JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Kanisa Katoliki lafanya misa takatifu kuombea waliofariki wakati wa Uchaguzi Mkuu, wasisitiza hakuna amani bila haki
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amesema haki ndiyo msingi wa amani, akisisitiza kuwa amani haiwezi kupatikana bila haki.
Akizungumza Novemba 10, katika Misa Takatifu ya kuombea waliofariki wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Tanzania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Dar es Salaam, Askofu Ruwa’ichi aligusia hali ya taifa kufuatia matukio ya wiki ya uchaguzi, akibainisha kuwa matendo ya watu kuuawa kiholela yamepoteza heshima ya taifa.
Maoni ya Wananchi:
Wananchi wengi wamelipongeza Kanisa Katoliki kutokana na tamko hilo huku wakionyesha fahari yao kuwa Wakatoliki, wakisifu ujasiri wa Askofu Ruwa’ichi kwa kusema ukweli na kusimama upande wa haki na utu, hasa baada ya matukio ya mauaji kwenye maandamano. Pia wamesisita uwajibikaji kwa wale wote wanaohusika kwenye mauaji hayo.
Rais Samia awateua Bashiru Ally, Dorothy Gwajima na wengine wanne kuwa wabunge
Rais Samia amewateua Dorothy Gwajima, Balozi Mahmoud Kombo, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Omar na Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Wabunge wa Bunge la Tanzania.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa Novemba 10, na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, ambapo Rais amebakiwa na nafasi 4 za uteuzi huu wa wabunge kati ya 10 kama katiba inavyompa mamlaka.
Maoni ya Wananchi:
Wananchi wengi wamekejeli uteuzi huo wakidai Serikali inaendelea kufanya uteuzi huku damu za watu zikiwa zimemwagika nyingi na haitoi kauli yoyote. Pia wengine wamehoji kama Tanzania ina Serikali ama ni maigizo tu!
Kesi ya uhaini ya Lissu yaahirishwa hadi Novemba 12, 2025, Jamhuri yasema usalama haujatengemaa Dar es Salaam
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, iliyopangwa kuendelea Jumatatu, Novemba 10, imehairishwa hadi Jumatano, Novemba 12, itakapotajwa tena Mahakamani hapo, huku ikiwa mshtakiwa huyo hajafikishwa mahakamani.
Aidha, upande wa Jamhuri walitakiwa kuleta mashahidi wanne, lakini wakasema kutokana na hali ya Jiji la Dar es Salaam kutokuwa kwenye utulivu, mashahidi wao kutoka mikoa ya Ruvuma na Mbeya wameshindwa kusafiri kwenda Dar es Salaam.
Maoni wa Wananchi:
Wananchi wahoji kuwa usalama unakosekana tu kwenye kesi ya Lissu lakinbi kwenye shughuli nyingine pamoja na utalii amani na utulivu unakuwepo? Kama Dar hakuna amani kwanini Serikali imetoa matamko kuwa hali na shwari na shughuli kurejea kama kawaida?
Wengi wameona hili kama njia ya Jamhuri kusogeza kesi mbele bila sababu za msingi ili kumpotezea muda Lissu sababu mpaka sasa hakuna ushahidi wowote mzito uliowasilishwa unaoonyesha Lissu alifanya uhaini.
Balozi mbalimbali nchini zatoa salamu za pole kutokana na vifo wakati wa uchaguzi
Balozi mbalimbali nchini zimeendelea kuonyesha masikitiko yao na kutoa pole kufuatia vifo vya raia, majeruhi na wote walioathirika kutokana na matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Balozi hizo; Denmark, Norway, Finland, na Sweden, zimesisitiza umuhimu wa haki, maridhiano na uwajibikaji wa pamoja ili kujenga jamii yenye umoja.
Maoni ya Wananchi:
Wengi wamewapongeza kwa msimamo wao hasa kwenye msisitizo wa haki, na kuongeza japokuwa balozi na taasisi za nje ya Tanzania zimeendelea kutoa pole na kukosoa uchaguzi uliofanyika, serikali haijali chochote na kuendelea na majukumu kama hakuna kilichotokea.
Uhamiaji: Hatuwanyang’anyi Watanzania wanaorejea nchini ‘Passport’ pamoja fedha, ni uzushi
Idara ya Uhamiaji imetoa tamko kukanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni, zikidai kuwa Watanzania wanaorejea nchini kutoka nje wananyang’anywa pasi za kusafiria na fedha zao wanapowasili kwenye viwanja vya ndege au vituo vya kuingia nchini, na kisha kulazimishwa kwenda kufanyiwa mahojiano makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Dodoma.
Uhamiaji imeeleza kuwa madai hayo ni ya uzushi na upotoshaji wenye lengo la kuleta taharuki kwenye jamii, ikisisitiza kuwa Watanzania wanapaswa kupuuza taarifa hizo.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wameonyesha kutokuwa na imani na maelezo ya Idara ya Uhamiaji wakidai taasisi za serikali mara chache hukiri tuhuma, wakitilia shaka ukweli wa taarifa za kukanusha.
Baadhi walidai kuwa wamewahi kushuhudia au kusikia visa vya watu kunyimwa pasipoti, huku wengine wakihusisha hoja hiyo na kutokuwepo kwa uwazi na uaminifu serikalini wakikumbushia tukio la hivi karibuni ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche alipokonywa pasi yake na hajarudishiwa mpaka sasa.
Mara: 29 wafikishwa Mahakamani wakihusishwa na vurugu siku ya uchaguzi, jumla yafikia 492 nchi nzima
Watu 29 wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama ya kutenda jinai na uhaini. Hati ya mashitaka inadai kuwa kati ya Machi na Oktoba 30, 2025, walipanga njama za kuzuia uchaguzi mkuu, kutishia uongozi wa nchi, na kusababisha uharibifu wa mali za serikali.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wameendelea kuonyesha hasira na kutoamini mamlaka za nchi, wengi wakiona mashitaka ya uhaini yakitumika kupambana na wapinzani kisiasa au kuwatisha wananchi wanaodai haki zao.
Wengine wameuliza kwa nini serikali haiwashitaki wale wanaohusishwa na matumizi ya nguvu dhidi ya raia na kusababisha vifo.
Mlinzi wa Lissu adaiwa kuvamiwa na Polisi na kutokomea naye kusikojulikana
Kulingana na chapisho la mwanachama wa CHADEMA, Hilda Newton katika mtandao wa X, wanaodhaniwa kuwa polisi waliovaa kiraia walivamia nyumba ya mlinzi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu, ndugu Charles Hangaya, katika eneo la Bunju ‘A’ kisha kumchukua, na hajatambulika walimpeleka wapi.
Tukio hilo linaripotiwa kuwa lilitokea usiku wa kuamkia Novemba 10, 2025.
Maoni ya Wananchi
Wengi wameonyesha hofu na hasira, wakisema nchi inaelekea kubaya kutokana na matukio haya ya uhalifu kuwa ya kawaida bila mamlaka kuonyesha juhudi zozote za kukabiliana nayo.
Wengine wahoji sababu za mlinzi huyo kuchukuliwa tena kwa njia zisizo rasmi ikiwa Lissu ameshikiliwa gerezani muda mrefu, na kutilia mkazo kuhusu wananchi kujilinda wenyewe wakisema ndio njia pekee ya kujiweka salama wakati huu.
Polisi wazikataa video za mauaji kipindi cha maandamano, wadai zinaweza kuwa zimetengenezwa
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, ameiambia Idhaa ya Kiswahili (DW) kwamba video za mauaji zinazozunguka mtandaoni zinazodaiwa kurekodiwa wakati wa maandamo yaliyofanyika wakati wa uchaguzi Oktoba 29, zinaweza kuwa zimetengenezwa na watu wenye nia ya kupotosha akidai Polisi kwa nyakati fulani wamewahi kufanyia uchunguzi baadhi ya video zilizodaiwa kuchukuliwa kwenye baadhi ya maeneo nchini wakabaini hazikuwa na uhusiano wowote na maeneo husika.
Maoni ya wananchi
Wananchi wamepinga vikali kauli ya Muliro, wakisema kuwa video hizo ni halisia na kwamba mauaji hayo yameathiri maisha ya watu wengi.
Wengine wameilaumu Polisi kwa kupoteza miili ya marehemu kwa makusudi ili kuficha ushahidi, wakidhani wananchi hawatakuwa na rekodi ya matukio hayo ya kikatili, lakini pia misiba inayofanyika mtaani ikiwemo ya watu maarufu inathibitisha kuwa video hizo za mauaji ni halisi.
Mbunge Mteule Viti Maalum CHAUMMA, Sigrada: Sijafurahia kuwa Mbunge wakati watu mtaani wanazika wenzao
Mbunge mteule wa Viti Maalum kupitia CHAUMMA, Sigrada Mligo, ameeleza kutofurahia uteuzi wake wa ubunge wa Viti Maalum, akidai kuwa kwanza alinyang’anywa ushindi wa ubunge wa jimbo baada ya kuibiwa kura, lakini pia hajafuraia uteuzi huo kutokana na kuwa Taifa linapitia kipindi kigumu kutokana na vifo vingi vilivyotokea wakati wa uchaguzi ambapo wananchi wengi mtaani wapo kwenye majonzi ya kuzika ndugu zao huku serikali ikiwa kimya.
Maoni ya wananchi:
Wananchi wengi wameonyesha mshangao kutokana na kauli ya Mligo, wakibainisha unafiki wake wa kuonyesha kutoridhika huku akikubali kuapishwa, wakisema kama kweli hajafurahishwa na uteuzi huo basi ajiuzulu vinginevyo atakubali nafasi hiyo kwa maslahi yake binafsi.
TLS, THRDC na LHRC kutoa msaada wa kisheria kwa walioshtakiwa Uhaini kutokana na matukio ya Oktoba 29
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeanzisha msaada wa kisheria bila malipo kwa watuhumiwa waliokamatwa au kufunguliwa mashtaka kuhusiana na matukio ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, kwa kushirikiana na mashirika ya haki za binadamu THRDC na LHRC.
Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi, amesema msaada huu unalenga kuhakikisha uwakilishi wa kisheria kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Msaada wa Kisheria ya 2017, hasa kwa watuhumiwa kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha.
Mawakili zaidi ya 40 wameorodheshwa kutoa msaada katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Iringa, Njombe, Kilimanjaro, Mwanza, Songwe, Mbeya, na Mara. Familia zinaweza pia kuajiri mawakili wao binafsi, lakini msaada wa TLS unalenga kuhakikisha utetezi sahihi bila vizuizi vya kifedha.
Maoni ya wananchi
Wananchi wampongeza TLS na mawakili wa taasisi hizo nyingine kwa jitihada za kutoa msaada wa kisheria bure kwa vijana hao wakisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuhakikisha haki inatendeka na kudumisha uwakilishi wa kisheria.
Wengi wameonyesha kuwa msaada huu unaleta faraja kwa watuhumiwa wasio na uwezo wa kifedha na familia zao hasa ikizingatiwa kuwa tuhuma hizi zinachukuliwa kama njia ya serikali kukwepa uwajibikaji.
Ian Khama: Simtambui Samia kama Rais wa Tanzania
Rais wa zamani wa Botswana, Ian Khama, amesema hamtambui Rais Samia kama kiongozi halali wa Tanzania, akidai kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 ulitawaliwa na vitisho, mauaji na ukandamizaji wa wananchi, hali iliyozuia demokrasia ya kweli.
Aliongeza kuwa changamoto kama kuzimwa kwa mtandao, vurugu za waandamanaji na ripoti za waandamanaji waliouawa mikono ya polisi, pamoja na ukosefu wa uwazi kwa vyombo vya habari, ziliathiri uhalali wa uchaguzi.
Khama aliyasema hayo katika maadhimisho ya mwaka wa pili ya Pan-Africanism katika Chuo Kikuu cha Lukenya, Kaunti ya Makueni nchini Kenya.
Maoni ya Wananchi:
Wengi wameonyesha kumuunga mkono Khana, wakimpokesha kwa kusimama kwenye ukweli bila kupindisha maneno dhidi ya viongozi wa Afrika na hasa kwa Rais Samia kutokana na kuwa dhahiri kuwa uchaguzi huu wa 2025 haukuwa wa uhuru na haki, huku wakiongeza hata wao hawamtambui Samia kama Rais wa Tanzania hata kama ameapishwa na kuanza majukumu yake.