JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
116 wakamatwa Mwanza kwa kuratibu maandamano
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewakamata watu 116 wanaodaiwa kuhusika kuratibu maandamano yanayotarajiwa kufanyika Desemba 9, yakitajwa kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani, huku likisisitiza kuwa maandamano hayo yamekatazwa rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari Desemba 6, 2025 katika kituo kikuu cha Polisi Nyamagana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa amesema upelelezi dhidi ya washukiwa unaendelea sambamba na kuimarishwa kwa doria ili mkoa ubaki salama.
Aidha, Mutafungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwazuia vijana kushiriki maandamano hayo na badala yake siku hiyo itumike kuadhimisha kumbukizi ya Uhuru wa Tanzania, akisisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kulinda usalama wa wananchi na kuzuia madhara ya vurugu kama zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameendelea kuhoji kama kufanya maandamano ni kosa hasa inapotokea yanafanywa na wapinzani au wananchi ambao wanapingana na Serikali, wakati katiba imeruhusu. Wanasema hali hii inazidi kuongeza chuki kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na inaweza kuchagia wananchi kulipiza visasi kutokana na ukiukwaji wa haki unaofanywa kwa muda mrefu na vyombo hivyo bila ya hatua kuchukuliwa.
Wengine wameona ukamataji huo kama mbinu ya kuwatisha wasijitokeze kwenye maandamano, ambapo wamesema hilo haliwatishi, watajitokeza kuandamana na kama walivyotangazwa.
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania: Waislamu msiende kuandamana Disemba 9
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuber, amewataka Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutumia fursa walizonazo nje ya mipaka ya Tanzania kuchangia maendeleo na ujenzi wa uchumi wa taifa, badala ya kuchochea au kuunga mkono vitendo vinavyoweza kuvuruga amani na utulivu wa nchi. Amesisitiza kuwa amani ndiyo nguzo muhimu ya maendeleo, na bila mshikamano wa kitaifa, juhudi za maendeleo haziwezi kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Aidha, Mufti amewasihi Waislamu kote nchini kutojihusisha na maandamano ya Disemba 9 yanayoweza kuhatarisha amani, akiwataka waepuke uchochezi na chuki za kidini. Ameeleza kuwa Uislamu unahimiza kuishi kwa wema na watu wa dini zote, kulinda maisha ya wananchi na kudumisha umoja wa kitaifa. Amewaomba viongozi wengine wa dini kuendelea kuwaelimisha waumini wao umuhimu wa amani na utulivu nyakati zote.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamemtuhumu Mufti kama viongozi wengine wa kiislamu ambao wamekuwa wakitoa matamko, kutumika na Serikali katika kukwamisha juhudi za wananchi kudai haki nchini. Wamesema tamko lake halitazuia watu kuandamana kwasababu Watanzania wamekataa kugawanywa kwa udini, wakisisitiza kuwa ‘Gen Z’ hawana dini!
Msigwa: Serikali haiwezi kutishwa na CNN, tumejipanga kwa ulinzi wakati wote. Hatutaifungulia X mpaka tukubaliane…
Akizungumza katika mahojiano na mwandishi Edwin Odemba, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameonesha kuwa kauli yake ya hivi karibuni kuhusu Serikali ya Tanzania kutekeleza miradi kwa fedha zake imepotoshwa. Amesisitiza kuwa hakumaanisha kama ilivyochorwa au kusambazwa na baadhi ya watu, bali kauli hiyo imefanyiwa imegeuzwa (spinning). Pia ameeleza umuhimu wa waandishi wa habari kuzingatia kanuni na misingi ya taaluma, ikiwemo kusikiliza na kuzingatia pande zote kabla ya kuchapisha taarifa.
Kuhusu matukio ya Oktoba 29 na siku zilizofuta, Msigwa amefafanua kuwa ‘vurugu’ hizo zilisababisha vituo 672 vya mafuta kuchomwa moto huku mmiliki mmoja akipoteza vituo 33. Ameeleza kuwa idadi hiyo ni ile ile iliyotolewa na Waziri Mkuu, licha ya taarifa tofauti zinazosambaa kwenye vyombo vya habari. Msigwa amesisitiza kuwa vyombo vya usalama viko tayari kuhakikisha usalama wa wananchi, mali zao, na mipaka ya nchi siku zote.
Kuhusu Uhuru wa Habari na CNN, Msigwa ameeleza kuwa mwandishi wa chombo kikubwa cha habari kama CNN hawezi kutengeneza makala kwa kukusanya picha na video kupitia WhatsApp na ni kinyume na taaluma kufanya habari bila upande mwingine kupewa nafasi. Amesiisitiza kuwa Serikali ya Tanzania hawakupewa nafasi ya kueleza upande wao na kwamba wao hawawezi kutishwa na CNN. Ameongeza kuwa mwandishi Larry Madowo ametakiwa kufuata weledi wa kazi yake kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma katika kuwasilisha taarifa.
Aidha, Msigwa amesisitiza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuhubiri amani na upendo, badala ya kutoa matamko yanayoweza kuashiria uchochezi. Pia, ameeleza kuwa mtandao wa kijamii Twitter (X) utafunguliwa pale ambapo itakapokubaliana namna jukwaa hilo litakavyoendeshwa nchini Tanzania kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Maoni ya wananchi:
Wengi wamemkosoa Msigwa na Serikali kushindwa kutoa majibu kuhusu makala ya CNN wakijificha kwenye kisingizio cha kutopewa nafasi ya kujitetea.
Wengine wamesema wanaiamini zaidi ripoti ya CNN kuliko Serikali au hata Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na Rais, inayotarajiwa kutoa ripoti yake karibuni kutokana na historia ilivyowafunza kuwa Serikali siyo ya kutegemewa kutoa taarifa za ukweli kwenye matukio yanayohusu maslahi ya umma. Pia, wameongeza kuwa Larry alitoa ripoti hiyo kwa kuwasaidia Watanzania kupaza sauti zao baada ya waandishi wa ndani kuminywa kuripoti taarifa hizo.
Kuhusu takwimu za vituo vya mafuta kuchommwa moto, wananchi wameendelezea kuonyesha sintofahamu zao kutokana na Serikali kusema vituo zaidi ya 600 huku taarifa ya wamiliki wa vituo hivyo ikisema ni vituo 41 pekee ndivyo viliathiriwa. Wanasema ni mbinu inayotumiwa kuwapa lawama wananchi na pengine kutumia mwanya huo kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu. Wameendelea kuikosoa Serikali kwa kutotaja idadi ya waliopoteza maisha huku wakiwa na taarifa zote za uharibifu wa mali uliotokea, wakionyesha kuthamini zaidi vitu kuliko uhai wa mtu.
Kuhusu kufungwa kwa mtandao wa X (zamani Twitter) nchini, wengi wamesema utetezi wa uwepo wa ‘maudhui ya ngono’ unatumika kama kisingizio tu, lengo lenyewe likiwa ni kuzuia wananchi kuikosoa Serikali sababu wanajua hawana udhibiti wa mtandao huo kama ilivyotokea kwa Meta waliokubali kufunga akaunti za wanaharakati.