Mukoko Tonombe anukia Azam FC

Mukoko Tonombe anukia Azam FC

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Mukoko.jpeg
Imeelezwa kuwa kiungo wa kazi aliyewahi kucheza ndani ya Yanga, Mukoko Tonombe yupo kwenye rada za mabosi Azam FC ili kuweza kuinasa saini yake.

Nyota huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao waliweza kufanya vizuri ndani ya Yanga msimu uliopia wakati timu hiyo ilipomaliza ikiwa nafasi ya pili.

Pia alikuwa kwenye kikosi ambacho kiliweza kutinga hatua ya Fainali ya Kombe la Shirikisho na ikapoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Simba.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, ni bao la Taddeo Lwanga kupitia pasi ya Luis Miquissone liliweza kuipa ushindi Simba.

Habari zinaleza kuwa mabosi Azam FC wameanza mazungumzo na kiungo huyo ili kuweza kumrejesha kwa mara nyingine Tanzania.

Aliposepa ndani ya Yanga kwa makubaliano maalumu kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.



Source: East Africa
 
Inasikitisha mno Azam FC ,club yenye kila kitu ya kuwa top club hapa Africa inaishia kupigana kuwa kwenye first division na sio to chase the cups, ubora wa Azam FC ungeondoa ukiritimba wa Simba na yanga nchini, ningependa viongozi wa Azam FC wangefanya study tour pale Mamelodi Waone Sundown aka Masandawana wamepatia vipi,chief na pirates wamepotezwa kabisa,5th consecutive wamechukua ubingwa wa SA na wana star moja kwenye jersey zao.pls Azam FC you can do better than this
 
Back
Top Bottom