JF Summary
Senior Member
- Jul 3, 2015
- 163
- 109
Mawakili Mwabukusi na Mpoki wahojiwa kwa makosa ya ‘kuhamasisha maandamano ya Desemba 9 kwa Lengo la Kuvunja Muungano’
Jana, Novemba 12, Wakili Mwandamizi, Mpale Kaba Mpoki alipokea wito kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kawe akitakiwa kufika Kituo cha Polisi Mbweni leo Novemba 13.
Akiwa na mawakili wake, akiwemo Rais wa TLS Boniface Mwabukusi, Dkt. Rugemeleza Nshala, Paul Kisabo na Fredrick Msaki, waliwasili kituoni na kuelezwa kuwa anatakiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Walipofika, Kamanda wa Upelelezi wa Kanda aliwaeleza kuwa yeye Mpoki pamoja na Mwabukusi (aliyekuwa hapo kama Wakili wa Mpoki) wanahusishwa na tuhuma za kuhamasisha maandamano ya Desemba 9 kwa lengo la kuvunja Muungano. Baada ya mahojiano na ufafanuzi, wote waliruhusiwa kuondoka bila masharti yoyote.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameendelea kukosoa Polisi na vyombo vingine vya ulinzi ‘kushughulikia’ watu wanaodai haki kutokana na athari za maandamano ili kutisha wananchi waache kuhahakisha wote waliohusika wanawajibika.
Baadhi ya wananchi wanahoji ‘Muungano upi, wakati Wazanzibari na Wabara wote hawautaki?’ Lakini pia, wengine wamehoji kuna kosa gani ikiwa mtu anataka kuvunja muungano mpaka aitwe Polisi kuhojiwa kuhusu hilo?
Aidha, wengine wamesema uhuru wa maoni unazidi kuminywa nchini Tanzania, kumatwa na Oolisi inakuwa jambo la kawaida pale unapohoji jambo linalokinzana na Serikali.
LHRC: Wafanyakazi wetu wamevamiwa na kunyang’anywa vitendea kazi usiku wa Novemba 12
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimetoa taarifa ya wafanyakazi wake wamevamiwa usiku wa Novemba 12, wakati wakiendelea na majukumu yao katika Hoteli ya Whitesands iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hoteli yote ilizingirwa na kikosi kilicholenga moja kwa moja timu ya LHRC, ambapo simu na kompyuta mpakato za wafanyakazi hao zilichukuliwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa asubuhi ya Novemba 13, 2025, wafanyakazi hao wameitwa kuhojiwa.
LHRC imelaani vikali tukio hilo na kueleza kuwa imesikitishwa sana na hatua hiyo, ikisisitiza kuwa matendo kama hayo yanahatarisha uhuru wa taasisi pamoja na usalama wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania.
Maoni ya wananchi:
Wengi walio wengi wameonyesha wasiwasi kuwa, ikiwa taasisi kubwa kama hiyo (LHRC) wanavamiwa kihuni hivyo, vipi kwa mwanachi wa kawaida? Huku wengine wakisema hatua niyo imekuja baada ya taasisi hiyo kutoa Mawakili kwaajili ya kuwatetea wale waliokamatwa wakihusihwa na “ugaidi” pamoja na “unyang’anyi wa kutumia silaha” wakati wa maandamano Oktoba 29.
Hatua hii imezidi kuitia doa Serikali hasa baada ya uwepo wa taarifa kuwa Serikali yenyewe inahitaji kufanya maridhiano.
Mwigulu athibitishwa Kuwa Waziri Mkuu, aanza kwa kuonya watumishi wavivu na wala rushwa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya baada ya jina lake kupendekezwa na Rais Samia na kuwasilishwa bungeni Novemba 13.
Mara baada ya kuthibitishwa, Nchemba alitoa hotuba fupi akisisitiza uwajibikaji, uwazi na nidhamu kwa watumishi wa umma, akiwaonya wavivu, wazembe na wala rushwa.
Aidha, alieleza kuwa asilimia 8 ya Watanzania bado wanaishi katika umaskini wa kupindukia. Dkt. Nchemba anatarajiwa kuapishwa Novemba 14, saa 4 asubuhi Ikulu ya Chamwino, Dodoma.
Maoni ya wananchi:
Wengi wameonyesha kutoridhishwa na uteuzi wake wakimhusisha na tuhuma za ufisadi zilizowahi kumkabili alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Wengine wanasema kama alipokuwa Waziri wa Fedha alisema wananchi wanalalamikia tozo ya kwenye miamala ya simu wahamie Burundi, sasa amekuwa na cheo kikubwa zaidi, hali itazidi kuwa mbaya kwa wananchi.
Polisi wamkamata mwanachama wa CHADEMA kwa tuhuma za ‘kuhamasisha uhalifu kupitia kundi la WhatsApp’
Jeshi la Polisi limemkamata na linaendelea kumshikilia Ambrose Leonce Dede, mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya African Safari na mwanachama wa CHADEMA, kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha uhalifu kupitia kundi sogozi la WhatsApp linalojulikana kama 'Sauti ya Watanzania'.
Mtuhumiwa alikamatwa eneo la ‘Njia Panda ya Makiungu’, Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida, na ushahidi unaodaiwa kukusanywa na Polisi unaonesha kuwa yeye pamoja na wasimamizi wengine wa kundi hilo (Group Admins) wanashirikiana na baadhi ya watu waliopo nchini na wengine nje ya mipaka ya nchi.
Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi na kuwataka wananchi kuepuka kujiingiza katika makundi ya mtandaoni yanayoendeshwa na watu waliopanga na wanaoendelea kupanga ‘kufanya uhalifu kwa kivuli cha maandamano ya amani’ au ‘sababu nyingine’, kwani huo ni uhalifu na hatua za kisheria zitachukuliwa.
Maoni ya wananchi:
Wananchi walio engi wanalaani kitendo hicho wakisema kuhamasisha maandamano si kosa kisheria kama Polisi wanavyodai wakihoji kwanini mpaka sasa hawajawakamata waliofanya mauaji wakati wa maandamano?
Aidha wengine wameonyesha wasiwasi wao kwamba hatua hizi zinaashiria jitihada za kudhibiti uhuru wa wananchi kufanya mambo yao kwenye mitandao ya kijamii.
Zitto: Tanzania imejeruhiwa vibaya, ukweli lazima usemwe, ufanyike uchunguzi huru wa kimataifa
Aliyekuwa kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, amelaani vikali mauaji yaliyotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiyaita “Mauaji ya Oktoba” na kuyalinganisha na tukio la “Tiananmen Square”.
Katika andishi lake Novemba 13, Zitto alisema damu ya Watanzania wasio na hatia imemwagika, huku akitaka uchunguzi huru na wa kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa au Umoja wa Afrika, uwajibikaji wa waliohusika, kuanzishwa kwa mazungumzo ya kitaifa ya maridhiano na uandikaji wa Katiba Mpya, na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kujiuzulu mara moja.
Maoni ya Wananchi:
Wengi wamebaki na msimamo wa kutokuwa na imani nayenja chama chake, wakisema kitendo cha wao kushiriki uchaguzi huo kimehalalisha matukio ya mauaji ya Oktoba 29. Wananchi wanaona sasa Zitto na wenzake wanatafuta fursa ya kutumia mauji yaliyotokea kwa manufaa yao baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi.