Mshua's
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 804
- 553
Heshima kwenu wakuu! Naomba kufahamishwa kama mtumishi wa umma aliyehitimu masomo katika chuo kikuu huria (Open University) anaweza kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuta kwa kuunganisha bila kukaa miaka mitatu kama utaratibu unavyosema? Natarajia kuhitimu degree yangu mwaka huu katika chuo kikuu huria na nina mpango wa kuunganisha kuchukua masters mwaka huu baada ya ku-graduate. Utaratibu ninaoufahamu ni kuwa, wahitimu wa "Campus" huambiwa wafanye kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu ndipo waendelee na masomo kwa ngazi nyingine au kuacha kazi ili waajiriwe sehemu nyingine. Sasa, sijajua kama na wahitimu wa Open University huwa wanatakiwa wakae miaka 3 kazini ilihali walikuwa wanasoma wakati wakifanya kazi bila kuathiri utendaji kazi katika maeneo yao ya kazi. Naomba kujuzwa kwa anaye fahamu.