Muleba: Afungwa Jela miaka 3 kwa kupokea Rushwa ya Tsh. 250,000

Mkuu nahisi ume exaggerate hapo kwenye "15,000" kushindwa kupatikana kwenye ukoo mzima.
Siku hizi watu kama wanazo hawakupi na wakishaona umepiga simu kuomba mchango wanajua baada ya hio 15K huenda zikafuatia nyingine ndogo ndogo hivyo usishangae watu hawapokei simu au wengine wanakulia timing ukipiga tu wanakuwahi na kukupa matatizo yao....

Acha Mkuu we live in very dangerous times...., Hard Times, Getting Worse by the Day..., Wakati baadhi wachache hawajui hata pa kuzipeleka pesa na kila wanavyozitumia ndio zinavyoongezeka maradufu..., wengine wengi wakiamka asubuhi jioni hawajui hata kama mkono utakwenda kinywani..., Na watu wa hivyo huenda Ukoo ukipata SMS zao unajua ni mzinga hivyo kutokupokea simu...

Sasa jiulize watu wa hivyo ni wazembe (huenda kipindi cha kuwa na shamba na ilikuwa ni kuchukua tu jembe na kwenda kwenye ardhi na baada ya kuvuna kula mwaka mzima - ungewaita wazembe), Au kipindi cha ajira zenye ujira, ambapo mtu anapata ujira wa kumuwezesha kumaliza mwezi lakini anaamua kuzipiga pombe na kuzitawanya huyo alikuwa mzembe;

Ila zama hizi ambazo hata mbegu unahitaji kwanza pesa na ardhi tupu ya kukodi na kutupia vimbegu vyako huku ukisubiri betting ya mvua zinyeshe; watu wa aina ya mdau aliowasema wanaongezeka by the day.....
 
Rudia kusoma wenda hujanielewa wala sio kwamba sijui uhalisia wa maisha ila ndugu jaribu kupanua akili kuhusu muda ndipo utanielewa ila nje na hapo utatamani kunipiga mawe tu kwa kitu cha kikaa chini na kupiga mahesababu yasiyohitaji mahesabu ya log!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…