Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Muigizaji Rami Malek ameshinda Oscar kwa kucheza nafasi ya Freddie Mercury katika filamu inayoitwa, "Bohemian Rhapsody."
Nashangaa si watu wengi wameguswa na ushindi huu unaohusu filamu hii ya Freddie Mercury aliyezaliwa Zanzibar na kwa aina yake kaifanya Zanzibar izidi kufahamika.
Leo nyumba alimozaliwa Freddie Mercury na sehemu nyingine zinazomuhusu vimekuwa sehemu za kuvutia watalii wanaofika Zanzibar.
Siwezi kuwalaumu watu wasiomjua Freddie Mecury kwani mimi pia sikuwa namjua hadi siku moja usiku kiasi miaka 30 ishapita niko chumbani kwangu najitayarisha kulala mwanafunzi mwenzangu jina lake Panothiakis akawa anaupiga mlango wangu kama vile nyumba inaungua moto na anataka nitoke nje nisalimishe maisha yangu yangu.
''Mohamed Freddie Mercury is dead...'' nasikia akiniambia kutoka nje ya mlango wangu.
Kwa haraka nikafungua mlango, Panos kama tulivyomzoea kumwita amesimama anatweta, ''Mohamed Freddie Mercury is dead," karudia kusema.
Kwa kweli mimi simjui Freddie Mercury. ''Panos who is Freddie Mercury."
You don't know Freddie Mercury?''
Mshangao wa rafiki yangu Panos ulikuwa mkuwa na niliona sura yake ilivyokuwa na mfadhaiko.
Alitingisha kichwa na kwanza kabisa akaanza kwa kunifahamisha kuwa Freddie Mercury ni mwanamuziki mkubwa wa kikundi kinachoitwa Queen na kazaliwa Zanzibar akisisitiza neno, ''Zanzibar.''
Panos akajiondokea zake kurudi chumbani kwake.
Nikafungua TV na hapo ndipo nilipojua umaarufu wa Freddie Mercury kwa zile rambirambi zilivyokuwa zikiingia na watangazaji kueleza maisha yake na muziki wake.
Lakini nilikuja kumjua Freddie Mercury vizuri nikiwa Zanzibar na rafiki yangu Dr. Harith Ghassany.
Dr. Ghassany alinipa historia ya Freddie Mercury kwa utulivu na kunipitisha kwenye nyumba ambayo aliishi akiwa mtoto kabla hawajahama Zanzibar.
Turejee kwa Panos.
Siku nyingine tena akanigongea kunipa taarifa muhimu.
Kagonga mlango wangu na nilipomfungulia akaniambia kuwa kuna taarifa kwenye TV kuwa Magic Johnson amegundulikana kuwa ameathirika na AIDS.
Nilikuwa kimya namwangalia Panos sahib wangu. Nadhani aliona kuwa sura yangu ilikuwa, ''tupu,'' yaani blank.
Simjui Magic Johnson.
Panos kwa upande wake alikuwa kimya akiniangalia.
Nilipotulia kutoka katika ule mshagao wangu nikamuuliza sahib yangu mleta habari muhimu kwangu Panos, ''Who is Magic Johnson?''
Habari za filamu kuhusu maisha ya Freddie Mercury na kuwa filamu hii muigizaji wake amepatatuzo ya Oscar nimeiona kwenye post moja aliyoweka Dr. Ghassany mtandaoni.
Lakini naamini sote tunaijua nyimbo ya Queen, "We Will Rock You."
Huyo ndiye Mzanzibari Freddie Mercury.
Panos alipatapo kuniuliza kama namjua muigizaji Anthony Queen nikamjibu ndiyo.
Kisha akaniuliza kama namjua George Foundas.
Nakamjibu namjua.
Panos akaniambia kuwa huyo ndiye baba yake.