Muhoozi Kainerugaba anataka kuanza kumkamua mkosoaji wake utumbo.

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328

Mwana wa Museveni, Muhoozi Kainerugaba, anachapisha picha za mtu huyo akiwa karibu uchi, mtu ambaye amewatuma watu wake waovu wa Gestapo kumteka nyara, na anasema kwamba atampiga kwa fimbo tumboni.

Kumbukumbu: Muhoozi bado anaendelea kuwashawishi baadhi ya watu wanaomwamini kwamba yeye ni Mkristo. Nashangaa, hii ni aina gani ya Ukristo? Baadhi yao wanataka awe Rais wa Uganda. Wanajikunja na kujitahidi kwa kila namna kutetea vitendo vyake ambavyo haviwezi kutetewa. Inasikitisha!
 
https://www.facebook.com/
View: https://www.facebook.com/share/v/1DZGivFQsU/
 
Huyu jamaa huwa anapiga mikwara Tu na hawa ni watu wake
 
Moja Kati ya makosa makubwa Nyerere alifanya maishani mwake kumsaidia Museveni kuchukua utawala wa nchi ya Uganda.

Kosa la pili kuiuwa Tanganyika sababu ya kutaka muungano ufanikiwe aonekane amemshinda Kwame Nkrumah hoja ya kuunganisha Afrika kwa kuanzia nchi jirani regional integration.
 
Hapana mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Nyerere hakuhusika kabisa na Museveni kunyakua madaraka nchini Uganda kwani ambaye Museveni alikuwa anapigana kumwondoa madarakani alikuwa ni Obote ambaye Nyerere alimrejesha madarakani kwa damu za watanzania.

Pili, Nyerere alikuwa mtu mmoja mwenye kupenda sana sifa kwa mfano; alitoa watanzania kafara ili asifiwe kama mpigania uhuru wa Afrika; alitengeneza historia ya Tanganyika ili ionekane yeye ndiye aliyepigania uhuru wa Tanganyika wakati waanzilishi wa harakati za uhuru walikuwa ni wazee wa kiislamu wa mikoa ya Pwani.

Aliua kabisa elimu nchini Tanzania kwa kuogopa kwamba wasomi wangemsumbua kutawala na baadaye kuipindua serikali yake ya kiimla.

Alitengeneza mfumo ambapo yeye aliabudiwa kama Mungu na kuleta msemo kwamba "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti", nk nk.
 
Mama Sa100 ateua jaji toka Uganda kwenye tume ya Jaji Lali.
 
Muhoozi ni kama maji kupwa maji kujaa halafu ni mdharirishaji huwa nahisi hata babake anashindwa afanyeje tuu. Juzi tuu hapa mara Beyonce is my wife mara flat screen wote wafungwe.
 
Madaraka yamemlevya na ana tatizo la akili. Baba yake anajua lakini kwa sababu ni mtoto wake bado atafanya afanyalo awe rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…