Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Sabayi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
2,310
Reaction score
999


Habari Wakuu

Nilipitia maonesho ya nane nane mwaka huu na moja ya kilimo kilichonivutia ni kilimo cha Dengu na Conflower/Brocolli.
Mazao haya yana soko kubwa sana nje ya nchi hasa India kwa Dengu na ulaya/India kwa Conflower.

Kwa wale wazee wa kanda ya kati kuanzia Dodoma, Singida, Tabora hadi Shinyanga Dengu inakubali sana maeneo hayo sina uhakika na maeneo mengine ila nadhani Morogoro inaweza kukubali (I'm not sure) ni zao la muda mfupi.

Tuchangamkie hizi fursa ndugu zangu Tunapaswa kuwa wakulima tunaowaza kuexport mazao yetu sio kila siku tunapigana vikumbo kariakoo sokoni tu kwa mfano hii Conflower/Brocolli nimeambiwa gram 25 inauzwa 30000/= TZS sasa piga hesabu kwa ekari moja unaweza kupata kilo Kilo/Tani ngapi na unamake kiasi gani?

Naomba kuwasilisha

MUHTASARI WA KILIMO CHA MAZAO JAMII YA KUNDE

Kilimo cha zao la Choroko​

Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium.Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari.

Udongo na hali ya hewa
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.

Aina za Choroko
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.
A) Choroko zinazotambaa , hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.
B) Choroko zinazosimama, hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusimama kwenda juu.

Kipindi kizuri cha upandaji wa choroko
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.

Nafasi cha upandaji wa choroko na kiasi cha mbegu
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8)sentimeta

Samadi na mbolea ya viwanda
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.

Umwagiliaji
Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa choroko. Na palilia shamba lako mapema kuzuia magugu kuota ndani ya shamba lako na kwa palizi moja inaweza kutosha.

Magonjwa ya Choroko
1-yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
Dalili- mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.

2-Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.

Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).
anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi.

3-Leaf spot (Vidoti katika majani)
Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.
Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.

Wadudu
Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu baada ya mimea kuota, dawa kama karate, twigathoate, dimethote na nyinginezo zinaweza kutumika.

Uvunaji
Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe ukichelewa zitapukutikia shambani.
 
Mkuu hii bei ya hi conflower imenishitua, yani gram25 ni ths30,000?au typing error? So inamaana gram 250 ambayo ni robo kilo in ths 300,000 right?so kilo 1 ni ths 1,200,000. Ikiwa utalima heka1 na ukapata 100hks inamaana una 120million right?

Ebu fafanua mkuu juu ya bei.
 
Dengu ni zao potential sana, linatumika ktk kutengeneza biskuti na chokoleti nadhani. Ni kweli nami nina taarifa lina soko zuri sana hasa katika viwanda vya kutengeneza biskuti sio India tu hata hapa Nchini na nchi jirani katika Afrika Mashariki.

Mkuu na mimi nimefikiria kulima hili zao, na hapa nipo katika mchakato wa kupata eneo huko wilaya ya Chemba, Dodoma.
Tuendelee kutumia thread hii kuelimishana juu ya kilimo cha zao hili na masoko yake.
 
Habari zenu wana jamii, nimejitokeza kutaka kupata msaa kwa undani kwa mtu anafahamu kilimo cha Dengu,

1. Mbegu za dengu zinapatikana wapi?
2. Matayarisho yake yaweje.
3. Namna za kuzipanda ikiwemo nasafi kutoka shins moja mpaka jingine, na umbali kutoka mstari mpaka. Matunzo yake zikiwa shambani.
4. Zinachukua muda gani tangu kupandwa mpaka kuvunwa.
5. Soko lake likoje.
 
Sabayi,

Kwenye hiyo Mikoa ongeza mkoa wa Mwanza na hasa Wilaya ya Missungwi. Ni kilimo kinachomuokoa Mkulima Mdogo baada ya zao la Pamba kuuawa. Ni zao linalilimwa baada ya Wakulima kuwa wamevuna Mazao mengine kama Mahindi, Maharage na Mpunga. Ni zao lisilohitaji Mvua nyingi (kwa uzoefu, sio utaalamu). Hivi sasa kuna Mbegu bora kabisa zilozotolewa na Taasisi zetu hapa hapa kama Ukiriguru, n.k.

Dengu ina Soko kubwa sana hapa Nchini ukiachilia Nje ya Nchi. Ukulima Oyee!:smiling:
 

Juzi nimepita kutoka Shinyanga kwenda Mwanza hapo kupitia Old Shinyanga nimeona wakulima wengi sana wamepanda Dengu.
 
Juzi nimepita kutoka Shinyanga kwenda Mwanza hapo kupitia Old Shinyanga nimeona wakulima wengi sana wamepanda Dengu.

Ni ukweli usiopingika. Mwezi uliopita nilikwenda Kwimba na Missungwi, Wilaya za Mkoa wa Mwanza zinazopakana na Shinyanga. Nilipata nafasi ya kuongea na Wakulima kadhaa. Ninadiriki kusema kuwa huenda Dengu ndilo Zao la Biashara linalioongoza na linalowapa Wakulima matumaini kizidi mengine katika Wilaya hizo mbili.

Kwenye Nane-Nane ya Mwaka jana hapo Nyamhongolo, Mwanza nilioneshwa Mbegu mpya (hybrid) iliyotafitiwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru ambayo ni bora kuliko mbegu za kienyeji. Kwa ufupi Dengu, kama ilivyo Choroko, Mbaazi, Ufuta, n.k., ni fursa nyingine katika Kilimo!
 

Uzuri ni kwamba wanapanda dengu wakishavuna mahindi/mpunga na haitaki mvua au maji mengi.
 
Vipi kilimo cha dengu mkoa wa morogoro jaman kinakubali!? Choroko inasitawi vizuri
 
Wadau napenda kufahamu soko la mbaazi,kunde na choroko daresalamu maana ninampango nianze biashara hiyo kwa kununua choroko kutoka mtwara na kusafirisha dar naitaji mwenye ufahamu wa soko na hata changamoto zake
 
Hey guys, mimi ni mgeni lkn ni mwenyeji Sana kwa kupita humu ndani nimekuwa nafuatilia michango ya akina Malila na wenzie Muda mrefu, Sasa safari hii nimelima mihogo na choroko Tanga maeneo ya Marungu natarajia kuvuna mwezi wa 6 mwishoni mkae mkao wa kula Insha Allah
 
Mkuu mambo hayakuwa mazuri Sana ndege walizishambulia sana mlinzi wangu hakuwa makini kwenye ulinzi, hata hivyo choroko ilikuwa ni nyongenza tu kilimo kikuu kilikuwa ilikuwa ni zao la mihogo limekubali sana January natarajia mavuno mazuri tu mlio tayari nawakaribisha marungu Tanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…