaingiliwa sana kwenye mafuta bila kujua.
 
Tuna shida kubwa ya mafundi wa magari kiasi mm sio fundi but i wish to start my own Garage
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…