Muhitimu wa Open University anaweza kuendelea na masomo 'consecutively' kwa waajiriwa wa Seikalini?r

Mshua's

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2013
Posts
804
Reaction score
553
Heshima kwenu wakuu!

Naomba kufahamishwa kama mtumishi wa umma aliyehitimu masomo katika chuo kikuu huria (Open University) anaweza kuendelea na masomo kwa mwaka unaofuata kwa kuunganisha bila kukaa miaka mitatu kama utaratibu unavyosema?

Natarajia kuhitimu degree yangu mwaka huu katika chuo kikuu huria na nina mpango wa kuunganisha kuchukua masters mwaka huu baada ya ku-graduate nikiwa nje ya kituo changu cha kazi. Utaratibu ninaoufahamu ni kuwa, wahitimu wa "Campus" huambiwa wafanye kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu ndipo waendelee na masomo kwa ngazi nyingine au kuacha kazi ili waajiriwe sehemu nyingine. Sasa, sijajua kama na wahitimu wa Open University huwa wanatakiwa wakae miaka 3 kazini ilihali walikuwa wanasoma wakati wakifanya kazi bila kuathiri utendaji kazi katika maeneo yao ya kazi.

Naomba kujuzwa kwa anaye fahamu.
 
Kaka umesoma kihuria. Ulisoma huku unafanya kazi. Ruhusa kuunganisha.
 
Fanya kazi kwanza, achana na kuunga. Kumba hata hiyo degree uliyopata ni ya kimagumashi tu!
 
Kaka umesoma kihuria. Ulisoma huku unafanya kazi. Ruhusa kuunganisha.

Mkuu nashukuru kwa ushauri wako! Lakini kama kuna uthibitisho wowote unaomruhusu graduate wa 'OUT' kuendelea na masomo unaweza ukautupia hapa ili tuweze kujiridhisha
 
Fanya kazi kwanza, achana na kuunga. Kumba hata hiyo degree uliyopata ni ya kimagumashi tu!

Majibu hayo yanaonesha jinsi tabia yako ilivyo ambayo haiendani na mwonekano wa jina lako. Please, binadamu tuwe wastaarabu jamani tunapomjibu mwenzetu humu jamvini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…